Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 39 - Wakati Wa Taabu

    U Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Danieli 12:1.TK 370.1

    Wakati ujumbe wa malaika wa tatu utakapofungwa, watu wa Mungu watakuwa wamekamilisha kazi yao. Watakuwa wamepokea “mvua ya masika” na wamejiandaa kwa ajili ya saa ya majaribu iliyo mbele yao. Jaribu la mwisho litakuwa limeletwa duniani na wote ambao wamethibitika kuwa waaminifu kwa sheria za mbingu watakuwa wamepokea “muhuri wa Mungu aliye hai.” Kisha Yesu atakoma kufanya kazi yake ya upatanisho katika patakatifu pa mbinguni na kwa sauti kubwa atasema “imekwisha.” “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.”- Ufunuo22:ll. Kristo atakuwa amefanya upatanisho kwa ajili ya watu wake na kufuta dhambi zao. “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote,” (Danieli 7:27) umekaribia kutolewa kwa warithi wa wokovu na Yesu atatawala kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.TK 370.2

    Atakapoondoka katika patakatifu, giza litawafunika wakazi wa dunia. Wenye haki itawapasa waishi mbele za Mungu Mtakatifu pasipo mpatanishi. Kiizuizi kwa watu waovu sasa kitakuwa kimeondolewa na Shetani atakuwa na udhibiti kamili kwa wale ambao hawakutubu. Hatimaye Roho wa Mungu atakuwa ameondolewa. Shetani atawaingiza watu wa dunia kwenye taabu kuu ya mwisho. Malaika wa Mungu wataacha kuzuia pepo kali za tamaa za wanadamu. Dunia yote itaingizwa katika maangamizi mabaya kuliko yale yalioipata Yerusalemu ya zamani. Zipo nguvu ambao ziko tayari hivi sasa, zinazosubiri ruhusa ya Mungu, kueneza uharibifu kila mahali.TK 370.3

    Wale wanaoiheshimu sheria ya Mungu watachukuliwa kuwa ndio wanaosababisha migogoro ya kutisha na umwagaji damu ulioenea duniani pamoja na huzuni.Uwezo ulio kwenye onyo la mwisho utawakasirisha waovu na Shetani ataweka roho ya chuki na mateso dhidi ya wale wote watakaokuwa wameupokea ujumbe.TK 370.4

    Uwepo wa Mungu ulipokuwa ametolewa kwa taifa la Wayahudi, makuhani na watu bado walijihesabu kwamba wao ni wateule wa Mungu. Huduma za hekaluni ziliendelea; kila siku baraka ya mbingu ilitolewa kwa watu ambao walikuwa na hatia ya damu ya Mwana wa Mungu. Kwa hiyo uamuzi usioweza kubadilika wa patakatifu utakapokuwa umetangazwa na hatima ya dunia itakapokuwa imekwisha kuamriwa milele, wakazi wa dunia hawatajua. Mitindo ya dini itaendelezwa na watu ambao Roho wa Mungu atakuwa ameondolewa kutoka kwao; ari ya Shetani ya kutaka mafanikio ya mbinu za uharibifu itafanana na ari kwa ajili ya Mungu.TK 371.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents