Mapatano Yaliyofanywa na Ushenzi
Kwa hivyo Shetani aliazimia kupigana vita vikali zaidi na mamlaka ya Mungu. kwa kutia bendera yake katika kanisa la Kikristo. Kama wafuasi wa Kristo wangeweza kudanganywa na kuongozwa kumwasi Mungu, ndipo nguvu yao na uthabiti wao ungepungua, na wangeshindwa kwa urahisiVK 11.1
Adui mkuu sasa alijitahidi kufanya kwa hila jambo lile aliloshindwa kufanya kwa nguvu. Mateso yalikoma, na badala yake yalikuja mashawishi ya kimwili yenye hatari ya kutamanisha watu kama fanaka na heshima ya kidunia. Watu waliokuwa wakiabudu sanamu walivutwa kupokea sehemu ya imani ya Kikristo, na huku walikana mambo mengine yaliyokuwa ya muhimu sana. Walijidai ya kwamba walimkubali Yesu kama Mwana wa Mungu, na kuamini juu ya kufa na kufufuka kwake lakini hawakuchomwa mioyoni na kujua ya kwamba ni wenye dhambi, kwa hivyo hawakuona ya kwamba wana haja ya kutubu na kugeuka mioyoni. Wakristo kwa mambo mengine, waliwashauri Wakristo ili wao pia wapate kuwaridhisha kwa mambo yao mengine. kusudi wote waungane katika kumwamini Kristo.VK 11.2
Sasa kanisa liliingia katika hatari kubwa zaidi. Kufungwa gerezani, kutcswa, kuunguzwa kwa moto na kuuawa kwa panga kulikuwa kama mibaraka zikilinganishwa na hatari hii ya baadaye. Wakristo wengine walisimama imara, wakisema ya kwamba hawawezi kufanya upatanisho na dini ya kishenzi. Wengine walisema ya kwamba wakijitoa au kubadili kidogo mambo makubwa ya imani yao, na kuungana na wale waliopokea sehemu tu ya Ukristo, labda kwa njia hiyo wangewavuta hata waongoke mioyo kabisa. Ulikuwa wakati wa maumivu makuu ya rohoni kwa wafuasi waaminifu wa Kristo. Kwa njia ya watu waliojifanya kuwa ni Wakristo, Shetani alijiingiza pole pole katika kanisa, kusudi kuipotosha imani yao na kugeuza fikara zao kutoka kwa ukweli.VK 12.1
Hatimaye wingi wa Wakristo walishusha kipeo chao cha kanuni za dini, na wakafanya umoja fulani kati ya Ukristo na Ushenzi. Ingawa waabuduo sanamu. walijidai kuwa wamegeuka, na kuungamana na kanisa, lakini waliendelea kuishikilia ibada ya sanamu, ila tu walibadilisha vitu walivyoabudu, vikawa sanamu michoro ya Yesu, hata na ya Mariamu na wafu walioheshimiwa. Chachu hii mbaya ya ibada ya sanamu, baada ya kuingizwa hivi kanisani, iliendelea na kazi yake ya uharibifu. Mafundisho yasiyo ya kweli, urembo wa ibada kama ya mambo ya ushirikina, na kawaida na ibada za sanamu ziliingizwa katika mafundisho na ibada za dini. Wafuasi wa Kristo walipoungamana hivi na waabuduo sanamu, dini ya Kikristo ilichafuliwa na kanisa lilipoteza utakatifu na uwezo wake. Walakini, kulikuwa na wengine ambao hawakupotoshwa na madanganyifu haya. Walishikilia uthabiti wao kwa Yeye mwenye kweli, wakamwabudu Mungu peke yake.VK 12.2
Tangu awali, wale wanaojiita kuwa ni wafuasi wa Kristo wamekuwa wakigawanyika makundi mawili. Kundi moja la watu wakijifunza juu ya maisha ya Mwokozi kwa moyo, na kijibidisha sana kusahihisha maisha yao na kumfuasa Kristo, mfano wao; kundi la pili la watu huyadharau mafundisho yaliyo dhahiri na ya kweli kwa kuwa huyafunua makosa yao. Hata katika siku za usitawi, si kwamba watu wote waliokuwako kanisani walikuwa wenye haki, wenye mioyo safi, waaminifu. Mwokozi wetu alitoa fundisho ya kwamba wale ambao hufanya dhambi kwa kusudi wasikubaliwe kuingia kanisani; walakini, Yeye mwenyewe aliungamana na watu waliokuwa wapotovu kwa tabia zao, wapate kusaidiwa na mafundisho yake na kwa mfano wa maisha yake, kusudi wapate nafasi ya kusahihisha maisha yao.VK 13.1
Lakini hakuna umoja kati ya Mkuu wa nuru na mkuu wa giza, wala wafuasi wa wakuu hawa wawili hawawezi kupatana. Wakristo walipokubali kuungana na watu waliokuwa wamegeuka nusu tu kutoka kwa ushenzi waliingia katika njia iliyowatenga mbali na haki ya Mungu na mbali zaidi. Shetani alisimanga kwa vile alivyopata kuwadanganya wafuasi wengi wa Kristo. Ndipo Shetani aliendelea kuwaongoza zaidi, hata aliwatilia nia ya kuwatesa wale waliodumu kuwa wenye haki kwa Mungu. Hakuna ajuaye namna ya kushindana na imani ya kweli ya Kikh3risto kama wale waliokuwa wakiipigania mara ya kwanza; na hawa Wakristo waliomwasi Mungu, kwa kuungana na wenzao waliokuwa nusu washenzi, walianza kufanya vita na mafundisho ya Kristo yaliyo ya muhimu zaidi.VK 13.2
Wale ambao walitaka kuwa waaminifu, iliwapasa kushindana vikali sana, wakisimama imara na kujihadhari na madanganyifu na machukio yaliyofunikwa na mavazi ya kikasisi na kuletwa katika kanisa. Biblia haikukubaliwa kuwa upeo wa imani. Mafundisho ya uhuru wa kuwa mfuasi wa dini yo yote biia kuzuiwa na sheria yaliitwa uzushi, na wale walioyafuata walichukiwa na kugombezwa.VK 14.1