Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ukubwa wa Maendeleo ya Tabia

    Mungu amewapa wazazi kazi yao, kufanyiza tabia za watoto wao zifanane na Kielelezo Kitakatifu. Kwa neema yake wanaweza kuitimiza kazi hiyo; lakini itatakikana uvumilivu, na bidii ya kazi, nia thabiti, bila kulegea, kuiongoza nia na kuzizuia tamaa mbaya. Shamba likiachwa bila kulimwa huzaa tu miiba na mbigili. Apendaye kupata mavuno ya manufaa au mazuri hana budi kwanza kuutayarisha udongo na kupanda mbegu, kisha apalilie miche, na kuondoa kwekwe na kuulainisha udongo, ndipo mimea ya thamani itasitawi na kumlipa maridhawa kwa masumbuko na kazi yake aliyoifanya.KN 224.5

    Kuijenga tabia ndiyo kazi yenye maana sana waliyopata kukabidhiwa wanadamu na kamwe uchunguzi mkali wa kazi niyo haujapata kuwa jambo kubwa kama ilivyo sasa. Kamwe vizazi vilivyopita havikutakiwa kuyakabili mashindano makubwa namna hii; kamwe viiana wa kiume na wa kike hawakupambana na hatari zilizo kubwa kama wanavyokutana nazo siku hizi. 26169;KN 224.6

    Nguvu ya tabia ina mambo mawili-uwezo wa nia, na uwezo wa kujitawala nafsini. Vijana wengi hukosea na kuita tamaa isiyozuilika nguvu ya tabia; lakini ukweli ni kwamba mwenye kutawaliwa na tamaa yake ni mtu dhaifu. Ukuu halisi na ubora wa mtu hupimwa kwa uwezo wa maoni ya moyoni anayoyashinda, siyo kwa uwezo na wa maoni ya moyoni yanayomshinda. Mtu hodari ni yule, ambaye, huku akiwa mwepesi kutukanwa, lakini, ataizuia hasira na kuwasamehe adui zake. Watu kama hao ni mashujaa kweli kweli.KN 224.7

    Wengi wanayo mawazo kidogo sana ya vile wawezavyo kuwa hata wataendelea kudumaa na kukonda, ambapo, kama wangetumia vizuri uwezo waliopewa na Mungu, huenda wangeweza tabia bora na kutoa mvuto ambao ungeongoa watu kwa Kristo. Elimu ni uwezo; lakini uwezo wa akili bila wema wa moyoni, ni uwezo kwa mabaya.KN 225.1

    Mungu ametupa sisi uwezo wetu wa akilini na wa tabia ya moyoni, lakini zaidi sana kila mtu yu fundi mjenzi wa tabia yake mwenyewe. Kila siku jengo huzidi kupanda juu. Neno la Mungu hutuonya tujihadhari jinsi tujengavyo, tuone kuwa jengo letu limewekwa msingi wake juu ya Mwamba wa milele. Utakuja wakati ambapo kazi itadhihirika kama ilivyo hasa. Sasa ndio wakati kwa wote kukuza uwezo ambao Mungu amewapa, ili wapate kufanyiza tabia za kufaa hapa, na kwa maisha bora zaidi ya baadaye.KN 225.2

    Kila tendo la maisha, ingawa liwe dogo kama nini, lina mvuto wake katika kuifanyiza tabia. Tabia njema ni yenye thamani zaidi kuliko mali za dunia, na kazi ya kuifanyiza ndiyo kazi bora kabisa ambayo wanadamu huweza kuifanya. Tabia zinazofanyizwa kwa hali ya mambo yalivyo hubadilika na ni mbaya kabisa. Wenye tabia hizo hawana shabaha bora wala kusudi maishani. Hawana mvuto unaoadilisha tabia za wengine. Hawana kusudi wala uwezo.KN 225.3

    Muda mfupi wa maisha tuliowekwa hapa ungetumiwa vizuri kwa busara. Mungu apenda kanisa lake liwe hai, lililojitoa wakfu, lenye kufanya kazi. Lakini watu wa kanisa letu wako kinyume kabisa cha hayo wakati huu. Mungu ahitaji watu wenye nguvu, hodari, Wakristo wenye nguvu na bidii, wenye kumfuata Kielelezo wa kweli, na ambao watatoa mvuto wa nguvu kwa ajili ya Mungu na nuru. Bwana ametukabidhi amana takatifu, yenye maana sana na maneno mazito ya kweli, nasi tungeonyesha mvuto wake kwa maisha na tabia zetu. 274T 656, 657;KN 225.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents