Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hatari ya Kusoma Hadithi za Kushtusha

  Watoto wetu watasoma nini? Hili ni swali kubwa ajabu tena lenye kudai jibu kubwa pia. Naudhika nikiona nyumbani mwa watu washikao Sabato vijitabu na magazeti yenye mfululizo wa hadithi zisizotoa nafasi ya mawazo mema akilini mwa watoto na vijana. Nimewaangalia wale ambao tamaa ya hadithi za uongo imekuzwa jinsi hii. Wamekuwa na nafasi ya kusikiliza ukweli; kujua habari za imani yetu; lakini wamekua hata kukomaa zaidi bila kumcha Mungu kwa kweli wala kuwa na utawa wa kufaa.KN 193.3

  Wasomaji wa hadithi za upuzi zenye kutarakisha huwa watu wasiofaa kwa kazi za maisha mema. Wanaishi kwenye ulimwengu wa mashaka. Nimewaangalia watoto ambao wameachwa kuwa na mazoea ya kusoma hadithi hizo. Nyumbani au ugenini, hawakutulia, walikuwa wenye kuota ndoto au kuwaza mambo isivyo, wasioweza kuongea mambo mengine ila juu ya mambo ya hivi hivi tu. Mawazo na maongezi ya dim yalikuwa mambo mageni kabisa akilini mwao. Kwa kukuza upendo wa hadithi za kutisha akili hupotoshwa, na moyo hauridhiki hata kidogo mpaka ulishwe chakula hiki kibaya. Siwezi kufikiri jina la kuwafaa zaidi wale wanaojifurahisha kwa masomo ya jinsi hii kuliko kuwaita walevi wa akili. Mazoea ya kutokuwa na kiasi katika kusoma huleta madhara kwenye ubongo sawa na mazoea ya kutokuwa na kiasi katika kula na kunywa yanavyoudhuru mwili. 6 CT 132135;KN 193.4

  Kabla ya kulipokea Neno la Mungu, wengine walikwisha kuwa na mazoea ya kusoma hadithi ndefu za uongo za kutungwa tu. Katika kujiunga na kanisa, wakajitahidi kuyashinda mazoea haya mabaya. Kuweka mbele ya watu wa jamii hiyo masomo yanayofanana na yale waliyokwisha kuyakataa ni sawa na kumpa mlevi pombe. Wakashindwa na majaribu yanayowakabili daima, hupotewa upesi na utamu wa masomo ya kweli. Hawapendi kusoma Biblia. Uwezo wa tabia yao ya moyoni hudhoofika.KN 193.5

  Dhambi huzidi kuonekana kuwa jambo lisilo baya sana. Huonyesha zaidi kutokuwa na uaminifu, na kuzidi kuchukia kazi za maisha za manufaa. Kadiri akili inavyopotoshwa, ndivyo inavyozidi kuwa tayari kushika somo lolote lenye kutamanisha. Hivyo ndivyo Shetani anavyofunguliwa njia kuweka roho ya mtu chini ya utawala wake kabisa. 77T 203;KN 194.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents