Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ndoa ni Halali na Takatifu

  Hakuna dhambi katika kula wala kunywa, ama katika kuoa na kuolewa. Ilikuwa halali kuoana siku za Nunu, na ni halali kuoana siku hizi, ikiwa kile kilicho halali kinatendwa vizuri wala hakizidi hata kuwa dhambi. Lakini katika siku za Nuhu watu walioana pasipo kutaka shauri kwa Mungu au kutafuta maongozi yake.KN 152.2

  Kwamba uhusiano wote wa maisha ni wa kitambo tu yapasa uwe na mvuto uliogeuzwa kidogo juu ya mambo yo yote tutenaayo na yale tusemayo. Katika siku za Nuhu upendo usiokuwa na kiasi wa kile ambacho chenyewe kilikuwa halili ikiwa kingetumiwa vizuri, ndio uliofanya kuoa au kuolewa kuwa dhambi mbele za Mungu. Wako wengi wanaopoteza nafsi zao siku hizi kwa kufikiri sana juu ya ndoa na kushughulika na mambo yake hata kuwasahaulisha mambo mengine.KN 152.3

  Ndoa ni takatifu, lakini katika kizazi hiki kibaya inachukua ubaya wa udanganyifu wote ndani yake. Imetumiwa vibaya nayo imekuwa uhalifu ambao huifanya iwe mojawapo ya dalili za siku za mwisho, naam, kama kuoa na kuolewa, kulivyokuwa siku zile kabla ya Gharika. Hali takatifu na madai ya ndoa yakifahamika vizuri, nata sasa itaweza kuwa jambo la kumpendeza Mungu; na matokeo yake yatakuwa furaha kwa pande zote mbili, na Mungu atatukuzwa.KN 152.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents