Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kusudi la Shetani ni Kutia Mashaka

    Mara nyingi Shuhuda hizi hupokewa kabisa, dhambi na uzoefu wa kujifurahisha kwa anasa ukavunjwa, na mara moja matengenezo mapya huanzwa yanayopatana na nuru ambayo ameitoa. Lakini mara zingine mazoea mabaya ya dhambi hupendelewa moyoni, Shuhuda hizi zikakataliwa, na uahuru mwingi kwa kweli ukatolewa kwa wengine kama sababu ya kukataa kuzipokea. Sababu ya kweli haitolewi. Kufanya hivi ni kukosa moyo wa uadilifu nia yenye nguvu na kutawaliwa na Roho wa Mungu, kuyakataa mazoea mabaya yenye madhara.KN 108.1

    Shetani anao uwezo wa kutia mashaka na kufanya hila za vipingamizi vya ushuhuda huu halisi ambao Mungu hutuma, na wengi huudhania kuwa ni sifa, alama ya akili walizo nazo, kuwa watu wasioamini na wenye kutoa hoja na kulaghai. Wale wanaotaka kuzionea mashaka watakuwa na nafasi tele. Mungu hakusudii kuondoa uwezekano wote wa kutokuamini. Hutoa ushuhuda, ambao hauna budi kuchunguzwa kwa uangalifu kwa moyo mnyenyekevu na mwelekevu, na wote wanapaswa kuamua wakitegemea ushuhuda huu. Mungu hutoa ushuhuda wa kutosha kwa ajili ya moyo mnyofu kuamini; lakini yeye ambaye hajali uzito wa ushuhuda kwa sababu tu yako mambo machache yasiyomwelea vizuri ataachwa katika hali baridi ya kushushwa moyo ya kutokuamini na kuonea mashaka, naye atavunjikiwa na imani.KN 108.2

    Ni kusudi la Shetani kuidhoofisha imani ya watu wa Mungu katika Shuhuda hizi. Shetani ajua jinsi ya kuranya mashambuiio yake. Atenda kazi mioyoni kuamsha husuda na kutokuridhika na wale walio wakuu wa kazi. Kisha ndipo huhoji juu ya karama walizo nazo; ndipo, huanza kutozithamini sana, na yale mafundisho yaliyotolewa kwa njia ya njozi huyadharau. Halafu hufuata moyo wa kuonea mashaka juu ya mambo makubwa ya imani yetu, nguzo za hali yetu, ndipo kwa kuyaonea shaka Maandiko Matakatifu, hushuka hata kupotea milele (bila tumaini la wokovu). Shuhuda ambazo zilipata kuaminiwa zamani, zinapoonewa mashaka na kuachwa, Shetani hujua kuwa waliodanganvwa hawatakoma kwa hilo tu; naye huzidisha jitihada zake mpaka kuanzisha uasi dhahiri, ambao hauponyeki na mwishowe huwa kwenye uharibifu. Kwa kutoa nafasi ya kuonea mashaka na kutokuamini juu ya kazi za Mungu, na kwa kupendelea moyoni kutokuamini na moyo wa husuda kali, wanajitayarisha kudanganyika kikamilifu. Nao huondoka wakiwa na uchungu juu ya wale wanaothubutu kusema makosa yao na kugombezwa kwa dhambi zao.KN 108.3

    Siyo tu kwamba wale wanaokataa Shuhuda hizi, au wenye kupendelea moyo wa kuzionea mashaka, wamo hatarini. Bali kuidharau nuru ni kuikataa pia.KN 108.4

    Kama ukipotewa na matumaini katika Shuhuda hizi utapotoka na kuiacha kweli ya Biblia. Naogopa kwamba wengi hupenda kuingia katika kuhoji na kuonea mashaka, na kwa wasiwasi wangu nilio nao kwa ajili ya roho zenu napenda kuwaonya Je, ni wangapi watakaolitii onyo hili? 6672 - 680;KN 108.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents