Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 41 - Vyakula vya Nyama

    MUNGU aliwapa wazazi wetu wa kwanza chakula alichokusudia wanadamu wakile. Ilikuwa kinyume cha mpango wake kuua kiumbe cho chote. Hakupasa pawepo mauti katika Edeni. Matunda ya miti bustanini, yalikuwa chakula alichohitaji mwanadamu. Mungu hakumruhusu mwanadamu kula nyama mpaka baada ya gharika. Kila kitu ambacho mwanadamu angeweza kuponea kilikuwa kimekwisha kuharibiwa, na kwa hiiyo Mungu akampa Nuhu ruhusa kwa ajili ya riziki yao kula wanyama safi aliokuwa amewachukua ndani ya safma. Lakini nyama haikuwa chakuia chenye kutia afya kwa mwanadamu.KN 258.1

    Baada ya gharika watu walikula zaidi chakula cha nyama. Mungu aliona kuwa njia za mwanadamu zilikuwa mbovu, na ya kuwa huelekea kujiinua kwa kiburi na kufanya kinyume cha mwumbaji wake na kufuata tamaa za moyo wake mwenyewe. Naye akawaruhusu watu wale waliokuwa wenye maisha marefu kula chakula cha nyama apate kuyafupisha maisna yao ya dhambi. Mara baada ya gharika watu wakaanza kupungua upesi kimo na miaka. 1CD 373;KN 258.2

    Katika kukiteua chakula cha mwanadamu Edeni, Mungu alionyesha kile ambacho kilikuwa bora kuliko vingine vyote; katika kuteua Israeli alifundisha fundisho lile. Kwa njia yao alitaka sana kuwabariki na kuwafundisha walimwengu. “Mkate wa mbinguni.” Kwa sababu tu ya kutoridhika kwao na kunung’unika kwao kwa ajili ya vyungu vya nyama ya Misri ndiyo sababu tu iliyoacha wanewe chakula cha nyama, nacho kilitolewa kwa muda mfupi tu. Kukitumia kulileta magonjwa na kufa kwa maelfu. Ingawa ya hayo kutumia chakula kisicho cha nyama halikuwa jambo lililopendwa kwa moyo. Kikaendelea kuwa asili ya kutoridhika na kuleta manung’uniko wazi au siri, nacho hakikufanywa kiwe cha daima.KN 258.3

    Katika kukaa kwao Kanaani, Waisraeli waliruhusiwa kutumia chakula cha nyama, lakini kwa masharti maalumu, ambayo yalielekea kupunguza matokeo mabaya ya baadaye. Kutumia nyama ya nguruwe kulikatazwa, na pia nyama ya wanyama wengine na ndege na samaki wengine hawakuwa halali. Juu ya nyama lliyoruhusiwa, kula shahamu na damu kulikatazwa vikali.KN 258.4

    Wanyama hao waliweza tu kutumiwa kwa chakula wakiwa katika hali njema. Hakuna kiumbe kilichoraruliwa, kilichokufa chenyewe, wala kisichotolewa damu kwa uangalifu, kilichoweza kutumiwa kwa chakula.KN 258.5

    Kwa kuasi mpango wa Mungu ulioamriwa kwa habari za chakula. Waisraeli walipata hasara kubwa. Walikitamani chakula cha nyama, wakavuna matokeo yake ya baadaye. Hawakukifikia kipeo cha Mungu cha tabia wala kulitimiza kusudi lake. Bwana “akawapa walichomtaka, akawakondesha roho zao” (Zab. 106:15). Walithamini anasa za dunia zaidi ya mambo ya kiroho, na hawakupata sifa takatifu ambayo aliwakusudia.KN 259.1

    Wale wanaokula nyama hula nafaka na mboga za majani zilizokwisha kutumika; maana mnyama hupata kutoka kwa vitu hivyo chakula ambacho husaidia kukua. Uzima uliokuwa ndani ya nafaka hizo hupita na kuingia ndani ya mwenye kuzila. Twaupokea kwa kula nyama ya mnyama hatimaye. Basi, ingekuwa bora kama nini kuupata moja kwa moja, kwa kula chakula ambacho Mungu ametupa sisi kukitumia! 2MH 311 - 313;KN 259.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents