Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sabato ya Kweli Imekuwa IkishikwaDaima

  Tangu siku ile hadi sasa Sabato imekuwa ikishikwa. Ingawa yule “mtu wa kuasi” alifaulu kuikanyaga siku takatifu ya Mungu chini ya miguu yake, lakini katika sehemu za siri walikuwa wamejificha watu waaminifu waliokuwa wanaiheshimu. Tangu nyakati za matengenezo, baadhi katika kila kizazi wamedumisha utunzaji wake.TK 282.4

  Ukweli huu kuhusiana na “lnjili ya milele” utalitofautisha kanisa la Kristo wakati wa atakapotokea. “Hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Ufunuo 14:12.TK 282.5

  Wale walioipokea nuru juu ya Patakatifu na sheria ya Mungu walijazwa na furaha walipoona upatanifu katika ukweli. Walitamani ile nuru wapewe Wakristo wote. Lakini ukweli uliokuwa unahitilafiana na ulimwengu haukukubaliwa na wengi waliodai kumfuata Kristo.TK 282.6

  Madai ya Sabato yalipokuwa yanatolewa, wengi walisema: “Wakati wote tumekuwa tunaishika Jumapili, baba zetu walikuwa wanaishika, na watu wengi wazuri kwa furaha walikufa wakiwa wanaishika. Kushika Sabato mpya kutatufanya tutengwe na ulimwengu. Ni kitu gani ambacho kikundi kidogo cha watu wanaoshika Sabato ya siku ya saba kitafanikisha dhidi ya ulimwengu wote unaotunza Jumapili? Kwa kutumia hoja zinazolingana na hii, ndivyo Wayahudi walivyohalalisha tendo la kumkataa Yesu. Vivyo hivyo wakati wa Luther, Wakatoliki walikuwa wanatoa sababu kuwa Wakristo wa kweli walikufa wakiwa katika imani ya Kikatoliki; kwa hiyo imani hiyo inatosha. Hoja kama hizi zilikuwa kikwazo kwa maendeleo ya imani.TK 282.7

  Wengi walitoa hoja kwamba kushika Jumapili ilikuwa ni desturi ya kanisa kwa kame nyingi. Hoja kinyume na hiyo ilionesha kuwa Sabato na ushikaji wake ilikuwa ya kale zaidi, ikiwa na umri sawa na dunia na ilianzishwa na Mzee wa Siku.TK 283.1

  Wakiwa hawana ushuhuda wa Biblia, wengi walitoa hoja kuwa, “Kwa nini watu wetu wakuu hawalielewi suala hili la Sabato? Ni wachache tu wanaoamini kama ninyi. Haiwezekani ninyi mwe sahihi na wasomi wote wawe wamekosea.”TK 283.2

  Ili kuzipinga hoja hizo ilikuwa ni lazima kutoa nukuu za Maandiko na kuyaelezea matendo ya Mungu kwa watu wake katika zama zote. Sababu inayomfanya Mungu mara nyingi asiwachague wasomi na kuwafanya viongozi wa matengenezo ni kuwa wanazitumainia kanuni zao za imani na mifumo ya kiteolojia, na kuona kuwa hawana hitaji la kufundishwa na Mungu. Watu wenye elimu kidogo ya shuleni wakati mwingine huitwa ili wautangaze ukweli, siyo kwa sababu hawana elimu, lakini kwa sababu wanajitambua kuwa hawajitoshelezi na wako tayari kufundishwa na Bwana. Unyenyekevu na utii wao unawafanya wafae.TK 283.3

  Historia ya wana wa Israeli ni kielelezo kizuri cha uzoefu uliopita wa jamii ya Waadventista. Mungu aliwaongoza watu wake kwenye vuguvugu la Ujio, kama alivyowaongoza wana wa Israeli kutoka Misri. Endapo watu wote walioshughulika kwa umoja katika kazi ya mwaka 1844 wangeupokea ujumbe wa malaika yule wa tatu na kuutangaza kwa nguvu ya Roho Mtakatifu; miaka mingi iliyopita dunia ingekuwa imekwisha kuonywa na Kristo angekuwa amekuja kuwakomboa watu wake.TK 283.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents