Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuyaunganisha Maisha ya Wawili Yawe Kitu Kimoja

  Ingawa shida, matatizo na vipingamizi vije, mume wala mke asiweke fikara moyoni ya kwamba ushirika wao wa ndoa ni kosa au ya kwamba inashusha moyo kwa kuwa hali yake si kama ilivyotazamiwa. Nuieni kwamba mtashirikiana na kusaidiana katika mambo vote kadiri mwezavyo. Daima mkifanyiana mambo yapendezayo kama mwanzoni. Kwa kila njia mtiane nguvu kwa kupambana na mambo magumu ya maisha. Jitahidini kukuza furaha yenu, ninyi kwa ninyi, Upendano halisi na uwepo mkichukuliana katika upendo. Ndipo ndoa, badala ya kuwa mwisho wa upendo, itakuwa kama mwanzo wa upendo. Urafiki wa kweli, na kupendana, ni kama kuonja mbele raha za mbinguni.KN 149.1

  Wote yawapasa kuongeza uvumilivu kwa kutumia uvumilivu. Kwa kule kuwa wapole na wavumilivu, upendo wa kweli waweza kudumishwa kuwa moto, usipoe moyoni, na tabia zitakazokuzwa zitakuwa za kumpendeza Mungu.KN 149.2

  Shetani siku zote yu tayari kujinufaisha wakati ugomvi au neno lo lote baya linapotokea, na kwa kuchochea tabia mbaya kwa mume au mke, atajaribu kuleta mafarakano baina ya wale ambao walikwisha kuunganisha mioyo yao kwa agano takatifu la ndoa mbele za Mungu. Katika ahadi za ndoa wameahidi kuwa kitu kimoja, mke akaahidi kwa kicho kumpenda na kumtii mumewe, mume akaahidi kumpenda na kumfurahisha mkewe. Kama sheria ya Mungu ikishikwa roho mbaya ya ugomvi haitakuwako kwa watu wa nyumbani, na hapatakuwako na utengano, wala mafarakano hayataruhusiwa.KN 149.3

  Huu ni wakati wa maana sana katika maisha ya wale ambao wamesimama mbele yenu kuunganisha mioyo na mapenzi yao, utu wao wema, upendo wao, na kazi yao, katika kazi ya kuziongoa roho za watu. Katika agano la ndoa pana hatua iliyo ya maana sana ambayo hutwaliwa-kuyachanganya ama kuyaunganisha maisha ya wawili yawe kitu kimoja. Mungu apenda kwamba mume na mke waungamanishwe pamoja kazini mwake, kuiendesha kwa utimilifu na utakatifu. Hao waweza kulifanya hili.KN 149.4

  Mbaraka wa Mungu nyumbani mtakamokuwa na umoja huu ni kama mwangaza wa jua la mbinguni, kwa sababu Bwana anenda kuwa mume na mke waungane pamoja katika vifungo vitakatiru vya umoja, kwa Yesu Kristo, wakiwa naye kuwatawala, na roho yake kuwongoza.KN 149.5

  Mungu ataka nyumbani pawe mahali pa furaha kabisa duniani, mfano wa makao ya mbinguni. Kuchukua madaraka haya ya ndoa nyumbani, kuiunganisha mioyo yao na Yesu Kristo, wakiutegemea mkono wake na ahadi yake, mume na mke wanaweza kushiriki umoja huo, furaha ambayo malaika wa Mungu huisifu. 1AH 101-107;KN 149.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents