Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Onyesho la Dini Lifaalo

  Upungufu wo wote wa kazi itendwayo kwa bidii na ya uaminifu kwa Mungu husingizia uwongo dini yetu. Dini ya Kikristo ambayo tu hudhihirishwa kwa kazi ya uaminifu, ifaayo, ndiyo itakayowachoma mioyo wale ambao wamekufa katika uhalifu wa sheria na dhambi. Wakristo wenye kumwomba Mungu wanyenyekevu, na waaminio, wenye kuonyesha kwa matendo yao kuwa shauku yao kuu ni kuwajulisha wengine Neno la kweli liokoalo ambalo halina budi kuwajaribu watu wote, watavuna mavuno makubwa va roho kwa Bwana.KN 72.3

  Hakuna udhuru uwezao kutolewa kwa ajili ya imani ya makanisa yetu kuwa hafifu hivi na dhaifu. “Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini” (Zekaria 9:12). Pana nguvu kwa ajili yetu ndani ya Kristo. Yu Mwombezi wetu mbele za Baba. Anatuma wajumbe wake kila upande wa ufalme wake kupeleka habari za mapenzi yake kwa watu wake. Anatembea miongoni kuwaadilisha wafuasi wake. Mvuto wa wale ambao humwamini kwa kweli utakuwa harufu ya uzima ulimwenguni. Anashikilia nyota katika mkono wake wa kuume, na ni kusudi lake kuiacha nuru yake iangaze kwa njia ya hawa kwa walimwengu. Hivyo anataka kanisa la juu. Ametupa sisi kazi kuu kufanya, tuonyeshe maishani mwetu kile Neno la Mungu lilichofanya. Hebu tuifanye kwa usahihi na nia. Imegharamu kujikana nafsi, kujinyima, nguvu zisizoshindika, na sala nyingi kukuza kazi ya kuihubin injili mahali inaposimama sasa. Kuna hatari kwamba baadhi ya wale ambao sasa wanashika kazi wataridhika na kuwa watu wasiofanya kazi vizuri, wakiona moyoni kuwa sasa hakuna haja ya kujikana nafsi mwenyewe na kutenda kwa bidii kazi ngumu isiyopendeza kama watangulizi wa ujumbe huu walivyofanya maishani; nyakati zile zimepita; na ya kwamba kwa kuwa kuna fedha nyingi zaidi kazini mwa Mungu, si lazima kwao kujiweka katika hali ngumu kama wengi walivyotakiwa kufanya mwanzo wa ujumbe huu.KN 72.4

  Lakini kama bidii zile zile na moyo wa kujinyima ule ule ungeonyeshwa katika hatua hii ya kazi kama mwanzoni, tungeona ukifanya makuu mara mia kuliko ifanyavyo hivi sasa. 206T417 - 419; KN 73.1

  Ungamo letu ni kuu. Sisi tulio Waadventista wenye kuishika Sabato twakiri amri zote za Mungu na kutazamia kuja kwa Mwokozi wetu. Ujumbe mzito sana wa onyo umewekwa amana kwa wachache waho waaminifu wa Mungu. Yatupasa kuonyesha kwa maneno na matendo yetu kuwa twafahamu maaaraka makubwa tuliyotwishwa. Nuru yetu ingeangaza hata wote wapate kuona jinsi tunavyomtukuza Baba katika maisha yetu ya kila siku na ya kwamba tumeungwa katika umoja na wale wa mbinguni na tu warithi warithio pamoja na Yesu Kristo, ili atakapoonekana katika uwezo na utukufu mwingi, tupate kufanana naye. 214T 16.KN 73.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents