Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hekalu la Hapa Duniani

    Hema ya kukutania ilitengenezwa kulingana na agizo la Mungu. Bwana aliwainua mafundi stadi na kuwawezesha kwa vipaji visivyo vya kawaida ili wapate kutenda kazi iliyokuwa inahitaji uangalifu mkubwa sana. Si Musa wala wale mafundi waliachwa kupanga umbo na ustadi wa jengo lile. Mungu mwenyewe alibuni ramani na kumpa Musa, pamoja na maelekezo mahususi kuhusu ukubwa na umbile na vifaa vitakavyotumika, aliweka bayana kila samani ambayo ilikuwa iwe ndani yake. Alimwonesha Musa taswira ndogo ya patakatifu pa mbinguni na kumwagiza kufanya kila kitu sawa na mfano aliooneshwa juu ya mlima. Musa aliandika maelekezo yote katika kitabu na kuyasoma kwa watu wale mashuhuri.PLK 52.1

    Bwana alitaka watu walete sadaka za hiari kwa ajili ya kumtengenezea patakatifu, ili apate kuishi miongoni mwao. “Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa Bwana, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja, waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa Bwana.”PLK 52.2

    Matayarisho makubwa na aghali yalikuwa ni lazima yafanyike. Vifaa adimu na vya thamani kubwa vilikuwa ni lazima vikusanywe. Lakini Bwana alikubali tu sadaka za hiari. Mahitaji ya kwanza katika kumtayarishia Mungu mahali yalikuwa ni kujitoa kwa ajili ya kazi ile na kujinyima kutoka moyoni. Na wakati jengo la patakatifu lilipokuwa likiendelea kujengwa na watu walikuwa wanaendelea kuleta sadaka zao kwa Musa, na yeye alikuwa akizifikisha kwa mafundi stadi, watu wote wenye hekima waliokuwa wanatumika katika kazi ile walikagua matoleo yale na kuamua kuwa watu walikuwa wameleta ya kutosheleza, na hata zaidi ya walichoweza kutumia. Naye Musa akatangaza katika kambi zima, akisema, ” ‘Wasifanye kazi tena, mtu mume wala mwanamke, kwa ajili ya matoleo kwa mahali patakatifu.’ Basi watu wakazuiwa wasilete tena.”PLK 52.3

    Imeandikwa katika Kumbukumbu kwa Ajili ya Vizazi Vijavyo-Malalamiko ya kurudiarudia ya Waisraeli na adhabu za ghadhabu ya Mungu kwa sababu ya dhambi zao zimeandikwa katika kumbukumbu za historia takatifu ili kunufaisha watu wa Mungu ambao baadaye wangeishi duniani. Hata zaidi ya hapo, ilikuwa yatoe onyo kwa wale ambao wangeishi karibu na mwisho wa wakati. Kwa nyongeza, matendo yao ya ibada na nguvu zao na ukarimu katika kuleta sadaka za hiari kwa Musa yameandikwa katika kumbukumbu kwa ajili ya manufaa ya watu wa Mungu. Kutayarisha kwao vifaa kwa uchangamfu kwa ajili ya patakatifu ni mfano kwa wote wanaopenda ibada kwa Mungu. Wanapotayarisha jengo kwa ajili yake yeye ili akutane nao, wale wanaothamini baraka za utakatifu wa kuwepo kwa Mungu wanapaswa kuonesha moyo wa kupenda zaidi na bidii katika kazi hii takatifu kulingana na jinsi wanavyothamini baraka za mbingu kuliko starehe zao za kidunia. Wanapaswa kutambua kuwa wanatayarisha nyumba kwa ajili ya Mungu.PLK 53.1

    Ni muhimu kuwa nyumba ambayo inaandaliwa hasa kwa ajili ya Mungu kukutana na watu wake ipangwe kwa uangalifu-iwe ya kuridhisha, safi, na ya kufaa, kwa sababu wataiweka wakfu kwa Mungu na kuitoa kwake, huku wakimwomba apate kuishi katika nyumba ile na kuifanya kuwa takatifu kwa sababu ya kuwepo kwa utakatifu wake. Wanapaswa kutoa kiasi cha kutosha kwa hiari kwa Bwana ili kukamilisha kazi ile kwa ukarimu na kisha mafundistadi waweze kusema, “Msilete sadaka zaidi.”PLK 53.2

    Kulingana na Mfano-Baada ya kumaliza kujenga hema ya kukutania, Musa aliikagua kazi yote, akiilinganisha na mfano na maelekezo aliyopokea kutoka kwa Mungu. Aliona kuwa kila sehemu ya jengo lile ilipatana na mfano ule, na aliwabariki watu wale.PLK 54.1

    Mungu alitoa mfano wa sanduku la agano kwa Musa, pamoja na maelekezo maalumu ya jinsi ya kulitengeneza. Sanduku la agano lilitengenezwa ili lipate kutunza mbao za mawe ambazo juu yake Mungu alichora Amri Kumi kwa kidole chake mwenyewe. Lilitengenezwa katika umbo la sanduku la kuhifadhia nguo na kufunikwa juu kwa dhahabu ndani na nje. Lilipambwa kwa taji za dhahabu kuzunguka sehemu ya juu. Kifuniko cha sanduku hili takatifu kiliitwa kiti cha rehema, na kilitengenezwa kwa dhahabu tupu. Kila mwisho wa sanduku la agano kulikuwapo na kerubi wa dhahabu tupu iliyo safi. Nyuso zao ziligeukiana na zilikuwa zimeelekezwa chini kwa kicho katika kiti cha rehema. Hii iliwakilisha malaika wote wa mbinguni wakiangalia kwa kupenda na kicho katika sheria ya Mungu iliyowekwa katika sanduku katika patakatifu pa mbinguni. Makerubi hawa walikuwa na mbawa. Bawa moja la kila malaika lilinyoshwa juu, wakati ambapo bawa lingine la kila malaika liliufunika mwili wake. Sanduku la agano la patakatifu pa duniani lilitengenezwa katika mfano wa sanduku la kweli la agano lililoko mbinguni. Pale, pembeni mwa sanduku la agano lililoko mbinguni, wanasimama malaika walio hai, katika kila upande wa sanduku la agano, na wakiwa na bawa moja likifunika kiti cha rehema, na kunyoshwa juu yake, wakati ambapo mabawa yale mengine yamekunjwa juu ya maumbo yao katika onesho la kicho na unyenyekevu.PLK 54.2

    Musa alitakiwa kuweka mbao zile za mawe ndani ya sanduku la agano la duniani. Hizi ziliitwa mbao za ushuhuda, na sanduku liliitwa sanduku la ushuhuda, kwa sababu zilibeba shuhuda za Mungu katika jinsi ya Amri Kumi.PLK 55.1

    Vyumba Vhvil i-Hema ya kukutania ilikuwa na vyumba viwili, vilivyotenganishwa na pazia. Samani zote za hema ya kukutania zilikuwa zimetengenezwa kwa dhahabu tupu au kufunikwa kwa dhahabu. Mapazia ya hema ya kukutania yalikuwa ya rangi tofauti tofauti, zilizopangwa kwa uzuri mno, na katika mapazia haya makerubi walifumwa, kwa kutumia nyuzi za dhahabu na fedha. Hawa walikuwa wawakilishe mamilioni ya malaika, ambao wanahusika na kazi ya patakatifu pa mbinguni na wale malaika wanaohudumu wakiwatumikia watu wa Mungu duniani.PLK 55.2

    Ndani ya pazia la pili, au shela, liliwekwa sanduku la ushuhuda, na pazia zuri la gharama liliwekwa mbele ya sanduku takatifu. Pazia hili halikufika hadi juu mwisho wa jengo. Utukufu wa Mungu, ambao ulikuwa juu ya kiti cha rehema, ungeweza kuonekana kutokea katika kila chumba, lakini kwa kiasi kidogo zaidi kutoka kwenye chumba cha kwanza.PLK 55.3

    Moja kwa moja mbele ya sanduku la agano, lakini likiwa limetenganishwa na pazia, palikuwapo madhabahu ya dhahabu ya uvumba, na yalihifadhiwa kwa utukufii kwa kuwekewa uvumba mtakatifu, uliojaza patakatifu kwa wingu lenye harufu nzuri mchana na usiku. Harufu yake nzuri ilienea kwa maili kadhaa kuzunguka hema ya kukutania. Wakati kuhani alipofukiza uvumba mbele za Bwana, alitazama katika kiti cha rehema. Ingawa alikuwa hawezi kukiona, alifahamu kuwa kimo mle, na pale uvumba ulipoinuka kama wingu, utukufu wa Bwana ulishuka juu ya kiti cha rehema na kupajaza patakatifu pa patakatifu na ulionekana kutoka katika chumba cha patakatifu. Mara kadhaa utukufu ule ulijaza vyumba vyote viwili hata kuhani hakuweza kufanya kazi yake na alilazimika kusimama katika mlango wa hema ya kukutania.PLK 55.4

    Kuhani katika patakatifu, akielekeza maombi yake kwa imani kuelekea katika kiti cha rehema ambacho alikuwa hawezi kukiona, huwakilisha watu wa Mungu wakielekeza maombi yao kwa Kristo aliye katika kiti cha rehema katika patakatifu pa mbinguni. Hawawezi kumwona Mpatanishi wao kwa jicho la kawaida, bali kwa jicho la imani wanamwona Kristo akiwa amesimama mbele ya kiti cha rehema. Wanaelekeza maombi yao kwake na kwa uhakika wanadai manufaa ya upatanisho wake.PLK 56.1

    Vyumba hivi vitakatifu havikuwa na madirisha ya kuingiza nuru. Kinara cha taa, kilitengenezwa kwa dhahabu tupu safi mno na kiliachwa kikiwaka usiku na mchana, kikitoa nuru kwa vyumba vyote viwili. Nuru ya taa zile katika kinara cha mshumaa iliakisi katika mbao zilizokuwa pembeni mwa jengo hili zilizofunikwa kwa dhahabu na juu ya samani takatifu na mapazia yenye rangi ya kupendeza yaliyofumwa makerubi juu yake kwa nyuzi za dhahabu na fedha. Mwonekano ulikuwa wa fahari mno kupita maelezo. Hakuna lugha inaweza kuelezea uzuri, kupendeza, na utukufu mtakatifu ambao vyumba hivi vilikuwa vikionesha. Dhahabu iliyokuwamo katika patakatifu hapa iliakisi rangi za mapazia, ambazo zilionekana kama rangi tofauti tofauti za upinde wa mvua.PLK 56.2

    Mara moja tu katika mwaka kuhani angeweza kuingia katika patakatifu pa patakatifu, baada ya matayarisho makini na kwa uangalifu sana. Hakuna jicho la mwanadamu awezaye kufa isipokuwa lile la kuhani mkuu ambalo lingeweza kuangalia fahari ya chumba kile, kwa sababu palikuwa ni maskani maalumu ya utukufu wa Mungu ulioonekana. Siku zote kuhani mkuu aliingia mle kwa kutetemeka, wakati ambapo watu walisubiri kurudi kwake kwa ukimya ulio makini. Kwa dhati walimwomba Mungu kwa ajili ya baraka zake. Katika kiti cha rehema Mungu alisema na kuhani mkuu. Iwapo angedumu kwa muda mrefu isivyo kawaida ndani ya patakatifu pa patakatifu, kwa kawaida watu wangeliogopeshwa, wakihofu kuwa huenda utukufu wa Bwana ulikuwa umemwua kwa sababu ya dhambi zao au dhambi fulani ya kuhani mwenyewe. Lakini waliposikia sauti za njuga katika mavazi yake walifarijika sana. Kisha alitoka nje na kuwabariki watu wale.PLK 56.3

    Baada ya kazi ya hema ya kukutania kumalizika, “wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.” “Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.” Hema ya kukutania ilitengenezwa ili iweze kutenganishwa na kubebwa nao wakati wote wa kusafiri kwao.PLK 57.1

    Wingu Liongozalo-Bwana aliwaelekeza Waisraeli katika safari zao zote kupita jangwani. Wakati ambapo ilikuwa ni kwa manufaa ya watu hawa na utukufu wa Mungu kujenga mahema yao katika mahali fulani na kukaa pale, Mungu alionesha mapenzi yake kwao kwa kufanya nguzo ya wingu kusimama ikiwa karibu juu ya hema ya kukutania. Na ingebaki hapo hadi pale Mungu alipotaka wasafiri tena. Ndipo wingu la utukufu lilipoinuliwa juu ya hema ya kukutania, na ndipo wakasonga mbele.PLK 57.2

    Katika kusafiri kwao kote walidumisha utaratibu mkamilifu. Kila kabila lilibeba bendera yenye alama ya familia ya baba zao juu yake, na kila kabila liliagizwa kujenga mahema yake kando ya bendera yao wenyewe. Na waliposafiri, makabila mbalimbali yalisafiri kwa utaratibu, kila kabila chini ya bendera yao. Walipopumzika kutokana na kusafiri kwao, hema ya kukutania ilijengwa, na ndipo makabila mbalimbali yalijenga mahema yao kwa utaratibu, mahali pale hasa alipoagiza Mungu, kuzunguka hema ya kukutania, kwa mbali kidogo.PLK 57.3

    Watu waliposafiri, sanduku la agano lilibebwa mbele yao. “Na wingu la Bwana lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini. Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema: ‘Inuka, Ee Bwana, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao.’ Tena hapo liliposimama, akasema: ‘Ee Bwana, uwarudie maelfu kumi ya maelfu ya Israeli.’ ”PLK 58.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents