Kujiondoa kwa Waaminifu
Baada ya mashindano makali yaliyoendelea kwa muda mrefu, watu wachache waaminifu waliazimia kuutangua ushirika wote uliokuwa kati yao na kanisa lililoasi ikiwa litaendelea kukataa kuondoa madanganyifu na ibada ya sanamu. Waiiona ya kwamba utengano ulikuwa ni lazima kama wakitaka kulitii Neno la Mungu. Waliona ya kwamba wakitaka kulitii Neno la Mungu hawana budi kujitenga. Hawakuweza kamwe kukubaliana na mambo ya uongo yaliyohatarisha roho zao wenyewe, na kuweka mfano ambao ungehatarisha imani ya watoto wao hata wajukuu wao. Makusudi wawe na amani na umoja walikuwa tayari kukubali jambo lo lote lililohusiana na uaminifu kwa Mungu; lakini waiiona ya kwamba kupata amani kwa njia ya kutupa mambo ya asili ya dini ingekuwa vigumu kwao. Kama umoja usingekuwako, ila kwa njia ya kuyatupa mambo ya kweli na ya haki basi, na uwepo utengano, hata na mashindano. Ingekuwa vyeina kwa kanisa na kwa dunia kama mafundisho yale yaliyowaongoza wale waliosimama imara yangehuishwa katika mioyo ya wale wanaojidai kuwa ni watu wa Mungu.VK 14.2
Mtume Paulo asema ya kwamba “na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.’’ 2 Tim. 3:12. Kwa nini basi, mateso yanaonekana ya kwamba yamefifia? Sababu yake tu ni kwamba kanisa limejifananisha na dunia, na kwa hivyo kanisa haiishikilit mambo ya adili yawezayo kuleta ushindani. Hali ya dini katika siku zetu haifanani kwa usafi na utakatifu na hali ya imani ya Wakristo walioishi katika siku za Kristo na mitume. Sababu yake tu ni kwamba kanisa lina hali ya kupatana na dhambi, na kwa kuwa mafundisho makuu na Neno la Mungu hayajialiwi sawa, na kwa kuwa hali ya utauwa imekuwa kidogo kanisani, ndiyo maana ya dini ya Ukristo kupendelewa na watu wa dunia. Hebu kuwcpo na huisho la imani na uwezo ule uliokuwako katika kanisa la zamani, ndipo na moyo wa kuwatesa Wakristo utakapoamshwa, na mateso makali yataanzishwa mara ya pili.VK 15.1