Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 34 - Onyo Juu ya Mavazi

  KATIKA mavazi, kama ilivyo kwa mambo mengine pia, tumejaliwa kumtukuza Muumbaji wetu. Ataka sana mavazi yetu yawe safi na yenye kukidhi afya, tena mazuri na ya kufaa pia.KN 204.1

  Yatupasa kujitahidi kuwa maridadi. Katika huduma ya patakatifu Mungu alieleza kila jambo lenye kuhusu mavazi ya wale waliohudumu mbele zake. Hivyo twafundishwa kwamba kuna uvaaji upendelewao zaidi kwa wale wanaomtumikia. Maagizo maalumu sana yalitolewa juu ya mavazi ya Haruni, maana uvaaji wake ulikuwa mfano wenye maana. Katika mambo yote yatupasa kuwa wajumbe wake. Kuonekana kwetu katika kila jambo kungeainishwa na umaridadi, adabu, na usafi.KN 204.2

  Kwa viumbe vya asili (maua mazuri) Kristo aliuelezea uzuri ambao Mungu huuthamini, neema ya kutojivika kwa mapambo mengi, usafi, hali ya kufaa ambayo ingefanya uvaaji wetu kumpendeza. 1CG 413;KN 204.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents