Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ellen G. White Kama Alivyojulikana Kwa Wengine

    Wakiwa wamepata habari za maisha ya ajabu ya Ellen White kuwa ni mjumbe wa Mungu, wengine wameuliza, alikuwa mtu wa namna gani? Je, alikuwa na shida tulizo nazo? Alikuwa tajiri, au alikuwa maskini? Alipata kucheka?KN 20.5

    Ellen White alikuwa mama mwenye kufikiri, Alikuwa Bibi mwangalifu, mara nyingi aliwakaribisha watu wetu nyumbani mwake. Alikuwa jirani mwema. Alikuwa mwanamke mwenye nia thabiti, mwenye mwenendo mzuri, na mpole wa tabia na sauti. Hakuwa na natasi maishani mwake kuonyesha uso wa huzuni, kuwa na uso wa hasira, ama dini isiyo ya furaha. Mtu aliweza kujiona kuwa na raha kamili mbele zake. Pengine njia bora ya kumfanamu Ellen White ilikuwa kufika nyumbani kwake mwaka 1859, mwaka wa kwanza alipoanza kuandika kitabu cha kumbukumbu za kila siku.KN 21.1

    Twaona kuwa watu wa nyumba ya Bwana na Ellen White waliishi viungani mwa mji wa Battle Creek, katika nyumba ndogo, kwa sehemu kubwa akitoa nafasi kwa bustani, miti mingi ya matunda, ng’ombe, na kuku, na mahali pa watoto wa kiume kufanyia kazi na michezo. Ellen White wakati huu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mmoja. Mchungaji White alikuwa mwenye miaka thelathini na sita. Wakati huo palikuwa na watoto wa kiume watatu nyumbani, umri wao, miaka minne, tisa, na kumi na miwili.KN 21.2

    Tungetazamia pia kuona msichana Mkristo mzuri katika nyumba hiyo aliyeajinwa kazi za nyumbani, kwa mama White, maana mara nyingi alikuwa safarini na mara kwa mara alikuwa akishughulika na mazungumzo yake na maandishi. Lakini, tunamuona Ellen White akifanya kazi za nyumbani, kupika, kusafisha, kufua na kushona. Siku zingine alienda kwenye nyumba ya uchapaji ambapo alipata mahali patulivu kwa ajili ya kuandika. Siku zingine tunamwona bustanim, akipanda maua na mboga za majani na wakati mwingine akibadilishana miche ya maua na majirani. Alikusudia kufanya nyumbani kuwa mahali pa kupendeza kwa watu wa nyumba yake kama alivyoweza, ili watoto wapahesabu nyumbani kuwa mahali pa kutamanika kukaa.KN 21.3

    Ellen White alikuwa mnunuzi mwangalifu, na majirani Waadventista walifurahi walipoweza kwenda pamoja naye kununua vitu madukani, kwa sababu alijua ubora wa vitu. Mama yao alikuwa mwanamke mwenye busara na aliwafundisha binti zake mafundisho mengi ya thamani. Aliona kuwa vitu visivyotengenezwa vizuri mwisho vilikuwa vya gharama kubwa zaidi ya bidhaa bora.KN 21.4

    Sabato ilifanywa siku ya kupendeza kuliko siku zingine za juma kwa watoto. Naam, watu wa nyumbani humu walihudhuria ibada kanisani na ikiwa Mchangaji na Mama White hawahudumu basi familia yote walipenda kuketi pamoja wakati wa ibada. Chakulani walipenda kuchagua vyombo visivyotumika siku zingine, na tena kama hali ya hewa ikiwa nzuri, Ellen White alipenda kutembea na watoto wake mwituni, au kando ya mto, nao waliweza kutazama uzuri wa viumbe na kujifunza kazi za Mungu na uumbaji. Kama siku hiyo ikiwa na mvua au baridi, aliwakusanya watoto jikoni ambapo alipenda kuwasomea, mara nyingi alisoma habari alizokusanya huko na huko akifanya safari zake. Baadhi ya hadithi hizi zilichapishwa baadaye ili wazazi wengine wazipate na kuwasomea watoto wao.KN 21.5

    Ellen White hakuwa mzima wa afya sana wakati huu, na mara nyingi aliona kizunguzungu wakati wa mchana, lakini hili halikumzuia asiendelee na kazi yake nyumbani na kazi ya Mungu pia. Miaka michache baadaye, mwake 1863, akapewa njozi juu ya afya na utunzaji wa wagonjwa. Alionyeshwa katika njozi mavazi yafaayo kuvaa, chakula kifaacho kula, mazoezi ya mwili yalivyo muhimu na kupumzika, pamoja na ukubwa wa kumwamini Mungu kunavyotakiwa ili kuwa na mwili wenye nguvu na afya.KN 22.1

    Nuru iliyotoka kwa Mungu juu ya mlo na madhara ya nyama ilimshtua sana Ellen White mwenyewe kwa maana alidham ya kuwa nyama ilikuwa murua kwa afya na nguvu. Kwa kutumia nuru ya njozi hii kuangaza akili zake alimwamuru yule msichana aliyemsaidia kutayarisha chakula kwa watu wa nyumba yake kuweka mezani vyakula safi tu, vyakula vyepesi, ambavyo vilifanywa kwa nafaka, mboga za majani, mbegu jamii ya njugu, maziwa, mafuta ya juu ya maziwa (ya mtindi), na mayai. Palikuwa na matunda tele.KN 22.2

    Watu wa nyumbani walipofika mezani palikuwa na vyakula vingi vizuri, lakini hapakuwako na nyama. Ellen White alikuwa na uchu wa nyama, wala si wa vyakula vingine, hivyo akakata shauri kuondoka mezani mpaka atakapoweza kurudi na kupendezwa na chakula chepesi tu. Katika mlo mwingine mambo yakawa hali ile ile, lakini chakula chepesi hakikumvutia. Kisha tena wakafika mezani. Palikuwa na vyakula vyepesi, kama alivyoonyeshwa katika njozi kuwa ni jambo lililo bora kwa afya na nguvu na kukua. Lakini alitaka kula nyama, ambayo ameizoea. Walakini, sasa alikwisha kujua kuwa nyama haikuwa chakula bora. Anasema alishika mikono yake juu ya tumbo lake, na kuliambia maneno haya, “Waweza kungoja mpaka hapo uwezapo kula mkate.”KN 22.3

    Haukuwa muda mrefu Ellen G. White akaweza kupendezwa na vyakula vyepesi, na kwa kubadili ulaji wake, afya yake ikawa bora mara, na siku zote za baadaye maisnani mwake akafaidi afya bora. Hivyo yaonekana kuwa alikuwa na shida zile zile tulizo nazo sisi sote. Ilimbidi kujipatia ushindi juu ya tamaa ya chakula katika maisha yake mwenyewe sawa na sisi sote tupasavyo kupata ushindi. Kutokutumia vitu vinavyodhuru afya (health reform) Kumekuwa mbaraka mkubwa kwa watu wa nyumba ya Bwa na Bibi White, kama kulivyo kwa maelfu ya Waadventista ulimwenguni mwote.KN 22.4

    Baada ya njozi hii juu ya kutokutumia vitu vyenye kudhuru afya, na mageuzi katika nyumba ya Bwana na Bibi White ya njia nyepesi za kuwatibu wagonjwa, Mchungaji na Mama White waliitwa mara kwa mara na majirani wakati wa ugonjwa kusaidia kutoa matibabu, na Mungu alizibariki sana jitihadi zao. Nyakati zingine wagonjwa waliletwa nyumbani kwao na kutunzwa kwa uangalifu mwingi mpaka wakapona kabisa.KN 22.5

    Ellen White alifurahia sana vipindi vya kupumzika na kuburudika, ama milimani, ama ziwani, ama kando kando ya bahari. Katika umri wa kati, wakati alipokuwa akikaa karibu na Pacific Press, nyumba yetu ya uchapaji wa vitabu magharibi mwa Marekani, katika nyumba hii ya uchapaji ilikusudiwa kwamba siku moja itumiwe katika kupumzika na kujiburudisha. Ellen White na watu wa nyumbani mwake na watenda kazi wa oflsini wakaulizwa kujiunga na watu wa kazi ya uchapaji wa vitabu, naye akaukubali mwaliko huu upesi. Mumewe alikuwa pande za mashariki katika kazi ya Kanisa. Tumepata habari hizi katika barua aliyomwandikia juu ya jambo hili.KN 23.1

    Baada ya kufaidi chakula kizuri cha adhuhuri cha kufaa kwa afya ufukoni, kundi zima lilikwenda kupanda mashua katika ghuba ndogo ya San Francisco. Kapteni wa mashua hii alikuwa mshiriki wa Kanisa na ilikuwa alasin ya kupendeza. Kisha ikakusudiwa kwamba waende kwenye bahan pana. Katika kulisimulia jambo hili Ellen G. White ameandika:KN 23.2

    “Mawimbi yalikuwa makubwa, nasi tulikuwa tukirushwa lakini sikuwa na maneno ya kumwambia mtu awaye yote. Lilikuwa jambo zuri! Manyunyu yalitudondokea. Upepo ulikuwa wa nguvu nje ya Golden Gate, nami kamwe nilikuwa sijawahi kufaidi jambo zuri hivi maishani mwangu!”KN 23.3

    Kisha aliyatazama macho mapevu ya Kapteni huyu, na wepesi wa mabaharia kuzitii amri zake, naye akafikiri:KN 23.4

    “Mungu anazishikilia pepo mikono mwake. Anatawala maji. Nasi tu vitu vidogo tu juu ya maji mengi, yenye kina ya Pasifiki: Lakini malaika wa mbinguni hutumwa kuilinda mashua hii ndogo ikishindana na haya mawimbi. Ah, kazi za ajabu za Mungu! Kupita kabisa ufahamu wetu! Akitazama mara moja huona mbinguni juu sana na katikati ya bahari pia!”KN 23.5

    Ellen White alikuwa anao moyo mchangamfu. Siku moja aliuliza, “Je, unaniona kuwa mwenye huzum, mwenye kukata tamaa, mwenye kunung’unika? Ninayo imani yenye kulikataza jambo hili. Kutokufahamu vema tabia kamili ya Kristo na huduma ya Kikristo, ndiko kunakoleta miisho hii Kazi ya hiari ya moyo kwa Yesu huleta dini ya kupendeza. Wale wanaomwandama Kristo kwa karibu sana hawajahuzunika.”KN 23.6

    Tena wakati mwingine aliandika: “Wakati mwingine watu wamependa kufikiri kuwa uchangamfu haupatani na adabu ya tabia ya Knsto; lakini hili ni kosa. Mbinguni ni furaha tupu.” Naye akafahamu kuwa kama ukionyesha uso wa furaha, utaonyeshwa pia uso wa furaha; kama ukisema maneno ya upole utarudishiwa pia maneno ya upole.KN 23.7

    Ingawa mambo yalikuwa hivyo, kuna wakati alipoumia sana. Wakati mmoja wa jinsi hii ulikuwa mara baada ya kwenda Australia kusaidia kazi pande zile. Alikuwa mgonjwa sana karibu mwaka mmoja, akaumia sana. Alikuwa hawezi kutoka kitandani mwake wakati huo na hakuweza kulala usinginzi ila saa chache tu usiku. Juu ya jambo hili akamwandikia barua rafiki yake akisema:KN 24.1

    “Nilipojiona katika hali ya kutojimudu, nilisikitika sana kuwa nilivuka bahari kubwa. Mbona nisiwe Marekani? Mara kwa mara nalificha uso wangu katika matandiko ya kitanda na kulia sana. Lakini sikupendelea kutoa machozi hivi. Nikasema kimoyo moyo, Ellen G. White, unafikiri nini? “Nikasema, ‘Ndiyo’. “Basi, kwa nini waona kuwa umetupwa na kukatishwa tamaa? Je, hii si kazi ya adui? Naamini ni kazi yake!’ “Nikayafuta machozi upesi nilivyoweza na kusema, ‘Yatosha. Sitaangalia upande wa giza. Niishi au nife, naikabidhi roho yangu kwake Yeye aliyenifilia.KN 24.2

    “Kisha nikaamini kuwa Mungu atafanya yote kuwa sawa, na katika hii miezi minane ya kutokujimudu sikuwa na majonzi, wala mashaka. Sasa nalihesabu jambo hili kama sehemu ya kusudi kuu la Mungu kwa ajili ya faida ya watu wake hapa katika nchi hii, na kwa ajili ya wale walio Marekani na kwa raida yangu. Siwezi kueleza sababu wala jinsi mambo yalivyokuwa, lakini naliamini. Nami nafurahi katika mateso yangu. Naweza kumtumainia Baba yangu alive mbinguni. Sitalitilia shaka pendo lake.”KN 24.3

    Ellen White akikaa nyumbani kwake California katika miaka kumi na mitano ya mwisho wa maisha yake, alikuwa akizeeka; lakini alipenda kazi ya shamba dogo, na kazi ya kuwaweka katika hali njema watu wa jamaa waliomsaidia kazini mwake. Tunamwona akishughulika na maandishi yake, mara nyingi akianza mara baada ya usiku wa manane, kwa kuwa alienda kulala mapema. Kama hali ya hewa ikiwa nzuri, alipenda, akipata nafasi kazini mwake, kwenda kutembea kwa gari mashambani, akisimama kuzungumza na mama aliyeweza kumwona shambani au katika ukumbi wa nyumba aliyopita. Wakati mwingine aliona wenye haja ya chakula na mavazi, naye alipenda kwenda nyumbani na kuwapatia vitu kadha wa kadha kutoka katika vifaa vyake nyumbani. Miaka mingi baada ya kufa kwake alikumbukwa na majirani wa bondeni alipokaa, kama bibi kizee aliyesimulia vizuri sana habari zake Yesu.KN 24.4

    Alipokufa alikuwa anavyo vitu vingi kidogo vilivyotosha kumweka vizuri maishani. Hakuwauliza wengine kumhesabu kama kielelezo chema bali alikuwa mwenzetu miongoni mwetu, Waadventista Wasabato, mwenye kuyatumainia matendo mema ya Bwana wake aliyefufuka katika wafu na akajaribu kwa uaminifu kuitenda kazi aliyokabidhiwa na Bwana. Hivyo akiwa na matumaini moyoni mwake alifikia mwisho wa maisha yake, mnyofu katika maisha yake ya Kikristo.KN 24.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents