Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Pakitokea Hitilafu

    Ni jambo gumu kusawazisha matata ya watu wa nyumbani, hata kama mume na mke wanatafuta kufanya mapatano ya haki juu ya wajibu mbalimbali uwapasao, ikiwa hawakumpa Mungu moyo. Mume na mke wanawezaje kuwa na nyoyo moalimbau juu ya maisha yao nyumbani kisha wapendane, na kuwa na umoja imara? Yawapasa kuwa na moyo mmoja kwa mambo yote yahusuyo unyumba wao, na mke, kama ni Mkristo, atakuwa na moyo wa kumpenda mumewe na kumhesabu kama mwenzake kabisa: maana mume apaswa kuwa kichwa cha nyumba.KN 150.1

    Roho yako ni mbaya. Unapoyatwaa madaraka, hupimi mambo vizuri na kufikiri kwanza matokeo ya baadaye yatakayoletwa na kule kuyashikilia maoni yako mwenyewe, huku ukijitegemea unazua tu maneno katika sala zako na maongezi, hali ukijua kuwa mkeo hana maoni hayo uliyo nayo wewe. Badala ya kuyaheshimu maoni ya mkeo na kuepuka kwa moyo mwema, kama mwungwana, mambo hayo ambayo wayajua kwamba mnahitilafiana, umetangulia kuyatafakari mabaya, na kuonyesha ukaidi ikisema maoni yako bila kumjali ye yote aliye nawe. Umeona kwamba wengine hawana haki kuyaona mambo haya tofauti, kinyume cha uonavyo wewe mwenyewe. Matunda haya hayazaliwi na mti wa Kikristo.KN 150.2

    Ndugu yangu, dada yangu, fungua mlango wa moyoni kumpokea Yesu. Mkaribishe ndani ya hekalu la rohoni. Saidianeni kuvishinda vipingamizi katika maisha ya nyumba ya wote. Mtakuwa na vita vilivyo vikali kumshinda adui wenu Shetani, na kama mkimtazamia Mungu kuwasaidia katika vita hivi, hamna budi kuwa na umoja mkikata shauri kushinda, kufunga vinywa vyenu msiseme maneno yo yote mabaya, hata kama lkiwabidi kupiga magoti chini na kupaza sauti, “Bwana, mkemee adui wa roho yangu.”KN 150.3

    Ikiwa mapenzi ya Mungu yatatimizwa mume na mke wataheshimiana na kuwa na upendano na matumaini. Lo lote ambalo lingeharibu imani na umoja wa watu wa nyumbani Iinapasa kukomeshwa kabisa, na fadhili na upendo vingependelewa. Mwenye kuonyesha moyo wa huruma, uvumilivu, na upendo ataona kuwa moyo huo huo unaonyeshwa kwake. Mahali Roho wa Mungu anapotawala, hapatakuwako na mazungumzo yasiyofaa unyumbani. Kama Kristo kwa kweli anawekwa moyoni, tumaini la utukufu, kutakuwako na umoja na upendo nyumbani. Kristo akaaye moyoni mwa mke atapatana na Kristo akaaye moyoni mwa mume. Watafanya bidii pamoja ili wayapate makao ambayo Kristo alikwenda kuwaandalia wale wampendao.KN 150.4

    Wale wanaoihesabu ndoa kama mojawapo ya maagizo matakatifu ya Mungu, yenye kulindwa na mafundisho yake matakatifu, watatawaiiwa na maonyo ya akili ya moyoni.KN 151.1

    Katika maisha ya ndoa wanaume na wanawake wakati mwingine hufanya kama watoto wasiopata malezi mazuri, wakaidi. Mume ashika lake, na mke anashika lake, wala hakuna atakayekushindwa. Hali ya mambo ya jinsi hii huleta tu huzuni kubwa. Wote mume na mke, yawapasa kukubali kwa hiari kushindwa kwa njia yake. Hawawezi kuwa na raha wakiwa wanakazania kila mmoja kile apendacho mwenyewe. 2AH 118-121;KN 151.2

    Pasipo kuchukuliana na upendano hakuna uwezo duniani uwezao kukushikilia katika umoia na mumeo ndani ya umoja wa Kristo. Urafiki wenu katika ndoa wapasa uwe imara na wenye upendo, mtakatifu na bora, wenye kuwatia uwezo wa kiroho maishani mwenu, ili mpate kuridhisnana ninyi kwa ninyi kama neno la Mungu litakavyo. Mtakapoifikia hali ambayo Mungu ataka mwe nayo, mtapaonja mbinguni mkiwa mngali napa chini na Mungu mtamwona maishani mwenu.KN 151.3

    Kumbukeni, ndugu na dada, kwamba Mungu ni upendo na ya kuwa kwa neema yake mwaweza kufaulu kupendezana, kama mlivyokwisha kuahidi katika ndoa yenu. 3AH 112;KN 151.4

    Kwa neema ya Kristo mwaweza kupata ushindi juu ya nafsi na moyo wa choyo. Mkienenda kama alivyoenenda, na kuonyesha moyo wa kujinvima kwa kila hatua, daima mkiwahurumia zaidi wale walio shidani, wenye kuhitaji msaada, mtapata ushindi kila mara. Siku kwa siku mtafahamu zaidi kuushinda moyo wa kujifikiri nafsi mwenyewe bila kujali wengine na namna ya kuyaimarisha mambo manyonge ya tabia zenu. Bwana Yesu atakuwa nuru yenu, nguvu, yenu kipeo cha kufurahi kwenu, kwa sababu mkekubali nia yake iwe yenye kushinda na kuwa badala ya nia yenu. 477 49.KN 151.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents