Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maelfu Ya Wachungaji Walifukuzwa

  Katika karne ya kumi na saba, Wachungaji maelfu walifukuzwa na watu walikatazwa kuhudhuria mikutano yoyote ya dini, isipokuwa ile iliyoidhinishwa na kanisa peke yake. Wana wa Mungu wa kweli walikimbilia katika msitu, na huko wakakusanyika na kuomba na kumsifu Mungu wao. Kilichosababisha mambo hayo ni mateso. Wengi waliteswa kwa ajili ya imani. Magereza yalijaa tele na jamaa zilitenganishwa. Walakini mateso hayakuwanyamazisha. Wengi walikimbilia ng'ambo ya bahari mpaka Amerika, na huko wakaweka msingi kamili wa utengano wa dini na serikali, na uhuru wa kuabudu kila mtu kama apendavyo.TU 117.4

  Ndani ya gereza lililojaa wafungwa John Bunyan aliandika kisa chake cha ajabu, akijawa na mwamko wa mbinguni aliandika kisa cha safari ya msafiri kutoka katika nchi ya uharibifu kwenda katika mji wa raha. Maendeleo ya msafiri na neema nyingi mwenye dhambi mkuu, au kwa jina lingine “SAFARI YA MSAFIRI”; Kitabu hicho kimesaidia watu wengi wakafuata njia ya uzima.TU 118.1

  Wakati wa giza kuu la kiroho Whitefield na Weslyes walionekana kuwa wachukuzi wa nuru kwa ajili ya Mungu. Kanisa watu walikuwa wamepotoka sana, hata ilikuwa vigumu kuwapambanua na wamizimu. Watu wakuu waliwadhihaki wacha Mungu, na watu wa kawaida wakaachwa maovuni. Kanisa halikuwa na uwezo wa kuwasaidia walioangusha ukweli wa injili.TU 118.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents