Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Waadventisti Wasabato-Mfano kwa Walimwengu

  Sisi tunaodai kuwa viongozi, kuwa wachukuzi wa nuru ulimwenguni, kuwa askari waaminifu wa zamu kwa ajili ya Mungu, tulinde kila njia ambayo kwayo Shetani angeweza kuingilia na majaribu yake kuipotosha tamaa ya chakula. Kielelezo chetu na mvuto wetu hauna budi kuwa nguvu ya matengenezo haya mema. Yatupasa kuepukana na mazoea yo yote ambayo yataeneza dhamiri au kutia nguvu majaribu. Tusifungue mlango wo wote ambao utamwezesha Shetani kuingia moyoni mwa mwanadamu awaye yote ambaye ameumbwa kwa sura ya Mungu. 225T 360; KN 122.5

  Kwa habari za chai, kahawa, pombe, tumbaku, bangi, na vileo, njia ya salama ni kutokuvigusa. Haja ya watu wa kizazi hiki kutaka msaada wa uwezo wa nia thabiti iliyotiwa nguvu kwa neema ya Mungu, ili kuyastahimili majaribu ya Shetani na kupingana na uzoefu wa kujifurahisha kwa tamaa lliyopotoka ni kubwa mara mbili ya ilivyokuwa zamani za vizazi kadha wa kadha vilivyopita. Lakini kizazi hiki ni chenye uwezo kidogo wa kujitawala kuliko ule waliokuwa nao wale walioishi zamani zile. Wale wanaojifurahisha kwa tamaa ya vileo hivi wamerithisha tamaa zao za chakula zilizopotoka na ashiki kwa watoto wao, na uwezo mkuu zaidi wa tabia ya moyoni hutakikana kuzuia utovu wa kiasi, kutojizuia, au ulevi. Njia ya salama kabisa kuifuata ni kusimama imara upande wa kiasi (kutokunywa kileo cha namna yo yote) na kutojihatarisha.KN 123.1

  Kama akili za moyoni mwa Wakristo zingeamshwa kulifahamu jambo hili la kuwa na kiasi katika mambo yote, wangeweza, kwa kielelezo chao, kuanza mezani mwao, kuwasaidia wale ambao ni dhaifu katika kujitawala, ambao wako karibu kukosa kabisa uwezo wa kushindana na uchu. Kama tungeweza kufahamu kuwa mazoea tunayoyafanya katika maisha haya yatadhuru moyo wetu katika mambo yale yadumuyo milele, ya kwamba mwisho utakavyokuwa hutegemea juu ya mazoea ya kuwa na kiasi, tungefanya bidii tuwezavyo kuwa na kiasi katika kula na kunywa. Kwa kielelezo chetu na kujitahidi sisi wenyewe twaweza kuwa njia ya kuwaongoa watu wengi na kuwaepusha na hali mbaya ya utovu wa kiasi, kutojizuia, au ulevi, uhalifu wa sheria, na mauti. Akina dada waweza kufanya mengi katika kazi hii kubwa kwa ajili ya wokovu wa wengine kwa kutumia wakati wao ulio wa thamani katika kuzoeza uteuzi na tamaa ya chakula ya watoto wao, kufanya mazoea ya kuwa na kiasi katika mambo yote, na kuwavuta kujinyima na kuwa na ukarimu kwa faida ya wengine. 233T 488, 489.KN 123.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents