Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Njozi Isiyoweza Kusimuliwa

  Katika mikutano ya Salamanca, New York, Novemba, 1890, ambapo Ellen White alikuwa akiihutubia mikutano mikubwa ya watu, alidhoofika kabisa, kwa kuwa alishikwa na ugonjwa wa mafua makali alipokuwa safarini kwenda katika mji huo. Baada ya mmojawapo wa mikutano hii akaondoka kwenda chumbani mwake akiwa amekata tamaa na huku yu mgonjwa. Akawa anafikiri kusali mbele za Mungu na kumtolea moyo wake kuomba rehema na afya na nguvu. Akapiga magoti kando ya kiti chake, na kwa maneno yake mwenyewe, akisimulia kilichotukia, anasema:KN 28.5

  “Nalikuwa sijatamka neno wakati chumba chote kilipoonekana kana kwamba kimejawa na nuru nyeupe na uchungu wangu na kukata tamaa kuondolewa. Nikajazwa faraja na tumainiamani ya Kristo.”KN 28.6

  Kisha akapewa njozi. Baada ya njozi hii hakutaka kulala tena usingizi. Hakutaka kupumzika. Alikuwa ameponywa-alikuwa amepumzishwa.KN 28.7

  Asubuhi ilibidi kuamua. Ama aendelee na kwenda mahali pa mikutano ifuatayo, ama hana budi kurejea nyumbani kwake Battle Creek., Mchungaji. A.T. Robinson, aliyekuwa mkuu wa kazi na Mchungaji William White, mwana wa Bibi White wakaitwa chumbani mwake kupata jibu lake. Wakamkuta amevaa nguo, yu mzima. Alikuwa tayari kwenda. Akasimulia jinsi alivyopona. Akahadithia njozi hiyo. Akasema, “nataka kuwaambia jambo lililofunuliwa kwangu usiku huu uliopita. Katika njozi nalielekea kana kwamba niko Battle Creek, na malaika mjumbe akaniambia, “Nifuate” Kisha akasita. Hakuweza kuikumbuka. Akajaribu mara mbili kuisimulia, lakini hakuweza kukumbuka kile alichoonyeshwa. Katika siku za baadaye akaandika kile alichokuwa ameonyeshwa. Kilikuwa mipango iliyofanywa kwa ajili ya gazeti letu la Uhuru wa Dini lililoitwa siku zile The American Sentinel.KN 29.1

  “Usiku nilikuwa kwenye mabaraza kadha wa kadha, na hapo nilisikia maneno yaliyorudiwa na watu wenye nguvu kuongoza kwenye matokeo mema kwamba kama The American Sentinel lingeacha kutumia maneno haya ‘Waadventista Wasabato katika safu zake, na lisiseme lo lote juu ya Sabato, watu mashuhuri ulimwenguni wangependelea kulinunua; nalo lingependwa na wengi, na kufanya kazi kubwa zaidi. Hili likahesabiwa kuwa jambo la kupendeza.”KN 29.2

  “Nikaona nyuso zao ziking’aa nao wakaanza kuifuata njia hiyo kulifanya gazeti la The Sentinel kuwa la kupendwa na watu wengi. Shauri hili lote lilianzishwa na watu waliotaka sana ukweli uwepo akilini na moyoni.”KN 29.3

  Ni dhahiri kwamba aliona kundi la watu likijadiliana juu ya mashauri ya utengenezaji wa gazeti hili. Kikao cha Halmashauri Kuu kilipofunguliwa Machi, 1891, Mama White akaombwa kuzungumza na watenda kazi kila siku asubuhi saa kumi na moja na nusu na kuhutubia kikao cha watu elfu nne siku ya Sabato alasiri. Fungu lake la Biblia siku ya Sabato alasiri lilikuwa. “Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” Mazungumzo yote yalikuwa ombi kwa Waadventista Wasabato kushikilia mambo yanayoonyesha imani yao. Mara tatu wakati wa mkutano huu alianza kusimulia ile njozi ya Salamanca, lakini kila mara alizuiwa. Mambo ya njozi hii yalimpotea akilini kwa urahisi. Kisha akasema, “Juu ya hii, nitakuwa na mengi ya kusema baadaye.” Akayasawazisha mahubiri yake kwa muda wa saa moja hivi, akamaliza vizuri, na watu wakaruhusiwa kuondoka na kwenda zao kutoka katika mkutano. Wote walikuwa wameona kuwa hakuweza kuikumbuka njozi hiyo.KN 29.4

  Kiongozi wa Halmashauri Kuu akamwendea na kumwuliza kama angechukuwa mkutano wa asubuhi.KN 29.5

  Akajibu, “La, nimechoka; nimetoa ushuhuda wangu. Huna budi kufanya mipango mingine kwa ajili ya mkutano wa asubuhi.” Mipango mingine ikafanywa.KN 30.1

  Bibi White aliporudi kwake akawasimulia watu wa nyumbani mwake kuwa hakukubali mkutano wa siku ile kwa kuwa hakukubali kuhudhuria mkutano wa siku ile asubuni. Alichoka, naye alitumaini kupumzika. Alikusudia kupumzika ndani Jumapili asubuhi ndivyo alivyopanga katika makusuai yake.KN 30.2

  Usiku ule, baaaa ya kikao cha Halmashauri Kuu kumalizika, kundi dogo la watu likakutanika katika mojawapo ya ofisi kwenve jengo la Review and Herald. Katika mkutano huo palikuwako wajumbe wa Nyumba ya uchapaji ambayo ilitoa gazeti la The American Sentinel; na pia walikuwako wajumbe wa Religious Liberty Association, (Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini). Walikuwa wamekutana kujadili na kukata shauri juu ya neno la kutatiza sana-mpango wa utengenezaji wa The American Sentinel. Mlango ulikuwa umefungwa, na wote wakakubaliana kuwa mlango hautafunguliwa mpaka shauri hili liamuliwe.KN 30.3

  Punde kabla ya saa tisa za usiku kabla ya kupambazuka Jumapili mkutano huu ukaisha kwa kupingana kwa madai ya upanae wa watu wa Religious Liberty (Kutetea Uhuru wa Dini kwamba Pacific Press isipokubali madai yao na kuacha kutaja jina la “Waadventista” na “Sabato” katika safu za gazeti hilo, hawatalitumia tena kama gazeti la Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini. Hivyo maana yake ni kuliua hili gazeti. Wakafungua mlango, na watu wakaenda nyumbani mwao, wakaenda vitandani, na kulala usingizi.KN 30.4

  Lakini Mungu, ambaye kamwe hasinzii wala kulala usingizi, akamtuma malaika wake mjumbe kwa chumba cha Ellen G. White saa tisa ya usiku ule. Akaamshwa usingizini mwake na kuamriwa kuwa hana budi kwenda katika mkutano wa watenda kazi saa kumi na moja na nusu, na hapo hana budi kutoa mambo aliyoonyeshwa Salamanca. Akavaa nguo, akaenda dawatini mwake, akatwaa daftari alimoandika mambo aliyokuwa ameyaonyeswa Salamnca. Maono yalipozidi kudhihirika wazi akilini mwake, akaandika zaidi mambo ya kwenda nayo.KN 30.5

  Wahubiri walikuwa wakiinuka kutoka katika kusali Kanisani wakati Mama White alipoonekana akiingia mlangoni, akiwa na bunda la maandishi kwapani. Kiongozi wa Halmashauri Kuu ndiye aliyekuwa mhubiri, na akamsemesha:KN 30.6

  Akamwambia, “Mama White, tumefurahi kukuona. Je, unao ujumbe kwetu?” Akamwambia, “Ndiyo ninao,” na akaenda mbele. Kisha akaanzia mahali alipoachia mazungumzo yake siku iliyopita. Akawaambia kuwa saa tisa usiku ule alikuwa ameamshwa usingizini mwake na kuamriwa aende kwenye mkutano wa watenda kazi saa kumi na moja na nusu na hapo atoe mambo aliyokuwa ameonyeshwa Salamanca.KN 30.7

  Akasema, “Katika njozi, nalionekana kana kwamba niko Battle Creek. Nalichukuliwa mpaka katika ofisi ya Review and Herald, na yule malaika mjumbe akaniamuru, ‘Nifuate.’ Nikachukuliwa chumbani mahali kundi fulani la watu walipokuwa wakijadiliana sana shauri moja. Palionyeshwa moyo wa biaii, lakini sio wa hekima.” Akasema jinsi walivyokuwa wakijadili mpango wa utengenezaji wa The American Sentinel, akasema “Naliona mmoja wa watu hawa akitwaa nakala ya The Sentinel akaishikilia juu ya kichwa chake, na kusema, ‘Isipokuwa habari hizi juu ya Sabato na Kuja kwa Kristo Mara ya Pili zimeondoka gazetini humu, hatuwezi kulitumia tena kama gazeti la Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini (Religious Liberty Association) ” Ellen G. White akazungumza muda wa saa moja, akieleza mkutano ule mambo aliyoonyesnwa katika njozi miezi kadha wa kadha zamani, na akitoa onyo lenye msingi juu ya mafunuo yale. Kisha akaketi.KN 31.1

  ..Kiongozi wa Halmashuri Kuu akawa na wasi wasi asijue la kufanya juu ya neno hili. Kamwe alikuwa hajakuwa na mkutano wa namna hii. Lakini hawakungojea muda mrefu kupata maelezo; maana mtu mmoja alisimama upande wa nyuma wa chumba, naye akaanza kusema:KN 31.2

  “Nilikuwa katika mkutano huo usiku huu uliopita.” Ellen White akasema, “Usiku huu uliopita, usiku wa leo? Nilidhani mkutano huo ulifanyika miezi kadha wa kadha zamani, nilipoonyeshwa habari zake katika njozi.”KN 31.3

  Akasema, “Nilikuwa katika mkutano huo usiku huu uliopita, nami ndiye mtu ambaye alisema maneno yale juu ya habari katika gazeti hilo, nikiliinua juu kichwani mwangu. Nasikitika kusema kwamba nilikuwa upande mbaya; lakini nachukua nafasi hii kujiweka upande mzuri.” Akaketi chini.KN 31.4

  Mtu mwingine akasimama kusema. Alikuwa ndiye mkuu wa Chama cha Uhuru wa Kutetea Dini. Tazama maneno yake; “Nilikuwa katika huo mkutano. Usiku huu uliopita baada ya kufunga kikao baadhi yetu tulikutanika chumbani mwangu katika ofisi ya Review mahali tulimojifungia na hapo tukajadili maswali na shauri ambalo tumepewa asubuhi hii. Tuhkaa katika chumba kile mpaka saa tisa usiku wa leo. Kama ningeanza kutoa maelezo ya mambo yaliyofanyika na moyo wa kila mtu aliyekuwako chumbani humo, singeweza kuyatoa kwa uhalisi na kwa usahihi kama yaliivyotolewa na Mama White. Sasa naona kuwa nilikosea na ya kwamba madaraka niliyojitwalia yalikuwa si halali. Kwa nuru ambayo imetolewa asubuhi hii, nakiri kwamba nilikosa.”KN 31.5

  Wengine walisema siku ile. Kila mtu aliyekuwa katika mkutano ule usiku uliopita alisimama na kutoa ushuhuda wake, akisema kuwa Ellen White alikuwa ameeleza kwa usahihi mkutano ule na moyo wa wale waliokuwako chumbani. Kabla ya kufungwa kwa mkutano siku ile ya Jumapili asubuhi, kundi la Chama cha Kutetea Uhuru wa Dini waliitwa wakusanyike pamoja, nao wakavunja mapatano waliyofanya mbele ya saa tano tu zilizopita.KN 32.1

  Kama Mama White asingezuiliwa naye angaliieleza njozi ile siku ya Sabato alasiri, ujumbe wake usingetimiza kusudi ambalo Mungu aliikusudia, maana mkutano ule ulikuwa bado kufanyika.KN 32.2

  Lakini watu wale hawakutumia onyo kubwa lililotolewa siku ya Sabato alasiri. Walidhani wanajua mambo viziri zaidi. Pengine Mama White hakufahamu,” au “Tunaishi wakati mwingine sasa,” au “Onyo hilo lilihusu miaka ya zamani, lakini je halitufai sasa?” Mawazo ambayo Shetani huyanong’ona kwetu siku hizi ni yale yale aliyotumia kuwashawishi wale watu mwaka 1891. Mungu, wakati aliochagua mwenyewe na kwa njia yake mwenyewe, alidhihirisha wazi kwamba ilikuwa kazi yake; alikuwa akiongoza; alikuwa akiendesha. Ellen G. White atwambia kwamba Mungu “mara nyingi ameyaruhusu mambo yaelekee kuleta hatari, ili kuingilia kwake katika mambo hayo kufahamike. Ndipo atakuwa amedhihirisha kuwa kuna Mungu katika Israeli.”KN 32.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents