Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 15 - Roho Mtakatifu

  NI bahati njema ya kila Mkristo, licha ya kutazamia, hata kuhimiza kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kama wote wanaolikiri jina lake wangezaa matunda kwa utukufu wake, upesi kama nini ulimwengu wote ungepandwa mbegu za Injili. Kwa haraka mavuno ya mwisho yangekomaa, na Kristo angekuja kukusanya nafaka pevu.KN 113.1

  Ndugu na dada zangu, ombeni mpate Roho Mtakatifu. Mungu yu tayari kutimiza kila ahadi aliyoitoa. Mkiwa na Biblia zenu mikononi, semeni: “Nimefanya kama ulivyosema. Naonyesha ahadi yako, “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, mtafunguliwa,” Kristo asema: “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.” (Mathayo 7:7; Marko 11:24; Yohana 14:13).KN 113.2

  Kristo huwatuma wajumbe wake katika kila sehemu ya milki yake kuwajulisha mapenzi yake watumishi wake. Hutembea katikati ya makanisa yake. Ataka sana kuwatakasa, kuwaadilisha, na kuwaongoza vema wafuasi wake. Mvuto wa wale wanaomwamini utakuwa ulimwenguni harufu ya uzima iletayo uzima. Kristo anashika nyota katika mkono wake wa kuume, na ni kusudi lake kuacha nuru yake iangaze ulimwenguni kwa kupitia kwao. Hivyo anataka sana kuwatayarisha watu wake kwa kazi bora zaidi katika kanisa lake. Ametupa sisi kazi kuu kuifanya. Tuifanyeni kwa uaminifu. Hebu tuonyeshe katika maisha yetu kile neema ya Mungu iwezacho kuwafanyia wanadamu. 18T 22,23;KN 113.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents