Sura Ya Tatu - Watengenezaji Wa Kanisa La Zamani
*****
KATI ya giza iliyoipata dunia kwa muda ule mrefu wa utawala wa Kanisa la Kirumi, mwanga wa ukvveli haukuweza kuzimishwa kabisa. Katika kila kizazi kulikuwa na mashahidi wa Mungu—watu waliohifadhi imani katika Kristo kama mpatanishi wa pekee kati ya Mungu na mwanadamu, watu walioheshimu Biblia kama kipeo cha pekee cha maisha, na walioitunza Sabato ya kweli. Watu wa vizazi vinavyowafuata watu hawa hawatafahamu kamwe ukuu wa mema wanaourithi kwa ajili ya matendo yao. Waliitwa wazushi, makusudi yao yalikanwa, tabia zao zilisengenywa, maandiko yao yalikatazwa, yalielezwa vibaya, au kuondolea sehemu fulani yenye maana Sana. Walakini, walisimama imara, na katika kila kizazi waliihifadhi imani yao halisi, kama urithi mtakatifu kwa vizazi vya nyuma.VK 29.1
Vita vilipigwa vikali mno juu ya Biblia hata mara zingine nakili zilizobaki zilikuwa chache sana; lakini Mungu hakuliacha Neno lake liharibiwe kabisa. Mafundisho ya kweli yaliyomo hayakuweza kufichwa milcle. Mungu aliweza kuyafunua maneno ya uzima kwa urahisi, jinsi alivyofungua milango ya gereza na kuviondoa vyuma vya milango kwa kuweka watenda kazi wake huru. Katika nchi mbali mbali za Ulaya, watu walivutwa na Roho ya Mungu wapate kuitafuta kweli kama watu waitafutavyo mali iliyofichwa. Roho ya Mungu akiwaongoza kuchunguza Maandiko Matakatifu, waliyasoma maneno ya Biblia kwa furaha kuu ajabu. Walikuwa tayari kujipatia nuru hata kwa njia ya shida. Ingawa hawakuona mambo yote dhahiri sana, waliwezeshwa kufahamu mambo ya kweli yaliyokuwa yakifichwa tangu miaka mingi. Waliendelea mbele kama wajumbe waliotumwa na Mungu, wakiivunja minyororo ya upotovu na kuamini mambo kama ushirikina, uchawi, mizimu na kadha wa kadha, na kuwaita wale waliokuwa utumwani hivi kwa muda mrefu wapate kuondoka na kudai uhuru wao.VK 29.2
Wakati ulikuwa umewadia kwa Biblia kutafsiriwa ili watu wa nchi mbali mbali waipate katika lugha zao wenyewe. Wakati wa giza nene ya dunia ulikuwa umepita. Saa za giza zilitaka kumalizika, tena katika nchi nyingi ilikuwa kana kwamba zinaonekana dalili za pambazuko.VK 30.1