Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Shindano Kuu Lionekanavyo

    Juu ya kiti cha enzi ulionekana msalaba; na kama picha inayopitishwa, yalionekana mambo ya jaribu la Adamu na kuanguka kwake dhambini, na hatua zote zilizofuatana katika azimio la wokovu. Kuzaliwa kwa Mwokozi kwa namna ya unyenyekevu; maisha ya udogo wake ya unyofu na utiifu; ubatizo wake katika Yordani; kufungwa kwake na majaribu yake jangwani; kazi yake miongoni mwa watu, akiwafunulia wanadamu mibaraka ilivo bora ya mbinguni; siku zake zilizojaa matendo ya upendo na rehema; kujitenga kwake nyakati za usiku akienda mlimani ili kuomba na kukesha; jinsi watu walivyomlipa fadhili zake wakimvizia kwa ajili ya wivu, chuki na kijicho; maumivu makuu aliyoyapata katika Gethsemane, akilemewa na uzito wa dhambi za walimwengu wote; kusalitiwa kwake na kuwekwa mikononi mwa kundi la wauaji; mambo ya kuogofya yaliyotendeka usiku ule; mfungwa asiyejitetea aliyeachwa na wanafunzi wake wapendwa, akitembezwa hima kwa ufidhuli katika barabara za Yerusalemu; Mwana wa Mungu akipelekwa na kudhihakiwa mbele ya Anna, akishitakiwa katika pumba la kuhani mkuu, katika jumba al hukumu la Pilato, mbele ya Herode mkali, akitukanwa na kushambuliwa, akiumizwa vibaya, akihukumiwa kufa— haya yote yatafafanuliwa dhahiri kabisa.VK 131.2

    Na hapo mbele ya makutano ya watu yatafunuliwa mambo ya mwisho katika maisha ya Kristo: Mshitakiwa mvumilivu asiye na hatia akienda kusulibishwa; Mfalme wa mbinguni akitundikwa msalabani; makuhani wenye kiburi na ghasia ya watu wakimcheka wakati wa maumivu ya kufa kwake; giza isiyo ya kawaida; dunia iliyopanda na kushuka kama mawimbi, miamba iliyopasuka, makaburi yaliyofunuka, yakionyesha wakati Mwokozi wa dunia alipofariki.VK 132.1

    Mambo yale yote ya kushtusha yataonekana jinsi yalivyotokea hapa duniani. Shetani, malaika zake, na watu wake hawatakuwa na uwezo wa kugeuka wasitazame ufafanuzi wa matendo yao. Kila mmoja atakumbuka kazi yake aliyoifanya. Herode, aliyewaua watoto wadogo wa Bethlehemu kusudi amwue Mfalme wa Israeli; Herode mwovu, ambaye kwa ajili ya ubaya wa moyo wake Yohana Mbatizaji aliuawa; Pilato mnyonge, aliyetaka kuwapendeza wakuu; askari waliokuwa wakimdhihaki Yesu; makuhani na wakuu na makutano ya watu waliokasirika na kusema, “Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu.”— Hawa wote wataona ubaya wa uovu wao jinsi unavyopita kiasi. Watajaribu kujificha mbele ya utukufu wa uso wake ambao unang’aa sana kushinda mwanga wa jua, nao watakatifu wataziweka taji zao miguuni pa Mwokozi wakisema, “Alikufa kwa ajili yangu!”VK 132.2

    Kati ya wale waliookolewa watakuwako mitume wa Kristo, shujaa Paulo, Petro mwenye juhudi, mpendwa Yohana mwenye upendo, na ndugu zao waliokuwa wanyofu mioyoni, na pamoja nao wataonekana kundi la mashahidi waliomfilia Kristo; na nje ya mji kitaonekana kila kitu kilicho kichafu, pamoja na wale watu waliowatesa mashahidi, wakiwatupa gerezani na kuwaua. Mfalme Nero, yule mkatili na mfisadi wa ajabu, atakuwapo akiwaona watu ambao aliwatesa kama sasa wameshangilia na kuheshimiwa; naye zamani alipokuwa akiwataabisha na kuwaumiza alipendezwa vibaya. Mama yake Nero pia atakuwa hapo, akiyashuhudia matokeo ya kazi yake mwenyewe kuziona tabia mbaya alizomfundisha mwana wake, na tamaa mbaya alizozikuza katika maisha ya mwana wake kwa mvuto wa matendo yake mwenyewe aone jinsi ambavyo mabaya yale yamezaa matendo ya uhalifu yaliyowashtusha walimwengu wote.VK 133.1

    Pale watakuwapo maaskofu na mapadre wa Kanisa la Kirumi ambao walijidai kwamba ni wajumbe wa Kristo, na huku waliyaleta mateso makali, wakiwatupa watu gerezani na kuwachoma moto kusudi wapate kuwatuliza watu wa Mungu. Pale patakuwako na mapapa wenye kiburi ambao walijiinua juu ya Mungu na kuthubutu kuibadili sheria yake Aliye Juu. Wale waliojiita kuwa ni kama baba za kanisa, hawana budi kutoa hesabu kwa Mungu, jambo ambalo wangetamani waachiliwe. Watafahamishwa ya kwamba Yeye Ajuaye Yote huona wivu kwa ajili ya sheria yake, na ya kwamba hatamwachilia ye yote aliye na hatia. Lakini watafahamu kwamba siku ya rehema imepita; wamekuwa wakichelewa kabisa. Watafahamu ya kwamba Kristo hujishughulisha na mambo ya watu wake wanaopotezwa; nao watayasikia maneno yake mazito, “Kadiri mlivyomtendea mmojowapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.” Mathayo 25:40.VK 133.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents