Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sifa za Mwalimu wa Shule

    Pateni mtu aliye hodari awe mkuu wa shule yenu, mtu ambaye nguvu za mwili wake zitamsaidia kufanya kazi kikamilifu kama mtawala ama mlezi mwema; mtu ambaye anastahili kuwalea watoto na kuwafanya wawe na mazoea mema ya utaratibu, unadhifu na utendaji wa kazi. Tenda kazi kikamilifu kwa lo lote ufanyalo. Karna ukiwa mwaminifu katika kuwafundisha mafundisho ya kawaida wanafunzi wako wengi wataweza kutoka shuleni na kusnika kazi kama wainjilisti. Hatuna sababu ya kufikiri kuwa ni lazima watenda kazi wote wawe na elimu ya juu. 18CT.213,214 ;KN 233.5

    Katika kuwachagua walimu, yatupasa tuangalie sana kabla hatujawachagua, tukijua kuwa hili ni jambo kubwa, la dini, kama ilivyo katika kuwachagua watu kwa kazi ya uchungaji wa kanisa. Watu wenye busara ambao wanaweza kupambanua tabia za watu wangefanya uchaguzi huo; kwa kuwa mwenye kipawa bora sana ndiye anayetakiwa kuwaelimisha na kuwaadilisha watoto, na kuendesha kazi mbalimbali zitakazobidi kutendwa na walimu katika shule zetu za kanisa Msiweke walimu vijana, wasio na utawala; kwa kuwa jitihada zao zitaleta machafuko. 19CT.174,175;KN 234.1

    Pasiwepo mwalimu anayeajiriwa, isipokuwa mmemshuhudia na kumpima kwa majaribio, mkaona kuwa anampenda na kumcha Mungu. Kama walimu wamefundishwa na Mungu, na kama mafundisno yao kila siku hutokana na Kikristo, watafanya kazi ya Kristo. Watawaongoa watu pamoja na Kristo; kwa kuwa kila mtoto na kila kijana ni mwenye thamam kuu. 20FE.260 ;KN 234.2

    Yafaa mazoea na kanuni za mwalimu zikumbukwe kuwa ni mambo makubwa kuliko elimu yake. Kusudi awe na mvuto yampasa ajitawale kabisa yeye mwenyewe, na moyoni mwake mwenyewe ajawe na upendo kwa wanafunzi wake, ambao utaonekana katika uso, maneno, na matendo yake. 21FE19 ;.KN 234.3

    Yampasa mwalimu siku zote afanye kiungwana kama Mkristo mwema. Yampasa awe na moyo wa kirafiki na mshauri mwema kwa wanafunzi wake. Kama watu wote wa kanisa letu walimu, wachungaji, na washiriki wa kanisa wangekuza moyo wa uadilifu na adabu ya Kikristo, wangepata kwa urahisi zaidi njia ya kuifikia mioyo ya watu; wengi zaidi wangeongozwa kulichunguza na kulipokea neno la kweli. Kila mwalimu atakapowafikiria wengine kuliko nafsi yake mwenyewe, na kupendelea sana maendeleo na mafanikio ya wanafunzi wake, akijua kuwa wao ni mali ya Mungu, na ya kwamba hana budi kutoa habari za mvuto wake juu ya nia na tabia zao, ndipo tutakuwa na shule ambayo malaika watapenda kukaa humo bila kuondoka upesi. 22CT.93,94 ;KN 234.4

    Shule zetu zahitaji walimu wenye sifa bora za uadilifu; wale ambao huweza kuaminiwa; wale ambao wana nguvu katika imani, na wenye akili na uvumilivu; wale wenye kutembea pamoja na Mungu, na kujiepusha na hatua ya kwanza kabisa ya maovu.KN 234.5

    Kuwaweka watoto wetu wadogo kwa walimu wenye kiburi na wasio wazuri ni dhambi. Mwalimu wa aina hiyo atasababisha madhara makubwa kwa hao ambao hukuza tabia kwa upesi. Kama walimu hawamtii Mungu, ikiwa hawana upendo kwa watoto wanaowaongoza, au kama huonyesha upendeleo kwa wale wenye sura zinazowapendeza, kutowajali wale wasio wazuri wa sura, wala wale walio watukutu na dhaifu, haifai kuajiriwa; maana kazi yao itamletea Kristo hasara ya roho za watu. Huhitajiwa, hasa kwa watoto, walimu ambao ni watulivu na wema, wanaoonyesha uvumilivu na upendo kwa wale hasa wanaouhitaji sana. 23CT.175,176 ;KN 234.6

    Mwalimu atapoteza kiini hasa cha elimu, kama asipofahamu haja yake ya maombi, na kunyenyekea moyoni mwake mbele za Mungu. 24CT.231 ;KN 235.1

    Ukubwa wa sifa za afya ya mwalimu ni vigumu kuudhania kuwa jambo kubwa kuliko ulivyo; kwa kuwa kadiri afya yake inavyozidi, ndivyo na kazi yake itakavyozidi kukamilika. Akili haziwezi kuflkin barabara na kuwa na nguvu kutenda kazi ikiwa nguvu za mwili zimedhurika kwa sababu ya udhaifu au ugonjwa. Moyo hushindwa na mawazo; lakini ikiwa, kwa sababu ya udhaifu wa mwili, ubongo kupotewa na nguvu zake, hapo ndipo njia ya maoni bora ya moyoni na makusudi safi itakuwa imezuiwa, na mwalimu hawezi tena kupambanua baina ya jema na baya. Ukiumwa na ugonjwa, si jambo rahisi kufurahi, wala kufanya kazi kwa uaminifu na haki. 25.KN 235.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents