Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  14/Ukweli Unaendelea Uingereza

  Wakati Luther alipokuwa akiwaeleza watu wa Ujerumani habari za Biblia ambayo ilikuwa imefungwa, Tyndale alikuwa akifanya kazi hiyo hiyo huko Uingereza kwa uongozi wa roho Mtakatifu. Wycliffe alikuwa ameitafsiri Biblia kutoka kwa Kilatini, lakini ilikuwa na makosa mengi. Bei yake ilikuwa kubwa sana, kwa hiyo ilinunuliwa na watu wachache tu.TU 114.1

  Katika mwaka wa 1515 Agano Jipya lilikuwa limechapwa, ambalo lilikuwa limetafsiriwa kutoka kwa Kigiriki. Makosa mengi yaliyokuwamo hapo kwanza yalisahihishwa, na ikaeleweka wazi. Watu wengi miongoni mwa wenye elimu walisoma na kuuona ukweli wazi, na kuongeza nguvu kwa kazi ya matengenezo. Lakini watu wa kawaida walikuwa gizani kwa wingi kuhusu Neno la Mungu. Tyndale alipaswa kuitimiza kazi ya kutafsiri Biblia kwa lugha yao, kazi ambayo ilianzishwa na Wycliffe.TU 114.2

  Alihubiri imani yake bila hofu. Yale madai ya papa kwamba kanisa ndilo lenye haki ya kuisoma na kuieleza Biblia ni wewe uliyetuficha ukweli huu, na ni wewe uliyewachoma moto wale waliofundisha ukweli wa Biblia, na kama ungeweza ungeichoma hata Biblia pia.TU 114.3

  Mahubiri ya Tyndale yaliwachangamsha watu sana. Lakini mapadri walijitahidi kuiharibu kazi yake. Tyndale alisema, “La kufanya ni jambo gani?” Mimi siwezi kufika kila mahali, Oh, kama wakristo wakipata Biblia katika lugha yao wangeweza wenyewe kupinga ufedhuli huu. Pasipokuwa na Biblia haiwezekani kuwadumisha wakristo katika ukweliTU 114.4

  Kusudi jipya likazuka mawazoni mwake, “Je, Injili haitazungumza kwa lugha yetu ya Kiingereza kati yetu? Je, nuru ya kanisa iwe ndogo wakati wa adhuhuri kuliko wakati wa mapambazuko? Wakrsito lazima wasome Biblia katika lugha yao” Mtu ataufahamu ukweli kwa njia ya Biblia tu Tyndale alipokuwa akihojiana na mkatoliki ambaye ni msomi, alisema, “Tulikuwa heri bila kuwa na sheria ya Mungu kuliko papa. Namdharau Papa na sheria zake zote, na kama Mungu atanilinda niishi miaka mingi, nitawaelimisha watu, hata kijana mdogo mwenye kuchunga au mkulima atajua Biblia kuliko wewe”.TU 114.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents