Wakati na Sheria Zabadilishwa
Kama kimekwisha kuondolewa kitu kilichoweza kuvumbua mambo ya uongo, basi Shetani aliweza kufanya apendavyo. Maneno ya unabii yalisema dhahiri ya kwamba Kanisa la Kirumi litatumaini “kubadili majira na .sheria.” Danieli 7:25. Tena halikukawia kujaribu kufanya hivyo. Makusudi kuwavuta watvi kutoka dini ya kishenzi. na kuwawezesha waongoke kwa urahisi katika dini ya Kikristo, badala ya kuabudu sanamu za kishenzi likaingizwa kanisani tendo la kusujudu picha au sanamu zilizowekwa wakfu, pamoja na makumbusho ya watakatifu wa kale. Na mwishowe amri iliyotolewa na baraza kuu (iitwayo “General Council”) ilithibitisha kawaida hii ya ibada ya sanamu katika Kanisa la Kirumi. Na kwao kutimiliza jambo hili la kukufuru na kumchukiza Mungu, Kanisa la Kirumi likathubutu kuondolea amri ya pili katika sheria ya Mungu, yaani amri ile inayokataza tendo la kuziabudu sanamu. tena wakagawa amri ya kumi kuwa sehemu mbili, ili waidumishe hesabu yake ya zamani.VK 18.3
Lakini nia hii ya kutoa idhini kwa matendo kama ya kishenzi ili yafanywe kanisani, ilitengeneza njia ili mamlaka ya Mungu ipate kudharauliwa zaidi. Shetani aligeuza amri ya nne pia, akijaribu kuondoa Sabato ya zamani, yaani siku ile ambayo Mungu aliibariki na kuitakasa; na mahali pake alitukuza siku ile iliyoshikwa na washenzi kuwa kama “siku kuu ya jua.” Mwanzoni badilisho hili halikufanywa dhahiri. Katika karne chache baada ya Yesu, Wakristo wote wakaishika Sabato ile iliyo ya kweli. Wakawa na uangalifu sana juu ya heshima iliyomhusu Mungu, wakaamini ya kwamba sheria yake haibadiliki, wakafanya bidii katika kuutunza utakatifu wa maagizo yake. Lakini Shetani alitumia hila sana kwa mawakili wake ili wapate kulitimiliza kusudi lake. Makusudi akawatazamisha watu siku kuu ile ya jua (yaani Sunday), siku ile ilifanywa kuwa siku kuu ya kukumbuka ufufuo wa Kristo. Ikafanywa thubutu kuondoa amri ya pili katika shcria ya Mungu, mikutano ya dini siku ile; hata hivyo ikahesabiwa kuwa siku ya mchezo na furaha, tena Sabato ikashikwa kuwa siku takatifu.VK 20.1
Konstantine alipokuwa angali mshenzi, alitoa amri akiamuru ili “Sunday” iwe siku kuu kwa watu wote na mahali pote katika Ufalme wa Kirumi. Baada ya kuongoka kwake aliendelea kuishika siku ya “Sunday,” tena amri ile aliyoitoa alipokuwa mshenzi, ilitiliwa nguvu kwa ajili dini yake mpya. Lakini kadiri siku ile ilivyotukuzwa haikutosha kuwazuia Wakristo wasiishike Sabato ya kweli kuwa siku takatifu ya Bwana. Basi ilikuwa ni lazima jambo jingine lifanywe; sabato ile ya uongo lazima ipate kutukuzwa sawa na Sabato ile ya kweli. Miaka michache baada ya Konstantine kutoa amri yake, Askofu wa Rumi alitoa neno kwa kuiita “Sunday” kuwa ni siku ya Bwana. Kidogo kidogo hivi, watu waliongozwa mpaka kuihesabu hiyo kuwa ni siku takatifu. Lakini watu wakaendelea kuishika Sabato ya zamani.VK 21.1
Lakini yule mdanganyifu mkuu alikuwa hajamaliza kazi yake. Aliazimia kukusanya jamii ya Wakristo wote chini ya uongozi wake, na kutumia nguvu zake kwa njia ya Askofu wa Rumi mwenye kujivuna na kujidai kuwa ni kaimu wa Kristo. Kwa njia ya watu waliojidai kuwa ni Wakristo lakini ni kama nusu washenzi, na kwa maaskofu waliotaka makuu, na kwa washiriki wa kanisa waliopenda anasa za kidunia, basi Shetani alifikiliza kusudi lake. Mara kwa inara zikakusanywa baraza zilizo kubwa, ambamo wakaitwa wakuu wa kanisa kutoka duniani pote. Na katika baraza karibu zote, Sabato ile iliyowekwa na Mungu ilikuwa ikizidi kuondolewa heshima na kutwezwa, na “Sunday” ikazidi kutukuzwa. Kwa namna hiyo siku kuu ya kishenzi ikapata kutukuzwa kuwa kama jambo lililowekwa na Mungu, na huku Sabato ya Biblia ikatangazwa kuwa ni msazo wa dini ya Kiyahudi, tena wale waliotukuza siku ile wakanenwa kuwa wamelaaniwa.VK 21.2
Sasa yule mwasi mkuu alikuwa amefaulu katika kujiinua nafsi “juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa.” 2 The. 2:4. Alikuwa amethubutu kugeuza amri katika sheria ya Mungu iliyo amri ya pekee ambayo kwa dhahiri huwaonyesha wanadamu Mungu wa kweli aliye hai. Katika amri ya nne Mungu hudhihirishwa kuwa ni Muumbaji wa mbingu na nchi, na kwa hiyo ametofautishwa na miungu mingine yote ya uongo. Siku ya Saba ilitakaswa kuwa pumziko kwa wanadamu ili iwe kuna ukumbusho wa kazi za kuumba. Ilikusudiwa kuwa kitu cha kuwakumbusha wanadamu daima ya kwamba Mungu aliye hai ndiye asili ya kuwako kwetu. tena yeye ndiye ahusuye kuheshimiwa na kusujudiwa. Shetani hujitahidi katika kuwavuta watu wasimche Mungu wala kuitii sheria yake; kwa hiyo hujitia katika kushindana na amri ile hasa ambayo huwaonyesha watu jinsi Mungu alivyo Muumba.VK 22.1
Sasa Waprotestanti (yaani Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi) walio wengi husema sana ya kwamba “Sunday” ndiyo Sabato ya Wakristo kwa ajili ya ufufuo wake Kristo. Lakini Biblia haishuhudii neno hilo. Wala Kristo mwenyewe wala mitume wake hawakutukuza siku hiyo. Jambo la kuishika “Sunday” kuwa kama siku kuu ya Kikristo lilianzishwa na ile “sin ya kuasi” ambayo ilikuwa imeanza kutenda kazi yake hata zamani zile katika situ alipoishi Paulo. Basi siku gani, tena mahali gani ambapo Bwana alikubali jam bo hili ambalo ni mzaliwa wa Kanisa la Kirumi? Tena inaweza kutolewa sababu gani yenye nguvu kwa kuthibitisha badilisho hili ambalo haliwezi kamwe kuthibitishwa na Maandiko Matakatifu?VK 22.2
Katika kame ya sita, mamlaka ya Papa yalikuwa yameimarishwa zaidi. Kiti cha enzi yake kiliwekwa katika mji mkuu wa kifalme, naye Papa akatangazwa kuwa ni kichwa cha makanisa yote. Mamlaka ya zamani ya Ushenzi iliiondokea ile mamlaka ya Papa. Joka alikuwa amempa nyama “nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.” Ufunuo 13:2. Miaka 1260 ya mateso ya Kanisa la Kirumi ambayo yalitabiriwa na Danieli na Yohana yali-kuwa yakianzishwa. (Danieli 7:25; Ufu. 13:5-7). Wakristo walishurutishwa kuchagua, ili watupe uaminifu wao na kukubali urembo wa dini na ibada za Kanisa la Kirumi, ama kumaliza maisha yao gerezani, kuunguzwa kwa moto, kushtushwa viungo katika mtambo, au kukatwa vichwa. Ndipo maneno haya ya Yesu yakatimia, “Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.” Luka 21:16.17. Mateso yaliwapata waaminifu kwa ukali usivyoonekana tangu awali, na dunia yote ikawa kama uwanja wa vita. Kwa miaka mia nyingi watu wa kanisa la Kristo walikuwa wakijificha. Hivyo ndivyo asemavyo nabii: “Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.” Ufunuo 12:6.VK 23.1