Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sababu ambayo Kristo hakumwokoa Yohana

  Watu wengi huwaza kuwa kwa nini Yohana Mbatizaji aliachwa asumbuke na kufia gerezani. Lakini jambo hili la giza haliwezi kutikisa imani yetu kwa Mungu, tunapokumbuka kuwa Yohana alikuwa mtumishi wa Mungu, na mshiriki wa mateso ya Kristo. Wote wanaomfuata Kristo watavaa taji ya kujikana nafsi. Shetani atafanya vita na kanuni hii ya kujikana nafsi popote inapoonekana.TVV 122.1

  Shetani amekuwa akishughulika kumfanya Yohana Mbatizaji awe mtu wa kujipenda nafsi, akashindwa. Katika majaribu ya jangwani Shetani alishindwa. Na sasa alikusudia kumhuzunisha Kristo kwa njia ya kumshambulia Yohana kiajabu. Mtu yule aliyeshindwa kumvuta dhambini, alimletea mateso.TVV 122.2

  Yesu hakuingilia kati na kumwokoa mtumishi wake. Alijua kuwa Yohana atavumilia jaribu hilo. Mwokozi angemfariji katika gereza ili asiwe na wasiwasi. Lakini hakutaka kuhatarisha kazi yake mwenyewe. Yohana ilimpasa anywee kikombe cha namna hiyo, kwa ajili ya watu maelfu watakaofuatana, na kunywea kikombe cha mauti. Sisi kama wafuasi wa Kristo, tulalamike tunapotiwa gerezani, na kukabili mauti? Inapoonekana kuwa kana kwamba tumeachwa na Mungu mawazo Yohana aliyokuwa nayo gerezani, hatuwezi kuyakumbuka,?TVV 122.3

  Yohana hakuachwa na Mungu. Malaika wa mbinguni walikuwa wenzake, waliomufunulia unabii kumhusu Kristo na maandiko matakatifu. Kwa Yohana, na kwa wengine watakaofuata ahadi husema: “Tazama mimi nipo pamoja nanyi mpaka mwisho, wa dunia.’ Mathayo 28:20.TVV 122.4

  Mungu hawaongozi watu wake kinyume cha matakwa yao. Kama wangaliona mwanzo mpaka mwisho, kwamba wanatimiza jambo liwapasalo watenda kazi pamoja naye. Si Enoka aliyehamishiwa mbinguni, si Eliya aliyepazwa mbinguni bila kufa, kwamba walimzidi Yohana, aliyefia gerezani. “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, siyo kuamini tu, bali hata na kuteseka pia.” Wafilipi 1:29. Wote wapewao vipawa vya mbinguni, kuteswa na Kristo ni thamani kubwa.TVV 122.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents