Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Utaratibu Katika Utunzaji Mzuri wa Upendo

    Watoto wamekabidhiwa kwa wazazi wao kama amana ya thamani, ambayo siku moja Mungu ataitaka mikononi mwao. Yatupasa kutumia saa nyingi zaidi kwa mafundisho yao, pamoja na uangalifu mwingi zaidi, na maombi zaidi. Wanahitaji zaidi malezi bora.KN 160.3

    Mara nyingi ugonjwa wa watoto huweza kutokana na makosa ya maongozi. Kutokuwa na saa za kawaida za kula chakula, kutokuwa na mavazi ya kutosha jioni siku za baridi, ukosefu wa mazoezi ya viungo vya mwili kuuweka mwendo wa damu katika hali nzun ya afya, au ukosefu wa hewa safi ya kutosha kuisafisha damu, pengine nuwa ndiyo asili ya ugonjwa. Basi, yafaa waponye hali za makosa hayo upesi iwezekanavyo.KN 160.4

    Watoto, kwa kawaida huzoezwa tokea utotoni kujifurahisha kwa kuiridhisha tamaa ya chakula na kufundishwa kwa kuishi ili kula. Mama ahusikana sana na kukuzwa kwa tabia za watoto wake utotoni mwao. Aweza kuwafundisha kuitawala tamaa ya chakula na kuwafanya walafi. Mama mara nyingi hupanga mipango yake kuitimiza sehemu fulani kwa siku; na naipo watoto wakimsumbua, badala ya kutumia wakati kutuliza huzuni zao ndogo na kuwafurahisha, huwapa kitu fulani kukila ili wanyamaze, ambacho hutimiza mradi wake huo kwa muda mfupi tu lakini mwishowe huyafanya mambo kuwa mabaya zaidi. Matumbo ya watoto hushindiliwa kwa chakula wakati wasipokihitaji hata kidogo. Kilichokuwa kikitakiwa tu ni wasaa kidogo wa mama na aungaiizi wake. Lakini amehesabu wakati wake kuwa wa thamani sana hata hawezi kuutoa kuwapendeza watoto wake. Pengine mpango wa nyumba yake kwa namna ya kuwapendeza wageni hata wausifu, na kukipika chakula chake vizuri ndiyo mambo anayoyathamini zaidi kuliko furaha na afya ya watoto wake.KN 160.5

    Katika kutayarisha vazi la mtoto mchanga, hali ya kufaa, raha, na afya ingefikiriwa kwanza kabla ya kurikiria namna ama uzuri wa kusifika. Mama asingeumia wakati kwa mapambo na malidadi tu kuyafanya mavazi hayo madogo kuwa ya kupendeza macho, na kwa kufanya hivi kujichosha kwa kazi isiyo ya lazima pia. Asijishurutishe kushona kunakoyatumikisha macho na mishipa ya fahamu, wakati anapohitaji kupumzika na kufanya mazoezi mazuri ya viungo vya mwili. Apaswa kuufaha wajibu wake kutunza nguvu zake ili aweze kutimiza madai yatakayofanywa juu yake. 2AH 255-267;KN 161.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents