Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 29 - Maburudisho

  IKO tofauti kubwa baina ya maburudisho na mazungumzo, maongezi ama michezo ya kujifurahisha tu. Maburudisho maana yake nasa ni kutia nguvu na kujenga. Hutusahaulisha kidogo kazi na shughuli zetu za kawaida, na kuburudisha akili na mwili, na kwa hivyo kutuwezesha kuzirudia kazi zetu tukiwa na nguvu mpya za kufanya kazi ya maisha kwa uaminifu. Ambapo mazungumuzo, maongezi ama michezo ya kujifurahisha tu ni kutafuta anasa, na mara nyingi inafulilizwa kupita kiasi; inatumia nguvu kupita kiasi; nguvu ambazo zinahitajika kwa kazi ya manufaa, na hivyo mwisho wake ni kuyapinga mafanikio halisi ya maisha” - Ed. 207.KN 182.1

  Wakristo wana njia nyingi za kupatia furaha, nao huweza kusema kwa usahihi furaha zilizo halali na nzuri. Wanaweza kufaidi maburudisho ikiwa hayatapoteza akili wala kuharibu roho ya mtu, kama vile kukatisha tamaa na kuhuzunisha baadaye na kuharibu kujistahi nafsi au kuzuia njia ya manufaa. Kama wakimchukua Yesu pamoja nao na kuwa na moyo wa kumwomba Mungu kwa bidii, na salama kabisa.KN 182.2

  Maburudisho yo yote ambayo waweza kuyashiriki na kuomba mbaraka wa Mungu juu yake kwa imani hayawezi kuwa yenye hatari. Lakini maburudisho (starehe) yo yote ambayo hukukosesna sala ya faragha, kwa ajili ya ibada ya wakfu wa mahali pa kuombea, au kushiriki kwenye mkutano wa maombi si salama, bali ni yenye hatari.KN 182.3

  Sisi tu jamii ya wale wanaosadiki kwamba ni bahati yetu kila siku ya maisha yetu kumtukuza Mungu duniani, na ya kwamba haitupasi kuishi ulimwenguni humu kwa kujipendeza tu kwa anasa. Tuko hapa kuwanufaisha wanadamu na kuwa mbaraka kwa watu mtaani; tukiyaacha mawazo yetu kufuata njia ile mbaya ambayo wengi wanaotafuta ubatili na upuzi huyaacha mawazo yao kuifuata, twawezaje kuwanufaisha watu wa taifa letu na wa kizazi chetu? Twawezaje kuwa mbaraka kwa watu wanaotuzunguka? Tu wenve hatia kama tukijifurahisha kwa anasa yo yote itakayotufanya tusifae kwa kazi zingine zaidi za dini. Yako mambo mengi ambayo venyewe ni halali, lakini yaishapo hugeuzwa vibaya na Shetani, kuwa mtego kwa wale wasiojihadhari.KN 182.4

  Kuna haia kubwa ya kuwa na kiasi katika starehe, na katika mambo yote mengine. Na hali ya mambo haya ingefikiriwa vizuri kwa uangalifu. Kila kijana apaswa kujiuliza, je, starehe hizi zitakuwa na mvuto gani katika afya ya mwili, akili, na kwenye tabia ya moyoni? Je, akili zangu zitapumbazwa hata kumsahau Mungu? Je, nitapotewa na utukufu wake? 1 AH 512-514;KN 182.5

  Ni bahati njema na wajibu wa Wakristo kujaribu kuziburudisha roho zao na kuitia nguvu yao kwa maburudisho halali, wakiwa na kusudi la kutumia uwezo wao wa mwili na akili kwa utukufu wake Mungu. Maburudisho yetu hayapaswi kuwa kujifurahisha na vicheko vya ovyo, visivyo na maana, vya upuzi. Hatuwezi kuyafanya kwa njia itakayowanufaisha na kuwainua wale tunaoshirikiana nao, na kutuwezesha kufaulu zaidi kwenye kazi zitupasazo kama Wakristo? 2AH 493;KN 183.1

  Wakati unaotumiwa katika mazoezi ya kufaa ya viungo vyote vya mwili ni faradhi kwa kazi bora za kila kimoja. Ubongo ukichoshwa daima huku viungo vingine vya mashine hii yenye uhai visipofanya kazi, huwapo upotevu wa nguvu, mwilini na akilini. Mwili hunyang’anywa siha yake, akili hupotewa na nguvu zake, na mwishowe huleta fadhaa.KN 183.2

  Wale wanaoshughulika sana na masomo wangekuwa na pumziko (ama michezo). Akili hazitaki kufikirishwa daima, kwa lcuwa mashine hii ndogo ya kichwani huchoka. Mwili na akili pia havina budi kupata mazoezi. 3AH 494, 495;KN 183.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents