Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mvuto wa Namna ya Mavazi

  Kupenda mavazi huhatarisha tabia za uadilifu na kumfanya mwanamke kuwa kinyume cha mke Mkristo, mwenye tabia ya adabu na ya kiasi. Mavazi ya kujionyesha, ya bei kubwa, mara nyingi huzidisha tamaa ya mwili moyoni mwa mvaaji na kuamsha tamaa mbaya moyoni mwa mtazamaji. Mungu anaona kuwa uharibifu wa tabia mara nyingi hutanguliwa na kuendekeza kiburi na umaridadi usio na maana. Huona kuwa mavazi ya bei kubwa huzimisha tamaa ya kutenda mema. 74T 645;KN 209.4

  Mavazi rahisi, yasiyo na mapambo mengi yatakuwa sifa njema kwa dada zangu vijana. Hamwezi kwa njia iwayo yote nyingine kuacha nuru yenu langaze kwa wengine kuliko kwa njia hii ya mavazi yasiyo na mapambo mengi na mwenendo mzuri. Mwaweza kuWaonyesha wote kuwa, mwayathamini mambo ya maisha haya, hali kadhalika na yale ya uzima wa milele. 83T 376 KN 210.1

  Wengi huvaa kama walimwengu ili kuwa na mvuto kwa wale wasioamini, lakini kufanya hivyo ni kosa baya. Wakipenda kuwa na mvuto wa kweli uokoao, na wayashike maungamo yao maishani, waonyeshe imani yao kwa matendo yao ya haki, na kudhihirisha tofauti iliyopo baina ya Wakristo na ulimwengu. Maneno, mavazi, matendo, yangemshuhudia Mungu. Ndipo mvuto mtakatifu utaenezwa kwa wote wanaowazunguka, na hata wasioamini watawatambua kuwa wamekaa na Yesu. Kama wako wanaotaka mvuto wao ushuhudie ukweli, basi, wayashike maungamo yao maishani mwao na kwa njia hiyo wamwige Kielelezo Mnyenyekevu. 94T 633, 635;KN 210.2

  Dada zangu, epukeni hata umbo baya la nje. Katika zama hizi za upotevu, za kuoza hata kunuka, hamko salama msipojilinda. Sifa njema na adabu havipatikani ila kwa shida. Nawasihi, nawaomba kama wafuasi wa Kristo, mfanyapo maungamo makuu, kukithamini kitu hicho cha thamani kuu cha adabu nzuri. Hicho kitahifadhi sifa njema.KN 210.3

  Mavazi yasiyo ya kujipamba, pamoja na adabu nzuri, vitafanya makuu kumzungushia msichana usetiri mtakatifu ambao utakuwa kwake ngao ya kukingia hatari maelfu. 10 CG 417;KN 210.4

  Mavazi yasiyo na mapambo mengi yatamfanya mwanamke mwenye akili kuonekana bora sana. Vaeni kama iwapasavyo Wakristo kuvaa pasipo mapambo mengine, jitengenezeni kama wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu, kwa matendo mema. Wengi, ili wapate kuiga matendo ya kijinga, kupotewa na namna nzuri ya hali ya asili pasipo mapambo mengi nao nuvutWa na namna ya kuiga, isiyo ya asili. Hutoa wakati na fedha, nguvu za akili, na uadiliui na kuutumia mwili wao mzuri kwa desturi za akili, na uadilifu na kuutumia mwili wao mzuri kwa desturi za marsha ya kisasa.KN 210.5

  Vijana wapendwa, nia mliyo nayo ya kuvaa kama ulivyo mtindo wa siku hizi,,na kuvaa vazi jembamba, na mapambo ya dhahabu, na vitu vya kuiga kwa urembo, haitaishuhudia kwa wengine dini yenu wala neno la kweli mnalolikiri. Watu wenye akili watahesabu jitihadi zenu za kujipamba kwa nje kama thibitisho la nia dhaifu mliyo nayo na mioyo ya kiburi. 11 CG 421;.KN 210.6

  Kuna vazi ambalo kila mtoto na kila kijana aweza kulitafuta na kulipata tu pasipo kuwa na hatia. Hilo ni haki ya watakatifu. Ikiwa wangekubali tu kufanya bidii kulipata vazi hilo kama wanavyojitahidi katika mitindo ya mavazi yao katika kuwaiga walimwengu, haingepita muda mrefu wangevikwa haki ya Kristo, na majina yao hayangefutwa katika kitabu cha uzima. Mama, vijana, na watoto pia, Jiujitahidi kuomba, “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.” (Zaburi 51:10.) Huu usafi wa moyoni na uzuri wa roho ni vyenye thamani kuliko dhahabu kwa wakati huu na kwa uzima wa milele pia. Wenye moyo safi tu ndio watakaomwona Mungu. 12 CG 417, 418;KN 211.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents