Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Usahihi Wa Uwezo Wa Maandiko

  Kanuni iliyoshikiliwa na watengenezaji hao, ni ile ile iliyoshikiliwa na Waldenses, Wyclife, Huss, Luther, Zwingli na wenzao wote kwamba Biblia ni sahihi kabisa na uwezo wake ndio wenye kuongoza imani. Mafundisho yake ndicho kipimo cha madai yote. Imani ya watu hao kwa neno la Mungu, ndiyo iliwafanya kushikilia bila kuacha mpaka kifo cha kuchomwa moto. Latimer alisema: “Jipeni moyo, tangu leo tutawasha moto wa neno la Mungu kwa neema yake, katika Uingereza. Ndivyo nitumainivyo” maneno haya aliwaambia wenzake walipokuwa wanachomwa moto.TU 115.7

  Baada ya kupita miaka mamia tangu makanisa ya England yajitolee kufuata Roma, lakini makanisa ya Scotland yalidumisha uhuru wao. Walakini katika karne ya kumi na mbili Ukatoliki ukaimarika huko, na nchi ikawa gizani kamili. Lakini nuru ya ukweli ilikuwa ikilipenya giza hilo taratibu. Lolards alikuja kutoka England akiwa na Biblia pamoja na maandiko ya Wycliffe, alifanya mambo mengi kulinda ukweli wa Injili. Katika kuanza matengenezo walitumia pia maandiko ya Luther na Agano Jipya lililotafsiriwa kwa kiingereza na Tyndale. Wajumbe hawa walisafiri wakipanda milima na kutelemka mabondeni kimya kimya wakiwasha nuru ya Injili ambayo ilikuwa karibu kuzimika, na kujaribu kuharibu kazi ambayo kwa muda wa karne nne imefanywa na udhalimu.TU 116.1

  Mara ghadhabu ya Wakatoliki ikaamshwa na uchomaji wa waungwana wa Uskoch ukaanzishwa. Vifo vya mashahidi hawa viliamsha nia za watu kwa kuona jinsi walivyoushikilia ukweli mpaka kufa, ili kuupinga ufedhuli wa Rumi.TU 116.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents