Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Nguruwe Ni Najisi Kwenu”

  Nyama ya nguruwe ina wingi wa vijidudu vya magonjwa; juu ya nguruwe Mungu amesema: “Huyu ni najisi kwenu; msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse” Kumbukumbu 14:8. Amri hiyo ilitolewa kwa sababu nyama ya nguruwe haifai kwa chakula. Nguruwe ni wanyama. Kamwe kwa hali iwayo yote, nyama yao haikustahili kuliwa na wanadamu. Haiwezekam kwa nyama ya kiumbe cho chote chenye uhai kuwa kitu kizuri kwa chakula ikiwa chakula cha kiumbe hicho ni uchafu, na kiumbe huyo akiwa mwenye kula kitu kibaya, chenye kuchukiza. 7MH 313, 315;KN 260.1

  Nyama ya nguruwe, ijapokuwa ni mojawapo ya vyakula vikuu, ni mojawapo ya vitu vyenye madhara makubwa. Mungu hakuwakataza Waebrania kula nyama ya nguruwe kwa kuonyesha tu madaraka yake, bali kwa sababu haikuwa kitu kizuri kwa chakula cha mwanadamu. Ingeweza kuujaza mwili vijidudu vya ugonjwa wa kuvimba, na hasa kwa kuwa katika hali ya nchi za joto huleta ukoma, na magonjwa ya namna nyingine mbalimbali Matokeo yake mwilini katika hali hiyo ya nchi yalikuwa mabaya zaidi kuliko katika nchi za baridi Nyama ya nguruwe zaidi ya nyama ya wanyama wengine wote, huleta hali mbaya katika damu. Wale wenye kula sana nyama ya nguruwe huweza kuambukizwa ugonjwa. 8CD 392,393;KN 260.2

  Hasa misnipa mizuri ya fahamu ya ubongoni hudhoofishwa na kufanywa isiweze kufahamu mambo matakatifu, ila kuwekwa chini kwenye mambo hafifu. 92T 96;KN 260.3

  Wale wenye kufanya mazoezi mengi nje hawapatwi na madhara ya kula nyama ya nguruwe, kama wale ambao maisha yao ni ndani ya nyumba saa nyingi, na ambao wanayo mazoea ya kukaa kitako, na wenye kazi za kutumia akili. 10CD 393;KN 260.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents