Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuhesabiwa Haki Kwa Imani

  Fundisho kuu la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani kama ilivyofundishwa na Luther karibu limepoteza maana yake.TU 118.3

  Kanuni ya Warumi ya kwamba wokovu hutokana na matendo mema tu imekuwa badala ya haki kwa imani Whitefield na Weslyes walikuwa watafuta upendo wa Mungu kwa kweli. Wao walikuwa wamefundishwa kuwa upendo wa Mungu hupatikana kwa njia ya kuwa mwema na kushika kanuni na taratibu zote za dini.TU 118.4

  Wakati Charles Wasley alipougua na kuona kuwa kifo kiko karibu, aliulizwa aeleze tumaini lake la kupata uzima wa milele liko wapi. Jibu lake lilikuwa hili: “Nimemtumikia Mungu kwa uwezo wangu wote” Rafiki zake walielekea kutosheka na jibu hulo. Wesly alidhani kuwa hakuna kizuizi cha kupata fadhila za Mungu. Akasema, “Ni kitu gani kitanizuia kupata uzima?” Hakuna nilichobakiza. Hilo ndilo giza lililokuwa limefunika kanisa, likiwaelekeza watu kutegemea matendo yao mema ili wapate wokovu, badala ya kutegemea damu ya Mwokozi aliyesulubishwa.TU 118.5

  Baadaye Weslye na wenzake walifahamu kuwa sheria ya Mungu inahusu mambo yote, ya ama mawazo, maneno na matendo. Walipingana na utu wa kale ndani yao kwa maombi mengi na mashindano makuu. Waliishi maisha ya kujikana na kujitoa pamoja na unyenyekevu, wakishika kila kitu walichodhani kuwa kitawaletea maisha matakatifu yatakayowaletea fadhili za Mungu. Lakini ilikuwa kazi bure tu, hayo yote hayakuweza kuwapatia maisha ya utulivu wala kuwaondoa katika hukumu ya dhambi.TU 118.6

  Moto wa ukweli wa neno la Mungu uliokuwa ukizimika madhabahuni mwa waporotestant, ulipasa uwashwe tena kutoka katika kimuli cha zamani kilichokabidhwa na waumini wa zamani wa Bohemia. Baadhi yao walikimbilia Saxony, na waliihifadhi imani yao, Nuru iliyotokea kwa wakristo hao ilimwongoa Wesley.TU 119.1

  John na Charles Wesley walitumwa kwenda Amerika kama wahubiri. Katika meli waliyosafiria kulikuwamo kikundi cha Moravian. Dhoruba kali sana ilitokea, na John akakabiliwa na mauti. Akajisikia kuwa hajawa sawa na Mungu. Wajerumani wa Moravian walionekana kuwa na utulivu mkuu wa imani kuu kwa Mungu, hali ambayo kwa John ilikuwa ngeni. Baadaye alisema, “Nimewachunguza watu hawa kwa muda mrefu, nikaona utulivu wao na hali yao na sasa nina nafasi ya kujua kama wao hawana woga, kiburi, hasira wala roho ya kulipiza kisasi. Katikati ya nyimbo wakati ambao huduma inaanza, bahari ikachafuka, ikapasua tanga kubwa vipande vipande maji yakafunikiza meli na kumwagika stahani tukawa kama kwamba kilindi cha bahari kimetumeza. Kilio cha hofu kilianza baina ya Waingereza. Lakini Wajerumani waliendelea kuimba kwa utulivu. Baadaye nilimwuliza mmoja wao, ‘Je, ninyi hamkuogopa?’ Akajibu, ‘La namshukuru Mungu’. Nikamwuliza ‘Je, wanawake wenu na watoto wenu hawakuogopa?’ Akajibu kwa upole, ‘Wanawake wetu na watoto wetu hawakuogopa kufa’”TU 119.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents