Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Dibaji

  KADIRI Kanisa la Waadventista Wasabato lilivyozidi kukua katika iliyokuwa Afro-Mideast Division, washiriki wanaopenda kusoma walitamani sana kusoma vitabu vya Shuhuda kwa Kanisa (Testimonies for the Church), vitabu ambavyo kwa ujumla au kwa sehemu, vimeliongoza vizuri na kulineemesha Kanisa hili ulimwenguni mwote. Haiwezekani kuchapisha vitabu vyote tisa vya Shuhuda, na vingine vingi vya Roho ya Unabii. Lakini, pametolewa katika vitabu hivyo, mashauri mazuri yaliyochaguliwa kwa uangalifu sana baada ya kuonekana kuwa yenye manufaa makubwa na msaada wa kufaa kwa Kanisa.KN 4.1

  Uchaguzi wa maneno ambayo yamepangwa vizuri katika sura arobaini na mbili za vitabu hivi ni kazi ya ‘ Wadhamini wa Ellen G White, ambao ni juu yao kuyatunza maandishi ya Ellen White katika makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato, Maryland, Marekani.KN 4.2

  Imekuwa kazi ngumu kukusanya, kupanga, kutafsiri na kuvichapa vitabu hivi vyenye maneno ya maana yaliyochaguliwa kutoka katika vitabu vingi vya Ellen G White. Kwa sababu ya nafasi kuwa ndogo, mashauri yenye maana zaidi juu ya mambo makubwa tu ndiyo yaliyochapishwa. Hata hivyo hutoa mafundisho mengi mbalimbali. Wakati mwingine uchaguzi huu umefanywa katika mafungu makubwa kadha wa kadha tu ya maandishi ya mwanzoni yaliyoenezwa huko na huko Maelezo ya vitabu ambamo maneno haya yametwaliwa hupatikana kwa kifupi mwishoni mwa kila sura. Kwa kufuata Maelezo ya Ufupisho wa Majina ya Vitabu vilivyotumiwa humu waweza kupata kwa urahisi jina la kitabu kilichotajwa kwa kifupi. Hakuna maelezo yo yote yaliyotolewa kuonyesha mafungu ya maneno (ibara au sentenso) zilizoondolewa.KN 4.3

  Usichanganye huu utangulizi ulioandikwa na Wadhamini wa Vitabu vya Ellen G. White na maandishi yake mwenyewe ambayo huanzia katika sura ya kwanza.KN 5.1

  Inaridhisha na kupendeza kuona kuwa hivi vitabu viwili sasa vyaweza kupatikana kwa wale waliovingojea muda mrefu vitoke. Laiti mashauri na mafundisho yanayozijaza kurasa hizi yangeweza kuzidisha kina cha imani ya kila msomaji katika maneno ya kweli ya ujumbe wa Waadventista, kupanua maarifa na maisha ya Kikristo, na kuongeza kimo cha tumaini lake la ushindi wa siku ile ya mwisho Bwana wetu atakaporejea, ndilo lilikuwa ombi la Viongozi wa iliyokuwa Afro-Mideast Division na WADHAMINI WA VITABU VYA ELLEN G. WHITE.KN 5.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents