Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Haja Kubwa ya Wazazi ya Maongozi Ya Mungu

  Hamwezi kutoyajali malezi bora ya watoto wenu, bila ya hofu ya kupata adhabu ama matokeo mabaya baadaye. Tabia zao zilizoharibika zitatangaza kukosa uaminifu kwenu. Mabaya msiyoyasahihisha, tabia mbaya, zisizo za adabu, kukosa heshima na kutotii, mazoea ya uvivu na kutojali, yataletea majina yenu fedheha na uchungu maishani mwenu. Mwisho wa watoto wenu utakavyokuwa ni katika mikono yenu zaidi. Mkikosa kufanya wajibu wenu mwaweza kuwaweka upande wa yule adui na kuwafanya mawakili wake katika kuwaharibu wengine; ambapo, kama mkiwafundisha kwa uaminifu, ikiwa katika maisha yenu wenyewe mwawaonyesha kielelezo chema, mwaweza kuwaongoza kwa Kristo, hao nao kwa zamu yao watawavuta wengine na hivyo wengi huweza kuokoka kwa njia yenu. 317T 66;KN 226.4

  Mungu ataka sana tuwatendee watoto wetu kwa moyo mnyofu. Twaelekea kusahau kuwa watoto hawajapata kuwa na miaka mingi ya malezi ambayo watu wazima kwa umri wamekuwa nayo. Kama watoto wasipofanya sawasawa na mawazo yetu kwa kila jambo, pengine twafikiri kuwa wanastahili kukaripiwa. Lakini hilo halitasawazisha mambo. Wapelekeni kwa Mwolcozi, mwambieni habara zote; kisha amini kwamba mbaraka wake utawakalia. 32CG 287;KN 227.1

  Yafaa watoto kufundishwa kuiheshimu saa ya maombi kwa kicho. Kabla ya kuondoka nyumbani kwenda kazini, wote wa nyumbani wangeitwa mahali pamoja, na baba, au mama wakati baba asipokuwapo, angemwomba Mungu kwa bidii kuwalinda siku hiyo. Njoo kwa unyenyekevu moyo ukijawa na utu wema na kujua majaribu na hatari zilizo mbele yenu wenyewe na mbele ya watoto wenu, kwa imani wafungeni juu ya madhabahu mkiwaombea ulinzi wa Mungu. Malaika wahudumuo watawalinda watoto ambao wametolewa wakfu kwa Mungu kwa njia hiyo. Ni wajibu wa wazazi Wakristo, asubuhi na jioni kwa kuomba kwa bidii na imani daima, kufanya kitalu kuwazunguka watoto wao. Yafaa wawaamuru kwa uvumilivu, kwa upole na kuwafundisha bila kuchoka namna ya kuenenda ili kumpendeza Mungu. 331T 397, 398;KN 227.2

  Wafundishe watoto wako kuwa wamejaliwa kupata kila siku ubatizo wa Roho Mtakatifii. Hebu Kristo akupatie kuwa u mkono wake wenye kumsaidia kuyatimiza makusudi yake. Kwa sala waweza kupata jambo ambalo litaifanya huduma yako kwa watoto wako kufaulu kabisa. 34CT 131;KN 227.3

  Uwezo wa sala mama hauwezi kuthaminiwa mno kupita vile unavyostahili. (Mwanamke) mwenye kupiga magoti kando ya mwana na binti yake siku zote za mabadiliko ya utotoni, katika hatari za ujana, kamwe hatajua mpaka siku ya hukumu, mvuto wa sala zake juu ya maisha ya watoto wake. Kama akiungana kwa imani na Mwana wa Mungu, mkono wa upendo wa mama, waweza kumzuia binti yake asijifurahishe kwa anasa dhambini. Tamaa mbaya ikitaka kushinda, uwezo wa upendo, mvuto wa wenye kuzuia, wa kweli, thabiti huweza kuitegemeza roho upande wa mema. 35AH 266;KN 227.4

  Baada ya kufanya wajibu wako kwa uaminifu kwa watoto wako, ndipo wapeleke kwa Mungu na kumwomba kukusaidia; Mwambie kuwa umefanya sehemu yako, na kisha kwa imani mwombe Mungu kufanya sehemu yake, ambayo huiwezi. Mwombe kugeuza tabia zao, kuwapunguza ukali na kuwafanya wapole kwa Rono Mtakatifu. Atakusikia ukiomba. Atapenda kuyajibu maombi yako. Kwa njia ya Neno lake amekuamuru kuwarudi watoto wako, “wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia” kwao nalo Neno lake lapaswa kufuatwa katika mambo haya. 36GC 256, 257;KN 227.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents