Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hekalu Zuri Lakabiliwa na Uharibifu

  Siku mbili kabla ya Pasaka, alikwenda tena pamoja na wanafunzi wake katika Mlima wa Mizeituni uliokuwa mkabala na mji. Kwa mara nyingine alilitazama hekalu katika utukufu wake wa ajabu. Lilikuwa kilele cha uzuri. Sulemani, aliyekuwa na hekima kuliko wafalme wote wa Israeli, alikuwa amejenga hekalu la kwanza, jengo lililokuwa la fahari kuliko yote ambayo ulimwengu ulikuwa umepata kuyaona. Baada ya Nebukadneza kuliangamiza, lilijengwa upya takriban miaka mia tano kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.TK 22.3

  Lakini hekalu la pili halikulifikia la kwanza kwa uzuri. Halikuwa na wingu la utukufu, wala moto ulikuwa haushuki toka mbinguni kuja kwenye madhabahu yake. Sanduku la Agano, kiti cha rehema, na mbao za ushuhuda hazikuwepo. Hakukuwa na sauti toka mbinguni iliyokuwa inamjulisha kuhani mapenzi ya Mungu. Hekalu la pili halikupewa heshima ya kuwa na wingu la utukufu wa Mungu, bali lilipewa heshima ya uwepo wake yeye aliye Mungu mwenyewe aliyedhihirishwa katika mwili. “Shauku ya Mataifa yote” alikuwa amekuja kwenye hekalu lake wakati yule Mtu wa Nazareti alipokuwa akifundisha na kuponya katika zile nyua takatifu. Lakini Israeli waliikataa karama ya mbinguni iliyokuwa imetolcwa. Kwa kutoka yule Mwalimu mnyenyekevu katika lango la dhahabu la hekalu, utukufu uliondoka moja kwa moja katika lile hekalu. Maneno ya Mwokozi yalikuwa yametimia: “nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” Mt. 23:38.TK 22.4

  Wanafunzi walikuwa wamejawa na mshangao kutokana na utabiri Wakristo kuhusu kubomolewa kwa hekalu, na walitamani kuelewa maana ya maneno yake. Herode mkuu alikuwa ametumia kwa wingi hazina za Kirumi na Kiyahudi kwa ajili ya hekalu hilo. Sehemu ya hekalu hilo ilikuwa imetengenezwa kwa matofali makubwa ya marumaru nyeupe toka Rumi. Hii ndiyo ilipelekea wanafunzi kumwambia Mwalimu wao: “tazama, yalivyo mawe na majengo haya!” Mk. 13:1.TK 23.1

  Yesu akatoa jibu zito na la kushtusha: “Amin, nawaambieni, halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.” Mt. 24:2. Bwana alikuwa amcwaambia wanafunzi kwamba atakuja mara ya pili. Kwa sababu hiyo, alipotaja hukumu juu ya Yerusalemu, mawazo yao yalirudi katika suala la kuja kwake, na hivyo wakauliza: “Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?” Mt.24:3.TK 23.2

  Kristo alitoa muhtasari wa matukio muhimu yatakayotokca kabla ya mwisho wa wakati. Unabii alioutoa ulikuwa na maana mbili. Wakati ulikuwa unaonesha maangamizi ya Yerusalemu yatakavyotokea, pia ulikuwa unaonesha matatizo ya siku ile kuu ya mwisho.TK 23.3

  Hukumu zingewajia Israeli kwa sababu ya kumkataa na kumsulubisha Masihi. “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani.” Mt. 24:15, 16. Soma pia Lk. 21:20, 21. Bendera za Kirumi zinazoambatana na ibada ya sanamu zingesimamishwa katika nchi takatifu nje ya kuta za mji, ingewapasa wafuasi Wakristo kutafuta usalama kwa kukimbia. Wale waliokuwa wanataka kupona ingewapasa kufanya haraka. Kwa sababu ya dhambi za Yerusalemu, ghadhabu ilikuwa imetamkwa dhidi yake. Kutokuamini kwake kulikokuwa sugu kulifanya maangamizi yawe jambo la uhakika. Soma Mik. 3:9-12. Wakazi wa Yerusalemu walimtuhumu Kristo kwamba alikuwa chanzo cha matatizo yote yaliyokuwa yanawapata kwa sababu ya dhambi zao. Japo walikuwa wanajua kuwa hakuwa na dhambi, waliona kuwa kifo chake kilikuwa cha lazima kwa ajili ya usalama wao kama taifa. Walikubaliana na uamuzi wa kuhani wao mkuu kuwa ingekuwa bora mtu mmoja kufa kuliko taifa zima kuangamia. Soma Yn. 11:47-53.TK 23.4

  Wakati walikuwa wamemwua Mwokozi wao kwa sababu alikuwa amekemea dhambi zao, walikuwa wanajiona kuwa ni watu wa Mungu na kutarajia Bwana awakomboe kutoka kwa adui zao!TK 24.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents