Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  27 — Mwenye Ukoma wa Kwanza Kuponywa na Kristo

  Katika magonjwa yote yaliyojulikana huko Mashariki, ukoma ulikuwa ugonjwa mbaya mno. Hali yake ya kutoponyeka, na jinsi unavyoambukiza, na matokeo yake kwa mgonjwa, yote huufanya uwe wa kutisha sana. Kwa Wayahudi ukoma ulikuwa unahesabiwa kuwa ni adhabu ya kutenda dhambi, yaani adhabu ya Mungu; kwa ajili ya dhambi.TVV 141.1

  Mwenye ukoma alifungiwa nje ya makao ya watu, akawa sawasawa na mtu aliyekufa. Kila kitu alichogusa kilichohesabiwa kuwa kichafu. Pumzi yake iliichafua hewa. Mtu yeyote aliyetuhumiwa kuwa ana ugonjwa wa ukoma, alipaswa kujionyesha kwa kuhani. Kama kuhani akiona kuwa ni ukoma, basi hutoka kwa watu wazima, akaenda kuishi na wenye ukoma. Sheria hiyo ilikuwa ya lazima, kwa kila mtu mtawala na raia pia.TVV 141.2

  Mwenye ukoma alipaswa kubeba laana hiyo, akitengwa mbali, na jamaa zake na rafiki zake pia. Ilimpasa kutangaza habari za ugonjwa ili kuwahadhari watu wengine kwa kupiga makelele na kusema: “Mchafu! mchafu!” Kelele za kilio cha huzuni cha kuwaonya watu, kilikuwa ndicho kionyesho kwamba kuna hatari.TVV 141.3

  Habari za Kristo na kazi yake zilienea mahali pengi pa matuo ya wagonjwa hawa, na kuwaletea matumaini. Lakini tangu siku za Elisha jambo la kutakasa wenye ukoma halikusikika tena, wala kujulikana. Kulikuwa na mtu mmoja ambaye alianza kuwa na imani. Walakini angalimfikiaje Mponyaji huyo? Je, Kristo angeweza kumponya? Je, kama akiona kuwa ugonjwa wake ni adhabu kutoka kwa Mungu, asingalimlaani?TVV 141.4

  Mwenye ukoma akafikiri mambo yote aliyosikia juu ya Yesu. Hakuna mtu aliyemtaka amsaidie, akafukuzwa. Mgonjwa huyu alikusudia kutafuta mponyaji. Labda wataweza kukutana naye njiani, au akiwa katika kufundisha watu, au uwandani nje ya mji. Hilo ndilo lilikuwa tumaini lake tu.TVV 141.5

  Mwenye ukoma aliongozwa kwa Yesu, akamkuta akifundisha watu, kando ya ziwa. Mwenye ukoma akiwa anasimama mbali, aliweza kusikia maneno machache ya Kristo. Alimwona akinyosha mikono yake juu ya mgonjwa fulani, aliyekuwa kilema. Akaona tena kipofu, na mwenye kupooza. Akaona na wafu wakifufuka, na kusimama, hali wakimsifu Mungu, kwa ajili ya kuponywa. Akapata imani, akasogea karibu. Akazuiliwa asimwendee akijisahau alivyo, alitazamia kupona tu.TVV 142.1

  Alionekana kuwa kioja; mtu wa kuchukiza. Watu walipomwona walitawanyika kumpisha, huku wakipiga makelele. Wengine walijaribu kumzuia asimfikie Yesu. Lakini hakuwajali. Alimwona Mwana wa Mungu peke yake. Akimsogelea Yesu, alijitupa miguuni mwake, huku akipaza sauti na kueema: “Bwana ukitaka waweza kunitakasa.” Yesu akajibu: “Nataka, takasika.” Akaweka mkono wake juu yake.TVV 142.2

  Mara moja badiliko likatokea kwenye ukoma. Mwili wake ukatakasika, akawa mwenye afya, mishipa yake na misuli ikaimarika. Makovu katika uso wake yakatoweka. Ngozi nyororo kama ya mtoto mchanga ikatokea.TVV 142.3

  Kristo akamwagiza asimwambie mtu jambo hilo. Yesu akamwambia: “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe vitu vile Musa alivyoagiza kutolewa, ili kuwa ushuhuda kwako.” Kama kuhani angalijua maana yake, chuki yao kwa Kristo ingelitulia. Yesu alitaka mtu huyu afike hekaluni kabla uvumi wa kumponya haujawafikia. Hivyo uamuzi wa kawaida ungefikiwa, na mtu huyu angeruhusiwa kurudi katika jamaa yake. Mwokozi pia alijua kuwa kumponya mwenye ukoma kulikuwa kukizunguzwa popote na kwamba wenye ukoma wengine watakuja, na kelele zitapigwa kwamba watu wanatiwa unajisi kwa ajili ya wakoma wengi wanavyokuja. Wakoma wengi wasingaliona kuwa huu ni baraka mkubwa kwao na kwa wengine. Na kwa kuwa wakoma wengi wangemjia bila kushika utaratibu waliopewa angeshitakiwa kuwa anavunja sheria ya kuzuia wakoma. Na mahubiri yake yangevurugwa.TVV 142.4

  Makutano waliona kuponywa kwa mwenye ukoma, nao walitaka kujua jinsi makuhani watakavyosema juu ya jambo hilo. Mtu huyu aliporudi kwa jamaa zake, kulikuwa na furaha na hoihoi kubwa sana. Hakuzidi kunyamaza kuhusu kuponywa kwake. Maana hakuelewa kuwa kutangaza jambo hilo kungefanya makuhani na wazee wakaze nia juu ya kumwangamiza Yesu. Mtu aliyeponywa alifurahi kwa ajili ya kupona na kurudi katika jamii ya wengine, na ilikuwa vigumu kuacha kumsifu Tabibu aliyemponya. Lakini kitendo chake hicho, kilisababisha watu waendelee kumjia Yesu, hata ikamlazimu kukomesha kazi yake kwa muda.TVV 142.5

  Kila kitendo cha Kristo katika kazi yake kilikuwa na kusudi lake. Alitumia kila njia ya kuwanyamazisha makuhani na wazee wasimlaumu kama mvunja sheria au kawaida. Alipomtuma mwenye ukoma kwa makuhani alitaka kuwaziba vinywa wasiseme kuwa hafuati kanuni. Mafarisayo walidai kuwa Kristo ni mvunja sheria, lakini alivyomwagiza wenye ukoma kwenda kujionyesha kwa kuhani na kutoa sadaka, vilionyesha kuwa madai ya Mafarisayo siyo ya kweli. Kristo alionyesha kuwa aliwapenda watu na kuheshimu sheria, na ana uwezo juu ya dhambi, magonjwa, na mauti.TVV 143.1

  Makuhani hao hao walimtenga mwenye ukoma na jamii, ndiyo waliomthibitishia kuwa amepona kabisa, akarudishwa katika jamii. Alilitukuza jina la Yesu kwa shangwe kuu. Makuhani walipewa nafasi ya kuujua ukweli. Wakati wa kazi ya Kristo, makuhani walijali kidogo sana, lakini baada ya kupaa kwake mbinguni, “hesabu kubwa ya makuhani waliitii kweli.” Matendo 6:7.TVV 143.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents