Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 11 - Wakristo Kuwa Mfano wa Tabia ya Mungu

    MUNGU amekusudia kudhihirisha kwa njia ya watu wake kanuni za ufalme wake. Ili kwamba katika maisha na tabia wapate kuzidhihirisha kanuni hizi, anataka sana kuwatenga na kawaida, mazoea, na desturi za ulimwengu huu. Anataka kuwaleta karibu naye, kusudi apate kuwajulisha mapenzi yake.KN 90.1

    Kusudi ambalo Mungu anataka kulitimiza kwa njia ya watu wake leo ni lile alilotaka kulitimiza kwa njia ya Waisraeli alipowatoa kutoka Misri.KN 90.2

    Kwa kuutazama wema, rehema, haki, na upendo wa Mungu uliodhihirishwa kanisani, walimwengu hawana budi kuona mfano wa tabia yake Mungu. Na ndipo sheria ya Mungu ikionyeshwa kwa mfano namna hii maishani, hata walimwengu wataufahamu ukuu wa wale wampendao na kumwogopa na kumtumikia kuliko watu wo wote wengine duniani.KN 90.3

    Bwana humwangalia kila mmoja wa watu wake; na mipango yake kumhusu kila mmoja wa watu wake; na mipango yake kumhusu kila mmoja. Ni kusudi lake kuwa, wenye kuyaruata mafundisho yake matakatifu wawe wateule. Maneno haya yaliyoandikwa na Musa akiongozwa na Roho yanawahusu watu wa Mungu leo sawa na yalivyowanusu Waisraeli zamani: “Wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako; Bwana Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.” (Kumbukumbu la Torati 7:6). 16T 9, 12;KN 90.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents