Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wajibu wa Kanisa

  Wakati wa usiku nalionyeshwa kundi kubwa la watu ambapo jambo la elimu lilikuwa likijadiliwa na kutia wasiwasi akilini mwa watu wote waliokuwako. Mmoja ambaye amekuwa mwalimu wetu muda mrefu akawa akiwahutubia watu hao. Akasema: “Jambo hili la elimu lingekuwa lenye kulipendeza kanisa zima la Waadventista Wasabato.” 7 6T.127;KN 230.2

  Kanisa lina kazi maalum ya kufanya katika kuwaelimisha na kuwalea watoto wake ili kwa kuhudhuria shule au kuwa katika iamii yoyote nyingine wasiambukizwe na wale wenye mazoea mabaya. Ulimwengu umejaa maovu na kutojali masharti yake Mungu. Miji imekuwa Sodoma, na watoto wetu kila siku huhatarishwa kwenye maovu mengi. Wale wenye kuhudhuria shule za serikali mara nyingi hushirikiana na wengine waliotupwa zaidi, wale ambao, kando ya wakati unaotumiwa darasani, huachwa kupata elimu hafifu. Mioyo ya vijana huvutwa kwa urahisi, na kama mazingira yao yasipokuwa ya tabia nzuri, Shetani atawatumia hawa watoto waliotupwa ovyo kuwaambukiza wenzao ambao wamelelewa kwa uangalifu zaidi. Hivyo, kabla ya wazazi waishikao Sabato kujua kile kinachotendeka, mafundisho ya upotevu hujifunzwa, na roho za watoto wao wadogo huharibiwa.KN 230.3

  Jamaa wengi, ambao, kwa kusudi la kuwaelimisha watoto wao, huhamia mahali ambapo kuna shule zetu kubwa, wangemfanyia Bwana kazi njema kama wangebaki mahali walipo. Yawapasa kulitia moyo kanisa ambalo ndipo ulipo ushirika wao kuanzisha shule ya kanisa mahali watoto wao wawezapo kupokea elimu bora ya Kikristo, yenye ulinganifu. Ingekuwa bora kabisa kwa ajili ya watoto wao, kwa ajili yao wenyewe, na kwa ajili ya kazi ya Mungu, kama wangedumu kukaa kwenye hayo makanisa madogo zaidi, mahali msaada wao unapohitajiwa, badala ya kwenda katika makanisa makubwa, ambapo, kwa sababu ya kutotakikana huko, kuna hatari siku zote ya kutumbukia kwenye jaribu la ulegevu wa kiroho.KN 230.4

  Po pote penye wachache waishikao Sabato, wazazi wangejiunga kutayarisha mahali pa shule ya kutwa ambapo wanafunzi huhudhuria mchana na kulala makwao, mahali watoto na vijana wawezapo kufundishwa. Yafaa wamwajiri mwalimu Mkristo, ambaye, kama mmishenari aliyejitoa wakfu kwa Mungu, atawae-limisha watoto kwa njia ambayo itawaongoza kuwa wamishenari. 8.KN 230.5

  Tumo chini ya agano zito na lililo takatifu kwa Mungu kuwalea watoto wetu kwa ajili yake wala si kwa ajili ya walimwengu; kuwafundisha wasishikamane na walimwengu bali wampende na kumcha Mungu na kuzishika amri zake. Yapasa watiwe mioyoni mwao wazo hili, waone kuwa wameumbwa kwa sura ya Mungu aliye Muumbaji wao na ya kwamba Kristo ndiye kielelezo chema ambacho wamepaswa kukifuata, ili kufanana naye. Uangalifu mwingi watakikana sana juu ya elimu ambayo ltawafunuha na kuwajulisha habari za wokovu, na kufanya maisha na tabia ya mtu ifanane na ile ya Mungu mwenyewe. 9.KN 231.1

  Ili kutimiza haja ya watenda kazi, Mungu anataka sana kuwa vyuo vikuu vianzishwe katika nchi mbalimbali mahali wanafunzi wa ahadi wawezapo kuelimishwa juu ya sehemu za elimu ifaayo na katika kweli ya Biblia. Kadiri watu hawa wanavyoshughulika kazini, ndivyo watakavyoifanya kazi hii ya neno la kweli kwa wakati huu iwe kama ipaswavyo na kutofautikiana na kazi zingine mahali papya.KN 231.2

  Isipokuwa tu kwa habari ya elimu ya wale ambao hawana budi kutumwa nje kama wamishenari, ingefaa watu wa sehemu za nchi mbalimbali ulimwenguni wafundishwe kufanya kazi kwa watu wa kwao, miongoni mwa majirani zao wenyewe; kadiri iwezekanavyo ni bora na salama zaidi kwao kupata elimu mahali pale pale watakapofanyia kazi. Isipokuwa mara chache tu, si vizuri, licha kwa mtenda kazi mwenyewe, hata kwa ajili ya maendeleo ya kazi, kwenda kusomea nchi za mbali. 106T.137;KN 231.3

  Kama kanisa, kama mtu mmoja mmoja peke yake, tukipenda kusimama bila hatia hukumuni, hatuna budi kujitahidi zaidi kwa moyo kuwaelimisha vijana wetu, ili wafae zaidi kwa sehemu mbalimbali za kazi hii kubwa iliyowekwa mikononi mwetu. Yatupasa tufanye mipango kwa busara, ili wale wenye talanta ya akili wapate kuimarishwa akili zao na kuadilishwa na kupewa malezi mema hata wawe na ubora sawa na ule wa mbinguni, ili kazi ya Kristo isipingwe kwa ajili ya utovu wa watenda kazi waelekevu, ambao wataifanya kazi yao kwa bidii na uaminifu. 11CT.43;KN 231.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents