Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Kumi Na Sita - Mwisho Wa Rehema

    *****

    NALIONYESHWA wakati wa mwisho wa ujumbe wa malaika wa tatu. Uwezo wa Mungu uliwakalia watu wake; walikuwa wameimaliza kazi yao, na walikuwa tayari kwa wakati wa taabu uliokuwa ukiwajia. Walikuwa wameisha pata mvua ya masika, yaani kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana, na ushuhuda wa milele ulikuwa umeamshwa. Onyo kuu !a mwisho lilikuwa limetangazwa kila mahali, nalo lilikuwa Iikiwashtusha na kuwakasirisha wakaao duniani ambao hawakuukubali ujumbe huo.VK 109.1

    Naliwaona malaika wakiruka kwa haraka wakienda huko na huko mbinguni. Malaika mmoja mwenye kidau cha mwandishi kiunoni alirudi toka duniani akamwambia Yesu ya kwamba kazi yake ilikuwa imekwisha, na watakatifu wamehesabiwa wakatiwa muhuri, Ndipo nikamwona Yesu, ambaye alikuwa akihudumu mbele ya sanduku ziliinokuwamo amri za Mungu, akitupa chini chetezo cha uvumba. Aliinua mikono yake, na kwa sauti kuu alisema, “Imetimia.” Na jeshi la malaika waliziondoa taji zao walipoyasikia maneno haya mazito yakitoka kinywani mwa Yesu: “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” Ufunuo 22:11.VK 109.2

    Kesi ya kila mtu ilikuwa imeisha katwa, kwa uzima au kwa kufa. Yesu alipokuwa akihudumu katika patakatifu, hukumu ya wenye haki waliokufa ndiyo iliyokuwa ikifanyika, na ndipo baadaye ikafuata ya wenye haki walio hai. Kristo alikuwa ameupokea ufalme wake, baada ya kuufanya upatanisho kwa watu wake na kuzifuta dhambi zao. Hesabu ya raia za ufalme ule ilitimizwa. Arusi ya Mwana-Kondoo ilifungwa. Na ufalme ule na ukuu wa ufalme chini ya mbingu walipewa Yesu na warithi wa wokovu; na Yesu akaanza kumiliki kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.VK 110.1

    Yesu alipokuwa akitoka katika patakatifu mno, nalisikia mlio wa njuga katika joho lake; na alipoondoka, watu wakaao duniani wakafunikwa na wingu la giza. Ndipo hapakuwa na mpatanishi kati ya mwanadamu mvyenye dhambi na Mungu aliyekosewa. Yesu alipokuwa akisimama kati ya Mungu na mwanadamu mwenye dhambi, wanadamu walikuwa wakizuiliwa wasifanye maovu wapendavyo; lakini Yesu alipoondoka kati ya wanadamu na Baba yake, hapakuwa na kizuizi tena, na Shetani akawa na mamlaka kabisa juu ya wale ambao mwishoni walikataa kutubu.VK 110.2

    Haikuwezekana kuyamimina mapigo wakati Yesu alipokuwa akihudumu katika patakatifu; lakini kazi yake ikisha pale, naye aache kuwaombea wanadamu, hakuna jambo lo lote linaloweza kuizuia ghadhabu ya Mungu, nayo huanguka kwa ukali juu yao wenye dhambi wasio na mahali pa kukimbilia, ambao waliudharau wokovu na kuchukia kukaripiwa. Wakati ule wa kuogofya, kazi ya Yesu ikisha kukoma kama mwombezi wetu, watakatifu wataishi mbele za Mungu mtakatifu bila mwombezi. Hukumu zote zitakuwa zimekatwa, na hesabu zote za wateule wa Mungu zitakuwa zimetimizwa. Nalimwona Yesu akikawia kidogo katika chumba cha nje cha patakatifu pa mbinguni, na dhambi zote zilizoungamwa alipokuwa katika patakatifu mno ziliwekwa juu ya Shetani, mwanzishaji wa dhambi, ambaye alipaswa kuhukumiwa kwa ajili ya dhambi. *Maumivu haya ya Shetani si kwamba kufanya upatanisho kwa ajili ya wanadamu. Tukisoma katika sura fulani iliyopita, twaona ya kwamba “Kristo alikuwa badala ya wanadamu, ndiye mdhamini wa wanadamu, na dhambi zote za wanadamu zikawekwa juu ya Kristo.” Lakini baada ya kuokolewa wale wanaokubali ile dhabihu ya Kristo, ni jambo la haki ili Shetani, mwanzishaji wa dhambi, na ataabike kwa hukumu ya mwisho. Jinsi Bibi White asemavyo mahali pengine, “Kazi ya upatanishi imalizikapo katika patakatifu pa mbinguni, ndipo dhambi za watu wa Mungu zitawekwa juu ya Shetani mbele za Mungu na malaika za mbinguni, na mbele ya kundi la waliookolewa; naye Shetani atatajwa kuwa ni mwenye hatia ya maovu yote ambayo aliwaongoza kuyafanya.” — The Great Controversy, p. 658.VK 110.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents