Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kazi ya Hukumu

  Katika agano jipya, dhambi za wale wanaotubu huwa zinawekwa juu ya Kristo kwa njia ya imani na kuhamishiwa patakatifu pa mbinguni. Na kama vile kutakaswa kwa patakatifu pa duniani kulivyofanyika kwa kuziondoa dhambi ambazo zilikuwa zimepachafua, vivyo hivyo utakaso halisi wa patakatifu pa mbinguni unafanyika kwa kuziondoa au kuzifuta dhambi zilizoandikwa. Lakini kabla ya jambo hilo kufanyika ni lazima kuwa na ukaguzi wa vitabu vya kumbukumbu kuona ni nani anastahili kunufaika na upatanisho Wakristo kwa njia ya toba na imani kwake. Kwa hiyo kutakaswa kwa patakatifu kunaambatana na kazi ya upelelezi—kazi ya hukumu—kabla ya kuja kwa Kristo, kwani atakapokuja, ujira wake utakuwa pamoja naye kumlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. Ufunuo 22:12.TK 264.1

  Kwa hiyo wale walioifuata nuru ya neno la unabii waliona kwamba, badala ya kuja duniani mwishoni mwa zile siku 2300, mwaka 1844, Kristo aliingia patakatifu sana pa patakatifu pa mbinguni kufanya kazi ya mwisho ya upatanisho kama maandalizi ya kuja kwake.TK 264.2

  Kristo anapoondoa dhambi za watu wake kwa damu yake kutoka patakatifu pa mbinguni mwishoni mwa huduma yake, ataziweka juu ya Shetani, ambaye inampasa kupata ile adhabu ya mwisho. Mbuzi wa azazeli alikuwa anapelekwa katika nchi isiyokaliwa na watu, na hakurudi tena katika kusanyiko la Israeli. Hivyo ndivyo Shetani akakavyoondolewa katika uwepo wa Mungu na watu wake, na ataondoshwa kabisa wakati wa maangamizi ya mwisho ya dhambi na wenye dhambi na hatakuwapo tena.TK 264.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents