Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    “Fanyeni Yote kwa Utukufu wa Mungu”

    Hatuchori mstari halisi wa kufuatwa katika chakula; lakini twasema kuwa katika nchi zenye matunda, nafaka, na mbegu jamii ya njugu kwa wingi, nyama si chakula bora kwa watu wa Mungu. Nimeamriwa kuwa nyama yaelekea kufanya mwili uwe na tamaa mbaya za kinyama, kuwanyang’anya wanaume na wanawake ule upendo na huruma ambazo yawapasa kuwa nazo kwa kila mmoja wao, na kuacha tamaa mbaya za mwili kutawala uwezo bora wa mtu. Ikiwa kula nyama kulipata kuwa jambo la manufaa kwa afya, sasa si salama. Magonjwa ya donda baya ‘saratani,’ uvimbe, na magonjwa ya kifua hutokana zaidi na kula nyama.KN 266.2

    Haitupasi kufanya ulaji wa nyama kipimo cha ushirika, lakini yafaa kufikiri mvuto wa wale wanaodai kuwa ni waumini ambao hutumia nyama, juu ya wengine. Je, kama wajumbe wa Mungu, hatutawaambia watu: “Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu?” (1 Wakorintho 10:31). Je, tusitoe ushuhuda thabiti kupinga tamaa ya chakula iliyopotoka? Je, mhubiri awaye yote wa Injili, mwenyewe kulihubiri neno la kweli zito lililopata kupewa wanadamu, ataonyesha kielelezo kwa kuvirudia vyungu vya nyama ya Misri? Je, wale ambao hulipwa kutoka katika nyumba ya Mungu watakubali kwa kujifurahisha kwa anasa kutia sumu mkondo wenye kutia uzima unaotiririka mishipani mwao? Afya ya mwili haina budi kuhesabiwa kuwa kitu cha maana kwa kukua katika neema na upataji wa moyo mtulivu. Kama tumbo lisipotunzwa vizuri, kufanywa kwa tabia nyofu na ya uadilifu kutazuiwa. Ubongo na neva hulihurumia tumbo. Kula na kunywa ambako kuna makosa huleta kufikiri na kutenda kwenye makosa.KN 266.3

    Wote sasa wanapimwa kuthibitishwa. Tumebatizwa katika Kristo, na ikiwa tutafanya wajibu wetu kwa kujitenga na kila kitu kiwezacho kutuburura chini na kutufanya tuwe vile isivyotupasa kuwa, tutapewa nguvu kukua ndani ya Kristo, ambaye yu kichwa chetu chenye uhai, nasi tutaona wokovu wa Mungu.KN 266.4

    Tukiwa tu wenye akili juu ya kanuni za maisha ya afya ndipo tuwezapo kuamshwa kabisa kuona mabaya yanayotokana na chakula kisichofaa. Wale ambao baada ya kuyaona makosa yao, wana moyo kuyabadili mazoea yao, wataona kuwa njia ya matengenezo huhitaji jitihada na uvumilivu mwingi; lakini tamaa nzuri za chakula zikiisna kufanywa, watatambua kuwa kutumia chakula ambacho kwanza kilihesabiwa kuwa kisicho na madhara kuliweka pole pole msingi wa ugonjwa wa kutokiweza chakula vizuri tumbom na magonjwa mengine.KN 267.1

    Baba na mama, kesheni na kuomba. Jihadharini juu ya kutokuwa na kiasi kwa namna iwayo yote. Wafundisheni watoto wenu kanuni za matengenezo halisi ya afya. Ghadhabu ya Mungu imeanza tayari kuwapatiliza wana wa uasi. Uhalifu wa sheria kama nini, dhambi kama nini, maovu kama nini, hudhihirishwa kila upande? Kama watu yatupasa kutumia uangalifu mkubwa katika kuwalinda watoto wetu na marafiki wabaya.KN 267.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents