Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mashauri Mema kwa Waume na Wake Juu ya Mambo ya Fedha

    Yawapasa wote kujifunza kuandika hesabu za fedha. Wengine huidharau kazi hii na kuhesabu kama haina maana, lakini kufanya hivi ni kosa. Gharama zote zingeelezwa kwa usahihi. 14AH 374KN 178.1

    Pengine leo ungeweza kuwa na akiba ya mali ya kutumia kwa hatari au matukio ya ghafula, na kusaidia kazi ya Mungu, ikiwa ungetumia fedha kiasi ikupasavyo. Kila juma sehemu ya mshahara wako ingewekwa akiba na kwa hali iwayo yote isiguswe isipokuwa kama ikibidi kwa sababu ya kuumia, au kumrudishia Mtoaji k’wa njia ya sadaka kwa Mungu. Fedha uliyojipatia kwa kazi haijatumiwa kwa busara na kwa kiasi ili kuacha akiba ya kukusaidia iwapo utapatwa na ugonjwa jamaa yako isije ikakosa pesa za matumizi unazoleta kuwasaidia. Yawapasa jamaa yako kuwa na kitu cha kutegemea kama ukiingia katika shida. 15AH 395, 396;KN 178.2

    Yawapasa kusaidiana. Usidhani kwamba kubania mfuko, na kukataa kumpa mkeo pesa ni sifa njema. Ni vizuri kumpatia mkeo kiasi fulani cha fedha kila juma na kumwacha afanye apendavyo na fedha hiyo. Hujampa nafasi kutumia busara yake au akili yake kwa sababu hujafahamu vizuri cheo apaswacho mkeo kuwa nacho. Mkeo ana akili bora na timamu. Mpe mkeo sehemu ya pesa upatazo. Mwache achukue hizo ziwe mali yake mwenyewe, na kuzitumia kama apendavyo. Yapasa aruhusiwe Kutumia mali anazojipatia kwa kazi yake kama aonavyo mwenyewe kwamba yafaa. Kama angekuwa na kiasi fulani cha fedna ya kutumia jinsi apendavyo mwenyewe, bila kulaumiwa. angepunguziwa mzigo mzito unaomlemea mawazoni mwake. 16AH 378KN 178.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents