Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  24 — “Je, Huyu Siye Mwana wa Seremala?”

  Kuvuka ng’ambo ya kazi ya furaha na siku za mafanikio za Kristo huko Galilaya, kulikuwa na wasiwasi kama kivuli katikati ya mwanga, yaani ni watu wa Nazareti walimkataa. Walisema: “Je, huyu siye mwana wa seremala?” Mathayo 13:55.TVV 126.1

  Wakati wa ujana wake, Yesu alikuwa akishiriki kuabudu pamoja na ndugu zake katika sinagogi la Nazareti. Wakati alipoanza kazi yake, alikuwa haonekani hapo tena, lakini alipoonekana, matazamio yao yalikuwa tofauti. Hapo palikuwa na watu waliofahamiana tangu utoto wake. Mama yake, ndugu zake na dada zake wote wapo. Alipoingia katika sinagogi na kutafuta mahali pake kama kawaida, wote walimtazama ikiwa ni siku ya Sabato.TVV 126.2

  Katika ibada, mzee wa kanisa aliwasisitizia watu wadumu kuwa na tumaini la kumtazamia Masihi ajaye; ambaye ataleta utawala wa fahari, na kuondoa udhia wa kusumbuliwa na Warumi. Aliwakazia wasikihzaji wake wazidi kumtazamia Masihi, ambaye kuja kwake kunakaribia. Aliwaambia kuwa atakuja na mamlaka ili kuwakomboa Waisraeli.TVV 126.3

  Wakati Rabi alipokuja, alikuwa akitazamiwa kuhubiri na Mwisraeli fulani asome maandiko ya unabii. Kwenye Sabato hii Yesu alikuwa ndiye mhubiri. “Alisimama ili asome, naye alipewa chuo cha Nabii Isaya” Fungu alilosoma lilieleweka kuwa linamhusu Masihi:TVV 126.4

  “Roho ya Bwana ni juu yangu. Kwa sababu amenitia mafuta ili niwahubiri maskini Injili.TVV 126.5

  Amenituma niwaponye waliovunjika moyo; kuhubiri kufunguliwa kwa wafungwa; kuponya macho ya vipofu, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.”TVV 126.6

  Akakifunga chuo akampa msimamizi akaketi chini, macho ya watu wote waliokuwa katika sinagogi yakamtazama.... Wakamshuhudia wote, wakiyasta-ajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.”TVV 126.7

  Yesu akiyaeleza maneno aliyosoma, akanena kuhusu Masihi kama msaidizi wa wenye dhiki, mponyaji wa wenye kuteswa, mponyaji wa vipofu, na mfunua nuru ya Kweli, Uwezo wa maneno yake uliowasisimua, ambavyo hawajaona. Mawimbi ya mvuto wake wa kimungu ulivunja kila kipingamizi. Kadiri walivyosisimuka kwa ajabu, waliitikia, amina, na kumsifu Bwana.TVV 127.1

  Wakati Yesu aliposema kwamba: “Andiko hili leo limetimizwa masikioni mwenu, mara moja kwa ghafla walikumbuka madai anayodai huyu aliyewahubiri. Wao wakiwa watoto wa Ibrahim wamesemwa kuwa wamo utumwani, kwamba ni wafungwa wanaohitaji kufunguliwa kutoka katika nguvu za Shetani, kwamba wamo gizani wakihitaji nuru ya kweli ya Mungu. Kiburi chao kiliguswa. Kazi ya Yesu kwao ilikuwa kinyume cha matazamio yao. Matendo yao lazima yachunguzwe kikamilifu. Walijikunyata kutoka katika macho yao dhahiri yanayochunguza.TVV 127.2

  Waliuliza wakisema: “Yeye huyo ni nani?” Huyu anayedai utukufu wa Masihi alikuwa mwana wa seremala. Walikuwa wanafahamiana na ndugu zake na dada zake. Walimwona akipanda na kushuka milimani akiwa katika shughuli za kazi ya useremala. Walijua maisha yake na kazi yake, wamemwona na kufahamu alivyokua toka utotoni mpaka ukubwani. Ijapokuwa maisha yake yalikuwa matakatifu, wasingalikubali kuwa ndiye Masihi aliyeahidiwa. walifungulia mlango wa mashaka, na mioyo yao ikawa migumu zaidi, na Shetani akajitahidi kuwafunga wasiweze kuamini.TVV 127.3

  Dhamiri zao ziliwasadikisha kuwa, ni yeye Mwokozi aliyehubiri. Lakini Yesu aliwathibitishia kuwa ni yeye wa kurungua mioyo yao. “Hakuna nabii anayekubaliwa kwao na katika nchi yake mwenyewe. Lakini nawaambia yaliyo ya kweli kuwa, kulikuwa na vijana wengi katika Israeli katika siku za nabii Eliya, wakati mbingu ilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, kulipokuwa na njaa kuu katika nchi, na Eliya hakutumwa kwa mmoja wao, ila huko Zerefath katika nchi ya Sidoni kwa mmoja aliyekuwa mjane. Na kulikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli, katika siku za nabii Elisha, wala hakuna aliyetakasika, ila Naamani mtu wa Shamu.”TVV 127.4

  Watumishi waliotumwa na Mungu hawakuruhusiwa kufanya kazi kwa watu wagumu wasioamini. Katika siku za Eliya, Waisraeli walikuwa wamewakataa watumishi wa Bwana kabisa. Kwa hiyo Mungu aliwapatia watu wake maficho katika nchi za watu wa mataifa, kwa mwanamke mshenzi ambaye hakuwa katika hesabu ya watu wa Mungu. Lakini moyo wa mwanamke huyu ulifunguka ili apokee nuru kuu kutoka kwa nabii wa Bwana, ambayo ililetwa na nabii wake.TVV 127.5

  Kwa njia ile ile, katika siku za Elisha, wenye ukoma katika Israeli walipitwa. Lakini Naaman, jemadari wa Shamu, mtu wa mataifa ya kishenzi, alipokea neema ya Mungu.TVV 128.1

  Hakuponywa ukoma peke yake, ila alipata baraka ya kufahamu Mungu wa kweli. Watu wa mataifa waliochagua njia njema kadiri ya ujuzi wao, huwa katika upendeleo wa Mungu zaidi ya watu wanaojidai kuwa ni watumishi wa Mungu, bali hawajali kufuata njia ya nuru, na katika maisha yao ya kila siku wakienda kinyume na maungamo yao.TVV 128.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents