Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mambo Yaliyompata Mtu Mwenyewe Katika Kuwaonya Watoto

  Mama wengine hawana kanuni katika kuwatendea watoto wao. Wakati mwingine huwaendekeza kwenye madhara, na pengine huwakataza furaha nzuri ambayo ingewapendeza sana watoto moyoni. Kwa kufanya hivi hawamwigi Kristo; Yeye aliwapenda watoto; aliyafahamu mawazo yao ya moyoni na kuwahurumia katika furaha zao na katika taabu zao. 28MH 389, 390;KN 225.5

  Watoto wakiomba ili waende kwa marafiki hawa au kujiunga na kundi lile la wachezaji, huwaambia: “Siwezi kuwaruhusu mwende, watoto; ketini hapa; nami nitawaambia sababu. Nafanyia kazi uzima wa milele na namfanyia Mungu kazi. Mungu amempa ninyi kama watoto wangu; kwa hiyo sina budi kuwaangalia kama mtu atakayetakiwa kutoa habari siku ya hukumu ya Mungu. Je, mwataka jina la mama yenu kuandikwa katika vitabu vya mbinguni kama mtu aliyeshindwa kufanya wajibu wake kwa watoto wake, kama mtu mwenye kumwacha adui kuingia na kutangulia kutwaa mahali ambapo yanipasa kupatwaa? Watoto, nitawaambia njia iliyo bora, ndipo mkichagua kumwasi mama yenu na kufuata njia za maovu, mama yenu hatakuwa na hatia, bali mtaangamia kwa ajili ya dhambi zenu wenyewe.”KN 225.6

  Hii ndiyo njia niliyotumia kwa watoto wangu, na kabla ya kumaliza kusema, walilia, na kupenda kusema, “Je, hutatuombea?” Naam, kamwe sikukataa kuwaombea. Nalipiga magoti karibu nao na kuomba pamoja nao. Kisha nalijitenga na kumwomba Mungu mpaka jua likapanda juu angani, usiku kucha, ili nguvu ya mvuto wa yule adui zipate kuvunjwa, nami nimepata ushindi. Ijapokuwa ilinlgharamisha kazi ya usiku mzima, lakini naliona nimelipwa kabisa wakati watoto wangu walipoweza kuning’inia shingoni mwangu na kuniambia, “Ah, Mama, twafurahi sana kwamba hukuturuhusu kwenda wakati tulipotaka kufanya hivyo. Sasa twaona kuwa ingekuwa vibaya.”KN 226.1

  Wazazi, hii ndiyo njia iwapasayo kuitumia, kana kwamba mwainuia. Hamna budi kuifanya hiyo kuwa kazi yenu ikiwa mwatazamia kuwaokoa watoto wenu katika ufalme wa Mungu. 29AH 528;KN 226.2

  Kamwe mafundisho mazuri hayawezi kutolewa kwa vijana katika nchi hii, wala katika nchi yo yote nyingine isipokuwa wametengwa mbali na miji mikubwa. Desturi na mazoea mijini huzifanya akili za vijana zisifae kuingiliwa na ukweli. 30FE 312;KN 226.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents