Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Madhara Yake Akilini na Rohoni

  Ubaya wa nyama kwa tabia ya moyoni haupungui neno lo lote kwa yale madhara yake mwilini. Chakula cha nyama ni chenye kudhuru afya, na ijapokuwa matokeo yake mwilini yawe ya namna gani huwa yenye kudhuru akili na roho pia. 11MH 315;KN 260.5

  Chakula cha nyama huibadili tabia na kutia nguvu hali ya kuvutwa kwa tamaa za mwili tu. Miili yetu hufanywa na chakula tulacho, na kula nyama kwa wingi kutapunguza uhodari wa akili. Wanafunzi wangeweza kufaulu mambo mengi zaidi katika masomo yao kama wasingeonja nyama. Kadiri minofu ya mwili wa mtu inavyotiwa nguvu kwa kula nyama, ndivyo uwezo wa akili unavyopungua. 12CD 389;KN 260.6

  Kama kuna wakati ambapo yafaa chakula kiwe chepesi sana, sasa ndio wakati huo. Haifai kuweka nyama mbele ya watoto wetu. Madhara yake ni yenye kusisimua na kutia nguvu tamaa mbaya, na huelekea kuua uwezo wa tabia ya adili. 132T 352;KN 261.1

  Yafaa matengenezo makubwa zaidi yaonekane miongoni mwa watu wanaodai kutazamia kutokea kwa Kristo upesi. Matengenezo ya afya (health reform) hayana budi kufana miongoni mwa watu wa kanisa letu, kazi ambayo bado haijapata kutendeka. Kuna wale ambao yapasa kuamshwa waione hatari ya kula nyama, ambao wangali wakiila nyama ya wanyama na kwa njia hiyo kuihatarisha hali ya afya ya mwili, akili, na ya kiroho. Wengi ambao hivi sasa wameongoka nusu tu juu ya jambo hili la kula nyama watawaacha watu wa Mungu, wasifuatane nao tena. 14CH 575;KN 261.2

  Wale ambao hudai kuliamjtii neno la kweli yawapasa kuzilinda kwa uangalifu nguvu za mwili na za akili, kusudi Mungu na kazi yake asidharauliwe kwa njia yoyote kwa maneno yao wala kwa matendo yao. Mazoea na desturi havina budi kuwekwa chini ya mapenzi yake Mungu. Yatupasa kuangalia sana chakula chetu. Nalionyeshwa dhahiri kuwa watu wa Mungu yawapasa kusimama imara kupingana na ulaji wa nyama. Je, Mungu kwa miaka arobaini angewapa watu wake ujumbe kwamba ikiwa wanataka kuwa na damu safi na akili timamu hawana budi kuacha kutumia nyama, hali ya kinyama hutiwa nguvu na hali ya kiroho hudhoofishwa. 15 CD 383;KN 261.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents