Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Malaika wa Mauti.

    Sasa malaika wa mauti atatokea, aliyewakilishwa kwenye njozi ya Ezekieli kama watu wenye silaha za kuua, ambao kwao amri amri itatolewa: “Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu.” “Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Ezekieli 9:6.TK 392.3

    Walinzi wasio wakweli ndiyo watakaoanza kuangungamia. “Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani: ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.” “Mashaka makubwa yatokayo kwa Bwana yatakuwa kati yao; na kila mmoja wao atakamata mkono wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani yake.” Isaya 26:21; Zekaria 14:13.TK 392.4

    Katika hali ya mabishano makali ya hisia zao na kwa kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu isiyochanganywa makuhani, watawala na watu waovu watangamia “Na waliouawa na Bwana siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili.” Yeremia 25:33.TK 392.5

    Wakati wa kuja kwa Kristo waovu wataangamizwa kwa mng’ao wa utukufu wake. Kristo atawapeleka watu wake kwenye mji wa Mungu, na dunia itakuwa tupu bila wakazi wake. “Tazama, Bwana ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake....Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo...kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia: ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea.” Isaya 24:1,3,5,6.TK 392.6

    Dunia itaonekana kama jangwa lililo ukiwa. Miji itaharibiwa kwa tetemeko la ardhi, miti itang’olewa, miamba iliyopasuka kutoka kwenye dunia itasambaa juu ya uso wake. Mabonde makubwa yatakuwa alama za mahali ilipokuwa milima iliyong’oka kutoka kwenye misingi yao.TK 393.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents