Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nguvu ya Neno

    Mapema sana ilisikika katika mji wote wa Wittenberg kuwa Luther alikuwa amerudi na angehubiri. Kanisa lilijaa watu. Kwa busara ya hali ya juu na upole alifundisha na kukemea: “Misa ni jambo baya; Mungu hapendi jambo hilo; inabidi lipigwe marufuku...Lakini mtu yeyote asiachishwe jambo hilo kwa nguvu...Neno la Mungu ni lazima lifanye kazi, sio sisi...Tuna haki ya kusema: hatuna haki ya kutenda. Kazi yetu ni kuhubiri; mambo mengine ni ya Mungu. Kama ningewashurutisha watu ningepata faida gani? Mungu ndiye agusaye moyo, na moyo unapokuwa umekamatwa; kila kitu huwa kimepatikana...TK 123.1

    “Nitahubiri, nitazungumza, na nitaandika, lakini sitamlazimisha mtu yeyote, kwa sababu imani ni tendo la hiari...ninasimama kinyume na Papa, misamaha ya dhambi ya kununua, na utawala wa Papa na wafuasi wao, lakini pasipo kutumia nguvu wala ghasia. Ninaliweka mbele Neno la Mungu; Nilikuwa nahubiri na kuandika hayo yote ndiyo niliyokuwa nayafanya. Na bado nilipokuwa usingizini, neno nililokuwa nimelihubiri liliuangusha utawala wa Papa, hata hivyo si mwana mfalme wala mfalme aliyepata madhara makubwa. Mimi sikufanya chochote, Neno pekee ndilo lililofanya mambo yote.” 111Ibid. Neno la Mungu lilivunja laana ya msisimko wa itikadi kali. Injili iliwarejesha katika njia ya ukweli watu waliokuwa wamepotoshwa.TK 123.2

    Miaka kadhaa baadaye, itikadi kali ziliibuka zikiwa na athari za kutisha zaidi. Luther alisema, “Kwa watu hao Maandiko Matakatifu yalikuwa kama barua iliyokufa na wote walianza kupiga kelele, “roho! roho!” Lakini ninakuhakikishia sitakwenda kule roho wao anakowapeleka.” 112Ibid. bk. 10, ch. 8.TK 123.3

    Thomas Munzer, ni mtu aliyekuwa na bidii sana kati ya watu waliokuwa na itikadi kali. Alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa, lakini alikuwa hajajifunza dini ya kweli. “Alikuwa na shauku ya kufanya matengenezo ulimwenguni, lakini kama walivyo watu wengi wenye ari hiyo, alisahau kuwa inalazimika matengenezo yaanze na yeye mwenyewe.” 113Ibid. bk. 9, ch. 8. Hakuwa tayari kushika nafasi ya pili baada ya kwa Luther. Alidai mwenyewe kuwa alikuwa ameagizwa na Mungu kuanzisha matengenezo ya kweli: “Mwenye roho huyu ana imani ya kweli, hata kama kamwe hatayaona Maandiko katika maisha yake.” 114Ibid. bk. 10, ch. 10. Walimu wasiofaa walijitoa wenyewe kuongozwa na maono, wakilichukua kila wazo na msukumo kama sauti ya Mungu. Wengine walidiriki hata kuchoma Biblia zao. Maelfu waliyapokea mafundisho ya Munzer. Mapema alitangaza ya kuwa kuwatii wakuu ilikuwa ni kujaribu kumtumikia Mungu na Shetani.TK 123.4

    Mafundisho haya ya kimapinduzi ya Munzer yaliwaongoza watu kuasi kila mamlaka. Mandhari za kutisha na machafuko zilifuata, na maeneo mbalimbali nchini Ujerumani yaligubikwa na mauaji na umwagikaji wa damu.TK 124.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents