Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 32 - Muziki

  UFUNDI wa sauti tamu za nyimbo takatifu ulikuzwa daima (katika shule za manabii). Hakuna ngoma ya upuzi iliyosikika, wala wimbo hafifu ambao ungemsifu mwanadamu na kupotosha akili kumwacha Mungu: bali zaburi takatifu za sifa kwa Mwumbaji zenye kulitukuza jina lake na kuyasimulia matendo yake ya ajabu. Hivyo muziki uhfanywa kulitimiza kusudi takatifu na kuyainua mawazo kwa kile ambacho kilikuwa safi, bora na kikuu pamoja na kuamsha rohoni uchaji na moyo wa shukrani kwa Mungu. 1FE 97, 98;KN 195.1

  Uimbaii ni sehemu ya ibada ya Mungu mbinguni, nasi tungejaribu, kwa nyimbo zetu za kumsifu, kukaribia, kadiri iwezekanavyo, ulinganifu wa sauti za waimbaji wa mbinguni. Mazoezi mazuri ya sauti ni jambo lenye maana katika mafundisho, lisingedharauliwa. Kuimba, kama sehemu ya ibada ya dini, ni tendo la ibada sawa na sala. Mtu hana budi kusikia wimbo moyoni kabla ya kuweza kuupatia maneno mazuri ya kuufaa. 2PP 594;KN 195.2

  Nimeonyeshwa utaratibu kamili wa mbinguni, nami nimependezwa mno nilipokuwa nikisikiliza uimbaji ulio kamili pale. Baada ya kutoka katika njozi, nyimbo za hapa hazikunipendeza na sauti hazilingani. Nimeona jamii za malaika, waliosimama mraba, kila mmoja akiwa na kinubi cha dhahabu. Mwisho wa kinubi kuna chombo cha kubadilisha sauti. Vidole vyao havikuenda kwa uzembe juu ya nyuzi, bali waligusa nyuzi mbalimbali kutoa sauti mbalimbali. Palikuwa na malaika ambaye siku zote aliongoza ambaye kwanza hupiga kinubi na kutoa sauti, ndipo wote huungana naye kwa sauti kubwa ya uimbaji kamili wa mbinguni. Hauwezi kusifiwa mno kupita vile unavyostahili. Ni sauti tamu, takatifu, ya mbinguni, huku mionzi ya nuru ya sura ya Yesu iking’aa kutoka uso wa kila mmoja, kwa utukufu usioelezeka. 31T 146;KN 195.3

  Nalionyeshwa kuwa yawapasa vijana kujitia zaidi kwa jambo hili na kulifanya neno la Mungu kuwa mshauri wao na kiongozi wao. Vijana wana wajibu mzito ambao si wakuudharau. Ingizo la uimbaji nyumbani mwao, badala ya kuamsha utakatifu na hali ya mambo matakatifu limekuwa njia ya kupotosha mioyo yao kuiacha kweli. Nyimbo za upuzi na mtindo wa uimbaji upendwao na wengi huelekea kuwapendeza. Vyombo vya uimbaji vimechukua wakati ambao ungetumiwa kwa sala. Muziki, usipotumiwa vibaya, ni mbaraka mkubwa; lakini ukitumiwa vibaya, ni laana ya ajabu. Husisimua, lakini hautoi ile nguvu na moyo ambao Mkristo huweza tu kuupata kwenye kiti cha neema akionyesha kwa unyenyekevu wa moyo haja zake na, akilia kwa machozi, na kuomba kuongezewa nguvu za Mungu kumwezesha kushindana na majaribu makali ya yule mwovu. Shetani anawateka nyara vijana. Aha, nisema nini kuwaongoza kuukomesha uwezo wake wa kupumbazisha! Yu mpendezi mwerevu anayewashawishi kwenda hata jehanam. 41T496, 497.KN 196.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents