Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uaminifu wa Mkristo

  Katika kila shughuli uwe mwaminifu kabisa. Ijapokuwa ushawishiwe namna gani, kamwe usidanganye wala kusema uongo hata katika jambo lililo dogo kabisa. Wakati fulani tamaa ya mwili yaweza kukushawishi kuacha njia nyofu ya uaminifu, lakini usibadili hata kidogo. Kama katika neno lo lote ukisema vile utakavyofanya, na baadaye uone kuwa umejihatarisha kwa kuwapendelea wengine, usibadili hata kidogo kanuni inayoyaongoza maisha yako. Timiza mapatano yako. 2CG 154;KN 95.2

  Biblia hukataza kwa uthabiti uongo wote, udanganyifu, na hila. Haki na kosa vimeelezwa dhahiri. Lakini nalionyeshwa kuwa watu wa Mungu wamejiweka upande wa adui; wameshikwa na ushawishi wake na huzifuata hila zake mpaka wepesi wao wa kuona umepunguzwa nguvu kabisa. Kosa dogo la kupotoka na kuuacha ukweli, kubadili kidogo na kuyaacha matakwa ya Mungu, hudhaniwa kuwa si dhambi kubwa ikiwa pana uhusiano na pato la faida au hasara ya fedha. Lakini dhambi ni dhambi, kama ikitendwa na mwenye fedha mamilioni au ikitendwa na maskini mwombaji barabarani. Wale wenye kujipatia mali kwa udanganyifu hujiletea hukumu rohoni mwao. Yote yapatikanayo kwa udanganyifu na hila yatakuwa tu laana kwa mpokeaji. 34T 311;KN 95.3

  Mtu mwenye kusema uongo au kutumia udanganyifu hujipotezea heshima. Huenda asijue kuwa Mungu humwona, na huifahamu kila shughuli, na ya kuwa malaika watakatifu huyapima makusudi yake na kuyasikiliza maneno yake, na ya kwamba ijara yake itakuwa kama kazi zake zilivyo; hata kama ingewezekana kulificha kosa lake lisichunguzwe na wanadamu wala Mungu, kwamba yeye mwenyewe alijua, humwaibisha moyoni mwake na kumwondolea cheo cha tabia yake. Tendo moja haliyakinishi tabia, ila huvunja boma, na jaribu lingine hupokewa upesi kwa urahisi zaidi, mpaka mwisho yafanywe mazoea ya kusema uongo na kudanganya kazini, mpaka mtu huyo asiweze tena kuaminika. 45T 396;KN 96.1

  Mungu anataka watu kazini mwake, chini ya bendera yake, kuwa waaminifu kabisa, wasio na upungufu wo wote au lawama katika tabia, ambao ndimi zao hazitasema masingizio yo yote. Ulimi hauna budi kuwa wa kweli, macho hayana budi kuwa ya kweli, matendo yote pia yawe ya namna ambayo Mungu aweza kuyasifu. Tunaishi machoni pa Mungu Mtakatifu, ambaye kwa kicho asema, “Nayajua matendo yako.” Jicho la Mungu daima hutuangalia. Hatuwezi kumficha Mungu tendo hata moja lisilo la halali. Ushuhuda wa Mungu kwa matendo yetu yote ni ukweli ambao wengi hawaufahamu. 5CG 152;KN 96.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents