Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Fundisheni Watu

    Yafaa jitihada kubwa zaidi kutolewa kuwafundisha watu kanuni za matengenezo ya afya bora. Shule za upishi zingeanzishwa, na mafundisho yangetolewa nyumba kwa nyumba juu ya upishi wa chakula kizuri kwa afya. Yawapasa wazee na vijana kujimnza jinsi ya kupika chakula chepesi zaidi. Po pote neno la kweli lifundishwapo, yapasa watu wafundishwe jinsi ya kutayarisha chakula kwa njia nyepesi, tena ya kukifanya kiwe na ladha. Yafaa waonyeshwe kuwa cnakula kitiacho afya chaweza kupatikana bila ya kutumia nyama.KN 267.3

    Wafundisheni watu kuwa ni heri kujua jinsi ya kujitunza katika hali njema ya afya kuliko kujua jinsi ya kutibu ugonjwa. Yafaa madaktari wetu wawe walimu wenye busara, wanaowaonya wote juu ya kujifurahisha kwa anasa na kuonyesha kuwa kutokula vitu ambavyo Mungu amevikataza ndiyo njia tu ya kuulinda mwili na akili visipatwe na uharibifu.KN 267.4

    Yafaa akili na busara nyingi zitumiwe katika kukitayarisha chakula kitiacho afya badala ya kile ambacho zamani kilifmywa kuwa chakula cha nao wenye kujifunza kuwa viongozi wa haya matengenezo ya afya. Imani kwa Mungu, kusudi la kweli, na hiari ya kusaidiana vinahitajika. Chakula kisicho na sehemu nzuri zenye kuulisha mwili huyaletea matengenezo ya afya fedheha. Sisi tu wenye kufa, nasi hatuna budi kujipatia chakula bora ambacho kitautia mwili afya.KN 267.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents