Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maombi ya Asubuhi na Jioni

    Baba na mama, kila siku asubuhi na jioni wakusanyeni watoto wenu karibu nanyi, na kwa maombi ya unyenyekevu, inueni mioyo yenu kwa Mungu mpate msaada. Wapenzi wenu wako kwenye hatari ya majaribu. Udhia wa kila siku unasonga mapito ya vijana na wazee. Wale ambao wataishi maisha ya uvumilivu, upendano, na furaha hawana budi kumwomba Mungu. Twaweza kupata ushindi juu ya nafsi kwa njia tu ya kupokea msaada wa daima kutoka kwa Mungu.KN 173.1

    Kama pamekuwako wakati ambapo kila nyumba ingekuwa nyumba ya maombi, sasa ndio wakati huo. Ukafiri na mashaka vimeenea. Uovu umejaa tele. Makosa mabaya yanafurika katika njia kuu za rohoni, na uasi dhidi ya Mungu hutokea katika maisha. Zikiwa zimetawaliwa na dhambi, akili za kuchagua mema na mabaya ziko chini ya utawala wa mabavu wa Shetani. Roho imefanywa kuwa uwanja wa majaribu yake; na ikiwa mkono fulani wenye nguvu hauwezi kunyoshwa ili kumwokoa, mwanadamu atakwenda huko anakoongozwa na mkuu wa uasi.KN 173.2

    Lakini, wakati huu wa hatari za kutisha, wengine wanaodai kuwa ni Wakristo hawana maombi kwa watu wa nyumbani. Hawamheshimu Mungu nyumbani, hawawafundishi watoto kumpenda na kumcha Mungu. Wengi wamejitenga mbali naye hata hujiona kuwa wamestahili hukumu wakimkaribia. Hawawezi kukikaribia “kiti cha neema kwa ujasiri,” “huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.” (Waebrania 4:16; lTimotheo 2:8). Hawana umoja na Mungu. Wana namna ya utauwa bila uwezo.KN 173.3

    Wazo kwamba sala si faradhi ni mojawapo ya hila kubwa za Shetani anazotumia kuharibu roho za watu. Kuomba ni kushirikiana na Mungu, chemchemi ya hekima, Chimbuko la nguvu, na amani, na raha. Yesu alimwomba Baba dua “pamoja na kulia sana na machozi.” Paulo huwaonya waumini kuomba “bila kukoma” katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zao zijulikane na Mungu. Yakobo asema, “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana.” (Waebrania 5:7; 1 Wathesaloneke 5:17; Yakobo 5:16). Kwa kuomba kwa bidii wazazi wangewazungushia watoto wao kitalu. Yawapasa kuomba kwa imani kamili kuwa Mungu akae nao na ya kwamba malaika watakatifu wawalinde pamoja na watoto wao na kuwaepusha na nguvu za udhalimu za Snetani.KN 173.4

    Yawapasa katika kila nyumba pawekwe saa ya maombi ya asubuhi na jioni. Ni jambo zuri kama mni kwa wazazi kuwakusanya watoto wao kuwazunguka kabla ya kufungua kinywa, kumshukuru Baba aliye mbinguni kwa ulinzi wake usiku kucha, na kumwomba msaada na uongozi na ulinzi wake mchana kutwa! Pia yafaa kama nini, inapokuwa jioni, kwa wazazi na watoto kukusanyika tena mbele za Mungu na kumshukuru kwa ajili ya mibaraka ya siku hiyo ambayo imepita.KN 173.5

    Kila siku asubuhi jitoeni wakfu na watoto wenu kwa Mungu kwa siku hiyo. Msifikiri kwamba yafaa kufanya hivi baadaye miezi au miaka kadha wa kadha ikisha kupita; hiyo si yenu. Mmepewa siku moja fupi. Mtumikieni Bwana saa za siku hiyo, kana kwamba ndiyo siku yenu ya mwisho duniani. Wekeni mipango yenu yote mbele za Mungu, kutimizwa au kuachwa, kama Mungu anavyoamua mwenyewe. Kubalini mipango yake badala ya yenu wenyewe, ijapokuwa kuikubali hubidi kuyaacha mashauri yanayopendwa. Hivyo ndivyo yatakavyofanywa kufanana zaidi na kielelezo kitakatifu; na “amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zetu katika Kristo Yesu,” (Wafilipi 4:7).KN 174.1

    Baba, au, wakati asipokuwako nyumbani, mama, angefanya maombi, kwa kuchagua fungu la Biblia zuri na jepesi kufanamika. Ibada hii iwe fupi. Sura ndefu ikisomwa na sala ndefu ikiombwa, ibada hii hufanywa kuwa ya kuchosha, na kumfanya mtu aone ni heri kuufikia mwisho wa haya maombi. Mungu hatukuzwi saa ya maombi inapofanywa kuwa lsiyopendeza na ya kuchosha, ikiwa ya taabu na isiyo na mambo ya kupendeza, hata kuwafanya watoto waichukie.KN 174.2

    Enyi baba na mama, fanyeni saa ya maombi kuwa ya kupendeza sana. Hakuna sababu ya kuifanya saa hii isiwe nzuri na yenye kupendeza ya siku nzima. Matayarisho kidogo ya saa hii yatawawezesha kuifanya iwe ya kupendeza kabisa na yenye faida. Kila wakati ibada hii iwe na mambo mbalimbali. Maswali huweza kuulizwa juu ya fungu la Biblia lililosomwa, na maelezo mazuri machache yaweza kutolewa. Wimbo wa kumsifu Mungu waweza kuimbwa. Sala iombwayo iwe fupi na yenye kusudi maalumu. Kwa maneno mepesi ya uaminifu mwenye kuongoza maombi msifii Mungu kwa wema wake na kumwomba msaada. Ikiwezekana, waachieni watoto nafasi kushiriki katika kusoma na kusali.KN 174.3

    Milele peke yake ndiyo itakayodhihirisha faida iletwayo na saa hizi za maombi. 37T32-44.KN 174.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents